Moja ya watu wa kuwa nao makini kuhusu mke wako ni dada zako

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,434
5,095
Kama mwanaume ndio au miongoni mwa waliofanikiwa kwenye familia, usipokuwa makini utagombanishwa na mke wako. Dada zako watajifanya wana extra caring ya kumzidi mkeo + majungu kibao.

Kuna muda ni wifu kuwa wao hawafanyiwi na waume zao unayomfanyia mke wako na wapo pia hawaoneshi caring kwa wae zao kama wanayoonesha kwako.

Usiwasuse wala kuwasahau ndugu zako kama we ndo mwenye uwezo ila wasikugombanishe na mkeo.

Lakini pia mke asikuteke na kukugombanisha na ndugu

NB: Hili halijanikuta mimi bado ila nayashudia vya kutosha.
 
Kaka akimuhudumia mkewe, mawifi wanasemaga kuwa mke kampa limbwata kaka yao.

Lakini kaka akiwahudumia dada zake wanasema ni sawa.

Lakini hao mawifi; waume zao wakihudumia dada zao wanaona, waume zao wanaendeshwa na dada zao.

Kila dada ni wifi kwa upande mwingine. Kifupi ni vigeugeu.

Ugomvi wa mke na wifi haukuwahi, hauwahi na hautakuja kuwahi kuisha.
 
Jamii zetu wanaume tunashukaka majukumu ya kimume ingali hatujawa waume. Unaanza kutafuta pesa ukirudi nyumbani hauna wa kuwahudumia zaidi ya dada zako na wadogo zako.

Kimbembe kinakuja unapoingia kwenye nafasi ya mume. Hao uliokuwa unawahudumia nafasi yao inahamia kwa mhusika hapo ndo ugomvi huanzia.

Maana watakuwa walishajihesabia haki ya kupokea kutoka kwako na wanahati miliki ya kipato chako. Wanyime uone!!!
 
Mke na wifi ni upinzani ambayo hauna kikomo sawa na vita ya israel na palestina, na sijuwi kwanini iwe kwa maskini au matajiri??
 
Back
Top Bottom