Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,103
Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Februari 18, 2022 inatarajiwa kutoa uamuzi kama Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Washtakiwa wengine watatu wana Kesi ya Kujibu au Hapana.

Ile siku iliyosubiriwa ya kutolewa maamuzi kesi Mbowe na wenzake 3 kama wana kesi ya kujibu au hawana ni leo 18 Februari 2022 ambapo Jaji Tiganga anatarajiwa kutoa maamuzi hayo katika mahakama kuu ya Uhujumu Uchumi na Rushwa.

Kujua kesi ilipoishia fungua kiunganishi hiki: Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake. Tumaini Swila amaliza ushahidi. Mawikili wa Serikali wafunga Ushahidi. Jaji kutoa uamuzi 18/02/2022

=========

UPDATES


1230hrs: Freeman Mbowe na wenzake, bado hawajafikishwa Mahakamani. Kesi itaanza kusikilizwa saa nane za Mchana.

1330hrs: Freeman Mbowe na Wenzake wamefikishwa mahakani.


=========

Jaji ameingia Mahakamani Saa 7 na Dakika 55.. Yupo Tayari..

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na

  • Wakili Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka Mawakili Wa Serikali Waandamizi na
  • Wakili Tulimanywa Majige Wakili wa Serikali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja

  • Iddi Msawanga
  • Sisty Aloyce
  • John Malya
  • Edward Heche
  • Jeremiah Mtobesya
  • Nashon Nkungu
  • Fredrick Kihwelo
  • Dickson Matata
  • Michael Mwangasa
  • Seleman Matauka
  • Alex Massaba
  • Gaston Garubindi
  • Khadija Aron
  • Evaresta Kisanga
  • Maria Mushi
  • Paul Kisabo
Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya kutolewa Uamuzi Mdogo baada ya Upande Wa Mashitaka Kufunga Kesi Yetu tupo tayari Kupokea Uamuzi Mheshimiwa Jaji

Wakili Peter Kibatala: nasi pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kwa ajili ya Kupokea Uamuzi Mdogo

Jaji anaandika Kidogo Mahakama ipo Kimyaaa

Jaji kama ambavyo Mawakili Wame zungumza Kwamba Shauri lipo Mahakamani Kwa ajili ya Uamuzi Mdogo.. Na Uamuzi huu Mdogo upo tayari, Nafanya Chini ya Kifungu cha 41 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200, Ikitaka Kujibu Kama Washtakiwa Wana la Kujibu au Hapana

Jaji: Kupima Ushahidi, na angalia Kama Kuna chochote Cha Kuita Washtakiwa Waweze Kujitetea, Kama Mahakama ikiona Kwa Ushahidi Uliletewa Wana Kesi ya Kujibu, Watapata nafasi Ya Kujitetea, Na Mahakama ikiona Pia Kwa Ushahidi Uliletewa Hawana Vya Kujibu Basi Mahakama Itawaachia huru

Jaji: Kwa Mujibu Wa Sheria Kesi ya Mahakama Ya Rufani Phillip Vs Jamuhuri Kesi namba 217/2020, Mahakama Ilisema Kwamba Mahakama hii inakwenda Kutekeleza Jukumu hilo, Mahakama Kabla haijafika ni Vizuri iseme Washtakiwa ni akina nani na Wameshtakiwa Kwa Makosa Gani

Jaji: Washtakiwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe, Washtakiwa Wameshtakiwa Kwa Makosa Sita. Makosa ya Kula Njama Kutenda Vitendo vy Kigaidi Kwamba walivunja Kifungu Namba 4(3)i, 2(2), 9, na Kifungu cha 27 (c) la Sheria ya Uhujumu Uchumi

Shitaka la Pili Ni la Mshitakiwa wa Nne, anashitakiwa kwa Kosa la Kufadhili Ugaidi Kifungu cha 57, 62 Kosa Lingine ni Kushiriki Kikao cha Kula Njama Kutenda Vitendo Vya Kigaidi Hapa Wanadaiwa Kuvunja Sheria Kifungu cha 4(1) 3,5 na 57 ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi

Na Kosa la Tano ni Mshtakiwa wa Kwanza Peke yake Kukuta na Vifaa ambavyo ni Vya Kutendea Ugaidi, Anadaiwa Kuvunja Sheria Kifungu cha 6(1), 3(1)

