CUF hatutayumbishwa na nyodo zenu

CUF hatutayumbishwa na nyodo zenu


Wazo la UKAWA ni cuf hatakama wanatubeza. Kama mkifanikiwa kututukana tukashindwa kumbukeni bila sisi hakuna UKAWA.
Najua mtanikumbuka kwa hili.

Nashangaa kwa nini CDM na NCCR wanakibembeleza hiki chama ZNZ, futilia mbali tusonge mbele muda unakwisha.
 
Mkuu Prof,,Lipumba hapokei Simu inasemekana amekula PESA ila Maalim Sefu kawaambia wakijitoa UKAWA watajijua yy yuko na UKAWA

Mkuu Kumbe ndio hali halisi ilivyo ,sasa tegemeo langu la mabadiliko kupitia ukawa nipeleke wapi ???
 
Hii post mijitu ya ccm imetuma yenyewe na yanachangia yenyewe kiukweli ukawa wako smart so ccm tulien nyie c mumeleta tingatinga lenye kufanya kazi kwa nguvu bila akili ukawa tunawaletea akili kubwa yenye maono ya ufumbuzii.naona mnajitekenya wenyewe ccm ili kuonekane ukawa kunashida tulieni kwanza

Jibu muruwaa..akhsante
 
Ukawa walipompitisha bila mizengwe Maalim Seif kugombea urais Zanzibar hivi vikao vya cuf vilikaa lini kuridhia hayo maamuzi? Kama wewe ni mcuf kweli na unalete argument ya hivyo basi umefilisika kihoja.
Mkilogwa mkajitoa kwenye ukawa itakula kwenu. Someni wakati na kujua upepo wa mabadiliko unavuma kwenda wapi.
 
Ila umenena mie nilidhani UKAWA ni pamoja na wapambe kushabikia na kuelezana na kupanga mengi ya kuiletea ushindi, ila nao viongozi kukaa kinya na ahadi za kesho mara kesho kutwa zinatia watu mawazo mbalimbali na kuleta haya yote yanayoendelea sasa. Inasimitisha kwa nchi yetu
 
Ukawa walipompitisha bila mizengwe Maalim Seif kugombea urais Zanzibar hivi vikao vya cuf vilikaa lini kuridhia hayo maamuzi? Kama wewe ni mcuf kweli na unalete argument ya hivyo basi umefilisika kihoja.
Mkilogwa mkajitoa kwenye ukawa itakula kwenu. Someni wakati na kujua upepo wa mabadiliko unavuma kwenda wapi.

Mleta mada ana mapungufu. Hawa wanaoandika humu ni Watanzania na wanaandika kwa mitazamo yao. Hii ya kuja hapa JF na kuanza kulaumu CDM au NCCR ni ukosefu wa fikra. Mambo yao wayafanye ndani bila kujali kelele za nje. Wanachama wa CDM humu wanajulika kama akina Mnyika, Slaa na wengine lakini hatujaona wanasema kitu kuhusu CUF. Humu unaweza kusoma upepo unaendaje na siyo maoni ya vyama yakoje. Hawa CUF kama wa jambo basi wawambie Wananchi siyo JF!!
 
Wana CUF mna akili sana sikama hawa mazuzu hayana cha kupinga wala nn nikuburuzwa kama mkokoteni! lazima muamue jambo kwa kutazama mbele zaid na msijiingize ktk utawala wa miungu watu.TEAM WAZALENDO
 
Ukawa walipompitisha bila mizengwe Maalim Seif kugombea urais Zanzibar hivi vikao vya cuf vilikaa lini kuridhia hayo maamuzi? Kama wewe ni mcuf kweli na unalete argument ya hivyo basi umefilisika kihoja.
Mkilogwa mkajitoa kwenye ukawa itakula kwenu. Someni wakati na kujua upepo wa mabadiliko unavuma kwenda wapi.

Usiwe mpuuzi Maalim seif kachukua fomu na akawa mgombea pekee cuf. Zanzibar hakuna upinzani mbali ya cuf so hakukuwa na haja ya kupata baraka za ukawa.

Huku bara wote tunanguvu na uzoefu. Lazima tuchuane kidemocrasia na kuridhiwa na wanachama wetu.
 
Hapa kuna mengi ikiwemo kufail kupata nafasi ya urais je tutasongaje mbele? Kila tukitaka tujadili kwenye vikao kina mnyika wanasema tusubiri uchaguzi.. hii siri ya kusubiri kila kitu hapo baada ya uchaguzi ni ukosefu wa ukomavu.

Tulikubaliana kila chama kilete mgombea tuwapime ndipo tupendekeze nyie mnakuja na mtu anayekubalika... then tufanye study kujua nani anakubalika pande zote za muungano hamtaki... wabishiiii hadi mnakera.
 
