Elimu mliyonayo mnajua iliandaliwa na watu gani? Hapo Mwanzo hakukuwa na darasa wala chuo na si miaka mingi sana, na hao waliobuni mambo haya na kuweka mifumo na taratibu hizi walikuwa kama Sugu tnea labda chini ya hapo kwa kipimo mnachotaka. Ni hivi, ufahamu wa mtu, hekima zake, busara zake, uwezo wa kuwasilisha kile anacho jua na kukiamini na kuwashawishi wingine kuwa ni kweli na kinawezekana, na kuweza kushiriki katika kuona kuwa kinatekelezeka ni elimu zaidi ya Profesa anaehubiri darasani na ukimpa Idara ya maendleo au shirika au wizara unashindwa kujua tofauti.
Tutapia uwezo wako kwa kile unachoonyesha kwenye jamii si kwa elimu uliyosoma darasani halafu unaishia kulalamika kunungúnika kila kitu unataka uwe umeandaliwa wewe ukija unakula tu, ikiwemu kuilaumu serikali, wazazi na jamii. Hiyo ni dalili ya kuwa umesoma lakini huna upeo yaani huna uwezo wa kuona opportunities au kucreate opportunitites. Kwa nyinyi mnaokaaa mjini nendeni kule vijijini makone vijana wanavyotengeneza pesa na wanaishi maisha so natural. Nyinyi mnaita maisha duni kwasababu ya televission ya mzungu, ila ikifika wakati mnaambiwa na Daktari unatakiwa ule hivi au utembee sana au usilale kwenye kitanda hiki ndo unashtuka alah kumbe wale jamaa wanaishi maisha mazuri zaidi kuliko sisi?
Mtizamo ni kitu muhimu sana katika kumjudge mtu, na kukurupuka bila kumpima ni udhaifu mbaya sana. amini usiamini mimi naweza kuwa nimesoma sana, lakini nikienda kijijini kuongea na wenyeji huwa kila siku najifunza mambo mapya kabisa mbayo sikuwa nayafahamu, na wenig wao hawajaenda shule kama mimi au kwenda ulaya na kwingineko.
Tutatumia vigezo vyako vya performance shuleni kama tunataka uwee mwalimu, na hilo halina ubishi, ila mara nyingi tumekuwa tukiwaalika watu kutoa mada na lecrure kwa wanafunzi si kwasababu ni ma-profesa au wana degree, la ila kwasababu ya ujuzi walioupata katika maisha na wakiongea uzoefu na ujuzi wao, mnaweza kuona kabisa jambo linalofaa kuimarisha katika elimu yenu.