Jaji: Maelezo ya Mashtaka ni kwamba Washtakiwa Wote Wanne Wanadaiwa Siku ya Tarehe 1 May 2020 wakiwa katika Hotel ya HAI, na Maeneo Mbalimbali ya Arusha, Mwanza na Morogoro, Walikula Njama ya Kutaka Kuchoma Vituo Vya Mafuta

Vitendo ambavyo Walikuwa wanataka Kuleta Hofu Kwa Watanzania, Katika Kifungu hicho hicho Washtakiwa Wanadaiwa Kula Njama Kutaka Kumdhuru Lengai Ole Sabaya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kwa Kutaka Kuleta Hofu na Taharuki Kwenye Nchi

Jaji: Mshtakiwa Namba Nne Katika vipindi Mbalimbali yeye Mwenyewe alitoa Fedha Mbalimbali Kwa Mshtakiwa Namba 1,2,na 3, Kama Sehemu Ya Kutaka Kufadhili Ugaidi, Vitendo ambavyo Vilikuwa Vilete Madhara Kwa Watanzania na Kuleta Hofu Kwa Watanzania,

Washitakiwa namba Moja, Mbili, tatu na Moja, Wanadaiwa Kushiriki Katika Vikao kwa nia ya Kutaka Kulipua Vituo Vya Mafuta Vitendo Vilivyo Lenga Kuleta Hofu Kwa Watanzania..

Jaji: Kosa la Tano ni Mshtakiwa Namba Mbili, Eneo la Rau Madukani Mshitakiwa alikutwa anamiliki Bastola aina ya Luger A5340 ambayo Silaha hiyo ililenga Kutumika katika Vitendo Vya Kigaidi,

Jaji: Kosa la Tano ni Mshtakiwa Namba Mbili , Eneo la Rau Madukani Mshitakiwa alikutwa anamiliki Bastola aina ya Luger A5340 ambayo Silaha hiyo ililenga Kutumika katika Vitendo Vya Kigaidi,

Jaji: Kosa la Sita Mshtakiwa Namba Moja ndiye anayeshakiwa Peke yake, Ambapo Mshtakiwa Namba Moja alikutwa anamiliki pair Nne za Suruali za JWTZ, pair Nne za Suruali za JKT, pair Moja la Shati la JWTZ, pair Moja ya Shati la JKT

Jaji: Kosa la Sita Mshitakiwa Namba Moja ndiye anayeshakiwa Peke yake, Ambapo Mshitakiwa Namba Moja alikutwa anamiliki pair Nne za Suruali za JWTZ, pair Nne za Suruali za JKT, pair Moja la Shati la JWTZ, pair Moja ya Shati la JKT

Jacket, Kofia Tano za JWTZ, overoli la JWTZ, Ponjol Ya JWTZ, ballet Mbili za Kofia za JWTZ, Beji Mbili za HASSAN HD, Renki Mbili Vyeo Vya Coplo Mali ya JWTZ, Kidaftari Cha 5Srar ambacho alikutwa nacho, Mikanda Minne ya JWTZ, pair Moja ya Soksi , pair Moja ya Rasketi ya JWTZ

Kakutwa na Wing Moja ambayo ni Beji ya Ku attend Mafunzo ya Parashuti, Kisu cha AK 47 CHA JWTZ, Vitu Vyote Vililenga Kutumika katika Matendo Ya Ugaidi.

Jaji: Washtakiwa Wote Waliposimamishwa Mbele ya Mahakama Walikana Makosa, Mbele ya Kaka Yangu Jaji Siyani (Jaji Kiongozi Walikana Mashtaka yao, Walikubali Tu Maelezo Yao ya Particulars). Walikubali Kuwa Waliwahi Kufanya Kazi Katika Kambi ya Ngerengere.

Jaji: Mshtakiwa Namba Nne (Freeman Aikael Mbowe) alikiri kuwa ni Mwenyekiti Wa Chadema na Kwamba alikamatwa Mwanza Nyamagana,

Jaji: Upande wa Mashtaka Waliongozwa na Mawakili Robert Kidando, Pius Hilla, Abdallah Chavula, Jenitreza Kitali, Nassoro Katuga, Ignasi Mwinuka, na Wakili wa Serikali Tulimanywa Majige.