Hapa kuna mengi ikiwemo kufail kupata nafasi ya urais je tutasongaje mbele? Kila tukitaka tujadili kwenye vikao kina mnyika wanasema tusubiri uchaguzi.. hii siri ya kusubiri kila kitu hapo baada ya uchaguzi ni ukosefu wa ukomavu.Tulikubaliana kila chama kilete mgombea tuwapime ndipo tupendekeze nyie mnakuja na mtu anayekubalika... then tufanye study kujua nani anakubalika pande zote za muungano hamtaki... wabishiiii hadi mnakera.
Nilidhani we CUF kumbe ni gamba.Pole.unachokiomba hakitafanikiwa.
 
Tuheshimiane Mkuu... Cuf ndiyo chama pekee ambacho hatujapata kashfa juu ya matumizi ya pesa pia rushwa... wengine issue ya pesa wamevurugana sana.


Mawhelu, wakati wanasaini makubaliano pale Jangwani, cuf hamkuwepo? Kwa hiyo habari ya UKaWA mmeisikia leo? Ina maan CUF kwenu suala la muda halina msingi?

Naomba uwe mkweli.

Halfu wewe ni mwanamke gani unatumia maneno ya low class namna hii? "siamini mtu mstaarabu ana weza kuongea neno "nyodo", wakati akiwasilisha hoja muhimu. Kwa mtindo huu, naona wewe huwezi kuwa unasema kwa niaba ya CUF halisi. Si ajabu kweli hukujua kama CUF ni member wa UKaWA mpaka hiyo juzi. Ndiyo ukaweka shinikizo la kuongelea UKaWA kwenye mkutano wa July 25 kwa kuwa kwako ni jambo jipya. Sishangai.
 
Kwanini profesa alivyo unda ukawa akuwashirikisha wanachama wake kwanza?amesubiri mapaka.anyimwe kugombea urais na ukawa ndio anaibuka na hoja kuwa lazima.ashikishe wanachama?
 
Ndugu wanajamvi, nimehuzunishwa sana na jinsi ambavyo CUF na viongozi wetu wamekuwa wakibezwa na kuzodolewa na wafuasi na washabiki wenzetu wa UKAWA.

Kimsingi suala la sisi kuamua kukutana na kuweka maamuzi ya kichama ndio msingi imara wa kidemocrasia. Chama sio mtu mmoja kama ambavyo mnapenda tuamini. Prof lipumba hayupo juu ya sheria ya cuf. Tunaongozwa na katiba na maamuzi yetu tunaheshimu matakwa ya watu wetu.

Kwamsingi huu hakuna sababu ya wanachadema/nccr kutubeza. Kwenu wenzetu mmebahatika kwamba mkiamua kitu wafuasi wenu wanafuata tu hatakama mnawaburuza. huku kwetu hatuishi hivyo so naomba mtuheshimu.

Mnasema sisi ni wadini wabaguzi nk... kama nihivyo why mliungana na sisi hamkujua? ndio maana tunapata shaka uthabiti wa nia yenu katika muungano wetu... huenda ni kweli mnataka kupanda kupitia sisi then baadae mtugeuke...

Please tuacheni tufanye vikao vyetu kama katiba inavyotaka.

Nangu Mahwelu

Bw. Mahwelu kufuata taratibu za chama haswa chama chenye wafusi ni jambo jema. Labda unisahihishe kama nitakuwa nimesahau hivi wakati huu umoja unaundwa kwa haraka kwa dhumuni la kuiokoa katiba mbuvu na ya hila isipitishwe mle bungeni m/kiti wenu alikuja kutoa wazo hilo kwenye chama na kikao cha kumruhusu kikakaa na kumruhusu?Na kama ilifanyika hivyo mbona kilifanyika haraka sana. Lipumba kama m/kiti mwenza ndani ya ukawa ndie alieweka tarehe 14/7 iwe tarehe ya kikao cha kumtangaza mpeperusha bendera wa nafasi ya uraisi hivyo ilitarajiwa kikao cha chama chake kumruhusu kiwe kimeshafanyika. Hata hivyo kikao cha kumpitisha kama mgombea uraisi wa cuf kilikuwa kimeshafanyika ina maana hakikumpa na uwezo wa kuchaguliwa na kuchagua ndani ya ukawa?.Mbona alishasikika mara nyingi akisema endapo hatachaguliwa yeye atamuunga mkono yeyote atakaechaguliwa ndani ya ukawa? Ilipofika tarehe hiyo wenyeviti na makatibu wa vyama washirika walihudhuria na majibu yao isipokua yeye na katibu wake badala yake kamtuma mwakilishi asie na maamuzi. Inasemekana uamuzi wao utatoka tarehe 25 sasa cuf waelewekeje ndani ya ukawa? Imani ya wananchi inazidi kupungua kadri ukawa wanapozidi kushindwa kumtangaza mgombea uraisi wao. Hapa ndipo linapoingia suala la COALITION OF THE WILLING.
 
Back
Top Bottom