Hizo ni hisia zako tu!
Mbona nchi zingine zina majenerali zaidi ya mmoja na hakuna ukosefu wa nidhamu unaofanya hayo majeshi yasiweze kutekeleza majukumu yake?
Hujaandika kwa kujua! Umeandika kwa kuhisi lakini ukajifanya unaandika kama unajua ilhali haujui!!!
Hivi wewe si ndo umetaka kujua kie usichokijua? Kwa nini udai hujui halafu ukipewa jibu unajifanya kukosoa, kwa hiyo uliuliza wakati unalijua jibu?
Siendeshwi kwa hisia, kama jibu hulitaki ungekaa kimya lakini ndio uhalisia. Tatizo hukuwahi hata kujiunga JKT ama kwa hiari (volunteer) au kwa lazima (compulsory) ukitokea kidato cha sita au kazini na kuishi ukafundishwa si chini ya miezi 12-36 ukatambua kwa kina nilichokieleza kinasadifu kitu gani.
Kama uliwahi kuwa JKT basi inawezekana ulikuwa 'Selure (mwenye upendeleo wa kipi upangiwe cha kufanya kutokana na ushauri wa daktari) na au Jongolisti (mtoro aliyepindukia)' hivyo kukosa nasaha na mafunzo ya kina ya medani.
Ili uthibitishe kwamba hizo ni hisia zangu jaribu kupendekeza sasa hivi awepo jenerali mwingine na awekwe ama JKT, Navy au Anga halafu usikilizie kitakachotokea baada ya muda hasa kwenye utoaji amri ya utekelezaji kuhusiana na jambo nyeti la taifa.
Jeshi halina siasa, lina amini kabisa kwamba raia wanachokifanya huwa hakizingatii utaratibu ndio maana zamani wakati unajiunga JKT, miezi mitatu ya mwanzo ilikuwa ni kuondolewa tabia na mitizamo ya kiraia iliyojaa ujuaji, kila mmoja ana la kwake kwa kulingana na alivyolelewa kimaadili katika familia au jamii aliyoishi
1. Kiburi cha kujiona kinafutiliwa mbali na unafunzwa utii kwanza na nidhamu
2. Uvivu unaondoshwa kwa lazima mpaka wewe mwenyewe unaanza kupenda kufanya kazi na ubunifu ulio nje ya taaluma uliyoenda nayo
3. Uvumilivu wa changamoto zozote zile na kutafuta njia sahihi kujiondoa kwenye mtego na kushinda kwa kutumia akili kabla ya silaha
4. Kufikiria usalama wa taifa na watu wake kwanza, maana ukujidai kuhurumia nafisi yako na ukataka kuiponya ili wengine waangamie wewe ndio utaondoshwa usije ukafanyika faida kwa adui.
Muundo wa jeshi la Tanzania umeundwa kwa kujifunza changamoto zilizojitokeza kwenye majsehi mengine ndio maana wanapoenda kwenye kamisheni za usalama wa umoja wa mataifa ndio jeshi linaloonesha nidhamu ya hali juu sana hadi sasa.