Jaji: Kwa Upande Wa Utetezi walikuwa Mawakili 19.. Jeremiah Mtobesya na Nashon Nkungu wakimwakilisha Mshtakiwa wa 1, John Mallya Mshtakiwa Wa 2, Fredrick Kihwelo na Dickson Matata wakimwakilisha Mshitakiwa Wa 3, Peter Kibatala na Mawakili Wengine Wakimwakilisha Mshtakiwa Wa 4

Jaji: Mashahidi walikuja Walikuwa ni ACP KINGAI Kaaya Hafidh Mahita Madembwe Gladys Fimbari Luteni Denis Urio Swila Goodluck

Walileta Vielelezo, Silaha tab Bastola aina ya Luger A5340, Risasi Hai, Maganda Mawili Ya Risasi, Barua Kutoka Tigo, Mhamala Wa Fedha Kutoka TIGO, KYC, Barua Kutoka Kwa Marajisi, Certificate ya Handing Over ya Bastola, Seizure Certificate ya Kukamata Uniform za Mshitakiwa Wa kwanza, Barua ya Kamishina Wa Forensic Beaural, KYC ya 0784779944, KYC ya 0782 237913, Financial Transactions Riport ya 0787 555200, Financial reports Ya 0784779944, Taarifa Ya Uchunguzi kutoka Extraction Report, Simu Moja ya Techno labeled A, labeled B, labeled C, Lebeled D na Simu labeled H, Certificate of handing over ya Pistol, Certificate Ya Inspector Swila N Luteni Denis Urio.

Jaji: Upande Wa Mashtaka Wakati Wanasikikizwa, Upande Wa Utetezi Waliweza Kuingiza Kielelezo kama Maelezo Ya Justine Kaaya, Maelezo Ya Anitha Mtaro, Maelezo I a Shahidi Mahita, Maelezo Ya Shahidi Luten Denis Urio, Maelezo Ya Sostenes Swila Kama Kielelezo namba 5

Jaji: Katika Hatua hii ni Vizuri Kujua Kuwa Vielelezo Vyote Vilivyopokelewa kwa Upande wa Utetezi, Vilipokelewa Baada ya Mahakama Kufanya Kesi Ndogo.. Jukumu la Mahakama ni Kupitia Ushahidi Na Kuona Kama Kesi imetengenezeka.

Jaji: Kwa Mujibu Wa Maelezo ya DPP VS Philip Katika Ukurasa Wa 14, Na 15, Jukumu la Mahakama Kupitia Ushahidi Kuona Kam Washitakiwa wanayo Kesi ya Kujibu, Ushahidi Wa Maneno na Ushahidi Wa Nyaraka Kisha Kujibu Swali Moja tu, Kesi ya Upande Wa Mashtaka Kufunga imetengenezeka

Jaji: Mahakama ya Rufaa ilisema Kwamba, JAJI ANASOMA KINGEREZA

Jaji: Kwa Uelewa wangu ni Kwamba Katika Hatua hii katika Kungalia Washtakiwa kama Wana kesi ya Kujibu Mahakama Inatakiwa Kungalia Ushahidi Kwa Ujumla Wake.. Mahakama iangalie Ushahidi Wa Juu kama Uliletewa Kuna Kesi Ya Kujibu kisha Washtakiwa Waitwe Kwa ajili ya Utetezi..

Jaji: Katika Siku hizi Mbili, tatu, nimepitia Ushahidi Wote na Vielelezo Vyote 39 na baada ya Kupitia Vyote Maamuzi ni haya yafuatayo..

Mahakama iangalie Ushahidi Wa Juu kama Ushahidi Uliletewa kama Kuna Kesi Ya Kujibu kisha Washitakiwa Waitwe Kwa ajili ya Utetezi

Jaji: Naanza na Kosa la Namba Sita Kwa Mshtakiwa Namba Moja.. Anadaiwa alikuwa na Mali (Vifaa) Vinavyo Daiwa Kutendea Ugaidi, Kwamba akivunja Vifungu ambavyo nimeshavitaja Mali ambazo zilikuwa Nyumbani Kwake nimeshazitaja

Katika Kosa hili Ushahidi Uliletewa Mahakamani Katika Kosa hili, Walileta Uniform, Mahakama Ilikataa kupokea Vielelezo hivyo Kwa sababu Wakati wanakamata Walikula Misingi ya Kukamata Vielelezo hivyo Hapakuwa na Vielelezo Vingine hapo kuwa na Ushahidi Mwingine

Katika shtaka hili, Mshitakiwa Hana Kesi ya Kujibu, Na Mahakama imeenda Kuangalia Kuwa katika Kifungu hicho cha 21 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi,

Hakuna Jambo ambalo Mahakama Imeelekezwa isipokuwa Mahakama Imeelekezwa Kwamba Kama Sheria Ya Uhujumu Uchumi Hakuna Ulicho Kielelezo na Hakuna Maelekezo ya Sura namba 200 ya Sheria ya Uhujumu Uchumi..

