Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,770
- 10,650
Naomba kutofautiana nawe mkuu. Sio sawa binti anayejiheshimu kuzurura hovyo eti kutafuta mchumba. Tabia hii ndio inapelekea mimba za mapema na kukosa muelekeo kwa mabinti wengi. Kuna namna nyingi tu ambazo binti huonekana na mwanamume mwenye nia thabiti ya kuoa akavutiwa naye. Shughuli za kawaida za maisha mfano kwenda sokoni, dukani, kwenye ibada, harusini, kutembelea ndugu n.k. zinatosha kabisa kumtambulisha binti.Nafahamu kuwa Mabinti hutegemea wanaume wawatongoze ili kuanza kujenga mahusiano na baadae Ndoa. Ni sahihi kabisa.
.
Lakini, ukiwa kama Binti, unayo nafasi yako endapo mwanaume aliye sahihi atakufuata. Ukweli ni kwamba, kuna upungufu mkubwa wa wanaume bora ukilinganisha na mahitaji ya mabinti kuolewa.
.
Na Mtaalamu wa masoko yeyote yule atakwambia bidhaa yenye Uhitaji (demand) (m)kubwa hununuliwa sio na wale wanaostahili ama wenye fedha, bali wale walio fasta. Yaani wale ambao wako tayari kuchukua hatua kuipata bidhaa hiyo.
.
Hivyo, kama unahitaji Mwanaume bora, usiwe mtu wa kujifungia ndani all day.
.
Haitajalisha ni kwa kiasi gani utamuomba Mungu akupe Mume, Mungu hatamleta Huyo mume moja kwa moja nyumbani kwenu/kwako.
.
Hebu patikana. Kama umeenda kanisani, mnapomaliza ibada ongea ongea na waumini wenzako kidogo, sio ukitoka tu moja kwa moja nyumbani.
.
Kutana na watu, ongea nao, tengeneza network, acha kuwa serious na anti social kwa kujifungia fungia ndani.
.
Mungu hatamtuma huyo mume aje avunje mlango wa kwenu na kukushawishi Ndoa.
.
Hebu patikana, sali na angalia!
.
#SeeYouAtTheTop
View attachment 1168549
Habari ya kutoka matembezi ni chanzo cha kujiweka mdomoni mwa mamba. Wako wanaume wengi wanatega, wamejaa mistari ya kila namna, wanatafuta nafasi moja tu wafunge goli, na hao nfio wengi kuliko waoaji. Mwanamume aliyedhamiria kuoa hawezi kuchagua binti anayejitembeza mtaani, bali ataangalia sifa njema kama kutokuwa na mazoea na wanaume hovyo, na aibu ya kujichanganya kila mahali. Ukiona mwanamke hana aibu ujue unaoa mume mwenza, aibu ni sifa kuu ya mwanamke.
Mabinti wanaotaka waume wa kweli wasithubutu kuwatafuta, bali waendelee na maisha ya kawaida huku wakiepuka makundi ya marafiki wapenda starehe (viwanja) na kuwa karibu na wanaume ambao kiasili ni wapenda ngono kuliko kuoa.