Katika Kifungu hicho Mahakama umeona Hakuna Kesi kwa Mahakama Haiwezi Kuwaita Kwa Utetezi Bali wataachiwa.. Katika Kosa hili, Hakuna Ushahidi Wa Kufanya Mshtakiwa awe na Kosa la Kujibu na Mahakama Inamuachia huru Mshtakiwa Kwa Kosa hilo.

Jaji: Mahakama Imepitia Vielelezo Vyote Vya Upande Wa Mashtaka na Utetezi, Bila kwenda Ndani, Mahakama hii Inaona Upo Ushahidi Washitakiwa Wana Kosa la Kujibu, Kwa Maana hiyo Mahakama hii Imewakuta Washitakiwa wa 1, 2 na 3 na 4 Wana Kosa la Kujibu Kwa Makosa yanayofuata..

Kwa Maana hiyo Mahakama Inawapa nafasi ya Kujitetea na wanayo Haki ya Kukaa Kimya, Mahakama Inaruhusu Kufanya adverse Comment,

Jaji: Katika Hatua hii Kosa la Shitaka Moja la Sita Mshitakiwa Hana Kesi ya Kujibu, Kwa Maana hiyo nawaalika Kwamba not Kwa Utaratibu gani Wataamua Kujitetea, Kwa Maana hiyo NATOA AMRI

Wakili Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba Kujadiliana na Mteja wangu..

Jaji: na wengine Wote Mnaweza Kufanya hivyo Kwa Wateja Wenu sasa hivi

Mawakili wa Utetezi Wanaenda Kizimbani Kuongea na Watuhumiwa

Wakili Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji sijui Kama naruhusiwa Kuweka Maneno Kwa niaba ya Mteja Wangu..

Jaji: Kwa Kifungu hicho inaruhusiwa Kwa niaba ya Mshitakiwa

Jeremiah Mtobesya: Mshtakiwa Wa Kwanza (Khalfani Bwire), kwa shtaka Pili na la nne baada ya Kuwasiliana naye anategemea Kujitetea Chini ya Kiapo na Kuleta Mashahidi Watano pamoja na Yeye ni Wa sita..

Jeremiah Mtobesya: Mshtakiwa Wa Kwanza (Khalfani Bwire), kwa shtaka Pili na la nne baada ya Kuwasiliana naye anategemea Kujitetea Chini ya Kiapo na Kuleta Mashahidi Watano pamoja na Yeye ni Wa sita.., Na Kwamba atatoa Vielelezo Vitano Katika Ushahidi Wake

Wakili John Mallya: Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa 2 (Adamoo) Tumepokea Uamuzi Wa Mahakama, Na Makosa ya Kwanza, Pili na Nne na la Tano ambalo anashtakiwa Pekee yake, Anakusudia Kujitetea Mwenyewe Chini ya Kiapo na Kuleta Mashahidi 2 na Kuleta Vielelezo Vinne Katika Utetezi Wake

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu (Ligw'enya) Tumepokea Uamuzi wa Mahakama, Mshtakiwa atajitetea Mwenyewe Chini ya Kiapo atakuwa na Mashahidi Watano na Vielelezo Vitano,

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Mshtakiwa Wa Nne (Freeman Mbowe) atajitetea Chini ya Kiapo na ataleta Mashahidi 10 pamoja na Yeye Watakuwa 11 na Anategemea kutumia Vielelezo 20

Jaji: Baada ya hapa, nafahamu Kwamba Natakiwa Kutoa Nakala ya Mwenendo Wa Kesi, Kwa hiyo Nikipata Siku 7 natarajia Kuwa itakuwa tayari..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji nilikuwa napitia RULE 15 (2) the Economic and Bribe Crimes za Mwaka 2016, Moja ya Kanuni za Uendeshaji Wa Shauri hili, Pande zote Mbili zinatakiwa Kutoa Majina na anuani za Mashahidi pamoja na Orodha ambazo zitatumika Katika Kesi

Katika Shauri Dogo Wenzetu Upande Wa Utetezi Wakiwa wanafanya Uwakilishi Wa Pamoja, Waliorodhesha Mashahidi Wanne na waliomba Ruhusa ya Kuficha Shahidi Wa Tano, Walipewa Ruhusa Mpaka Pale walipohitajika Kukutwa na Kesi ya Kujibu Walipaswa Kutoa Majina.

Sasa Baada ya Kukutwa na Kesi ya Kujibu tulikuwa tunaomba Wenzetu Wakazingatia Rule 15 (2) ni Vema wa comply, Ni Vema Sasa Waseme Majina ya Mashahidi Kwa Minajiri ya Fairness ya Shauri hili..

Wakili Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kwa Kutokutaja Majina Imejielekeza Katika Kifungu cha Ulinzi Wa Mashahidi, Ukipata Jina na Usipomuita Utakuwa umepata Value gani? JAJI: wewe hayo Umeyatoa wapi?

Wakili Jeremiah Mtobesya: Ndiyo Maana Nasema tunaweza Kutaja Majina 100 na Tukaleta Mtu Mmoja atakuwa amefaidika nini?

Jaji: labda niseme Kwamba Je Kuna Amri ya Kuficha Majina ya Mashahidi?

Wakili Jeremiah Mtobesya: Ipo Ndiyo

Jaji: Ndiyo hiyo Ruling inasema hivyo?

Wakili Jeremiah Mtobesya: Vyovyote Vile itakavyokuwa, Mahakama Wakati Ule Ilitoa Rulling Wa Kujitetea Kwa Pamoja kwa Sasa labda Mahakama Irejee Maamuzi yake.

Jaji: Kwa sasa Ukitaja Majina Kuna tatizo?

Wakili Jeremiah Mtobesya: Ndiyo Kwa sababu Kifungu Cha Kutaja Majina ni Kidogo sana Mbele Ya Kifungu Cha Kumlinda Shahidi

Jaji: Turudi Kwenye Hoja ya Msingi, Je Mahakama Inaamua tu bila Kufuata Utaratibu? Mahakama Inafikiaje hapo Ndipo Uamuzi Ufanywe, Je Huo Utaratibu Umefuatwa?

Wakili Jeremiah Mtobesya: Sasa Mheshimiwa Jaji Tusomee Kama utaweza

JAJI: ambapo sasa Kwa Bahati Mbaya Sina hapa, Itabidi nikatafute. Au Kama Mnatu hakikishia Rulling inasema hivyo tuendelee..

Wakili Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Wenzetu hawajasema Kwamba tukitaja Mashahidi 100 akaja Mmoja Watakuwa wamefaidika nini

Jaji: kama Ambavyo Wao walitaja Mashahidi na hawakuwa wote

Wakili Jeremiah Mtobesya: Sasa Wao Wana Sheria Kabisa inawataka wao,, Naomba Kibatala anisaidie

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Hakuna Sheria inayotaka Baada ya Kuwa na Kesi ya Kujibu, tunatakiwa Kutaja Majina Mheshimiwa Jaji Mimi sikusudii Kutaja Majina Ya Mashahidi Wala Kutaja Anuani Zao, Wataje Sheria Ipi inayotubana hapa, Je tutazuiwa tusilete Mashahidi?

Kibatala: Wakati wa Commital tulisema Kwamba Mashahidi Wawili ni Wanajeshi Wanaogopa Kutajwa Kwanza kabla ya Ushahidi Kwa Ulinzi Wao, Sisi tumetaja Idadi na Hakuna Kinachotubana

Kibatala: Uamuzi wako (Jaji) Umesema Kwamba Tunatakiwa Kusema kama tutajitetea na Kuleta Mashahidi, Wala Hakuna Sehemu Ya Rulling Yako Kwamba tunapaswa Kutaja Majina na anuani Zao..

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji Nini Kimebadilika? Hakuna Kilichobaadilika baada ya Jaji Siyani Kuruhusu Mashahidi Wasitajwe

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Siku ile Ya Preliminary hearing walitakiwa Kutaja Mashahidi Wao,, Wakataja Shahidi IGP na Wengine

Jaji: Hoja ni Kwamba hiyo Rulling Haipo, na Je inasema Kwamba Amri hiyo itakuwepo Mpaka Baada ya Upande wa Utetezi Kufunga Ushahidi Wao, Je Ipo?? Ina ukomo? Kama Amri haina Ukomo itahamisha Kwamba Kutoka Mwanzo Mpaka Mwisho hawatotaja Mashahidi.

Na hii ni Kama Bado Upande Wa Utetezi Wakiwa Wanashikilia Uamuzi Wake,

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji huo ndiyo Msimamo Wetu na Tupo tayari Kufanya Submission

Jaji: Bado naahirisha nikaangalie

********************

Jaji amerejea

Jaji:
Nilisema nijiridhishe Kama Amri hiyo ipo, Kumbukumbu zinaonyesha Tarehe 10 September 2021 Upande Wa Utetezi ulitaja Mashahidi Saba, Ukaomba Mashahidi Wanne Msiwataje kwa Mujibu Wa Kifungu cha 21(4) Sheria ya Ushahidi Sura ya 367 ya Mwaka 2020

Ukizuka Ubishi, Baada ya Hapo Jaji alitoa Maamuzi Kwamba Kama Upande Wa Utetezi Utakutwa na Kesi ya Kujibu Amri itaisha, Kwa Maana hiyo Kama hamtaki Kuwa taja naomba Utaratibu Ufuatwe,

Wakili Jeremiah Mtobesya: Nimesoma Sheria ya Kuzuia Ugaidi, Sheria..

Jaji: Naomba Kusema Ilikuwa kama Amri hiyo ilitajwa, Lakini Kama Amri Imeisha Mtapaswa Kufuata Utaratibu, Hata hivyo Kama Amri hii Utaendelea Inawahusu Mashahidi Wanne

Wakili Jeremiah Mtobesya: Wakati huo Kibatala anazungumzia Upande Wote wa Utetezi, Sasa tumeshajigawa, Je Amri hiyo ni Valid katika Mazingira hayo?

JAJI: Mimi nakazia Amri ya Mahakama, Kwamba sasa Mmetaja Mashahidi 21

Jaji: Kama Nyinyi Mnahitaji Kuwalinda Mashahidi wenu basi Mui' move Mahakama ili Mahakama Ione itoe Muda au isitoe..

Wakili Jeremiah Mtobesya: Basi tunaomba Muda tushauriane

Jaji: Sawa Mawakili wa utetezi Wanakutana kama jopo

Jaji: Naona Maombi hayo yalikuwa in Common huenda yalikuwa ya Msingi

Wakili Jeremiah Mtobesya: Ndivyo hata Wakili wa Serikali Robert Kidando alishiriki Mheshimiwa Jaji

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji tunaomba tusimame Kidogo tutete Ofisini Kwako na Wenzetu wa Serikali

Jaji: Kwa Dakika ngapi

Wakili Jeremiah Mtobesya: Dakika 5

Jaji: Sawa, Kisha anasimama Kutangulia Ofisini Kwake

***********

Jaji amerejea

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile Vile kama awali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo Vile Vile.

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Baada ya Majadiliano Ya Maombi Iwapo au Lah Hitaji la Kutaja Majina na Anuani ni lazima Yatajadiliwa Siku ambayo Mahakama Itapanga Kwa ajili ya Washtakiwa watakapoanza Kujitetea

Ukizingatia Mheshimiwa Jaji Kwamba Nyaraka za Hukumu Ndogo na Nakala za Proceedings zitakuwa tayari baada ya Siku Saba, ambayo Tarehe 04 March 2022 ambapo Washitakiwa Wataanza Kujitetea.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi Kwamba Utetezi Waanze Tarehe 04 March 2022, Lakini pia yajadiliwe Maombi hayo Siku hiyo, Asante Mheshimiwa Jaji.

Jaji: Basi maombi ya ahirisho yanakubaliwa, Shauri kutakuja Tarehe 04 March 2022 Saa 3 Asubuhi, upande wa utetezi muwe tayari kuanza kujitetea, proceedings zitakuwa tayari baada ya siku saba,

Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya Magereza mpaka tarehe 04 March 2022 watakapoanza kujitetea, Baada ya maneno hayo naahirisha shauri hili.

Jaji anatoka nje ya chumba cha Mahakama
Wafuasi wa Chadema
 
Tujiandae kisaikolojia. FAM leo hawezi kuwa huru. Watesi wake bado hawajapata wanachokitaka toka kwake. Wanataka FAM awaombe msamaha kama mbinu ya kumuua kisiasa. Jaji tayari ana hukumu yake mfukoni na maelekezo mezani kwake.
Tujiandae kwa utetezi.
 
Tujiandae kisaikolojia. FAM leo hawezi kuwa huru. Watesi wake bado hawajapata wanachokitaka toka kwake. Wanataka FAM awaombe msamaha kama mbinu ya kumuua kisiasa. Jaji tayari ana hukumu yake mfukoni na maelekezo mezani kwake.
Tujiandae kwa utetezi.
Hatakaa afanye huo ujinga.. Yeye ndio anapaswa kuombwa radhi kwa kubambikiwa kesi mbaya ya ugaidi
 
Back
Top Bottom