Crazy things you did in secondary school

★Mimi hii ilinitokea kipindi nipo Form 4 (2012) ilikuwa Mocko Mkoa nikapiga Literature na English 20% kwa 22% na sio kawaida washazoea ni mtu wa 80~96 huko nikaitwa Staff nipigwe Collaboration nilipoona Fimbo zimezagazwa zakutosha na walimu wamekamia wanichape Nikaanza kutoa chozi nikasema Kipindi nafanya Mtihani nilifiwa na Wazazi wote wawili kwa ajari ya gari tena nalia haswa cha ajabu nilikuwa Boarding ko taarifa lazima zingeletwa waalimu bila kufikiri wakaachana na swala lakunichapa wakaanza kunipoza wakanipa na Rambi Rambi .
Kilichinisitua waliposema watangaze shule nzima wajue nikasema hiki kisanga sasa nikagoma nikasema ishapita achaneni nayo, nilipo enda likizo nyumbani nikamuomba MaMa samahani akauliza yanini nikamwambia nilikuuwa akasema kivipi? Nikajielezea Alicheka mpaka Kichomi kikamshika
nakumbuka nikiwa la std 7, afu ndo nilikuwa kati ya top 5 wanaotegemewa kubeba bendera ya shule.

Tukafanya mitihani, nikapata inglish 16% walimu walipagawa wakaniita ofisini wananishambulia wanataka kunichapa. Ile kuniuliza nimepatwa na nini.

Nikawajibu, Nimerogwa.

Ilibidi waniache maana nilikuwa nalia kama mfiwa.
 
★Nimekumbuka siku moja nipo Form 2 Boarding school tulikuwa tuna mtindo wakutoroka muda wa prepo mnaenda ku watch movies kitaa. Sasa mkiwa mnatoroka mfano mkikutana na Mwalimu hapo mnakuwa mmevaa nguo za nyumbani mnavunga kutembea style tofauti na za kawaida mwingine atatembea kama mchunga ng'ombe,kirema,Tahira ili kumchanganya tu mwalimu asiwafahamu maana Walikuwa wanakaa hapo hapo shule.
Kama kawaida za mwizi arobaini Wenzangu walinitangulia kuondoka baadae nikatoroka ile natoka tu maeneo ya shule Mala mbele yangu Headmaster huyo nikavunga kutembea kama kilema wa mguu mmoja kumbe keshanifahamu bwan:-
Headmaster-We si mwanafunzi wa Bweni?
Me-Ndio (nilijibu kwakuwa niliona keshanistukia)
Headmaster-Unaenda Wapi usiku huu wenzako wanasoma?
Me-Daftari limeisha na sabuni sikuwa na muda ndio nafuata hapo kibandani.
Headmaster-Sawa nenda uwahi kurudi.
Nikafurahi nikajua msara ushaisha ujinga na upumbavu wangu si nikajisahau nikatembea kawaida nikasikia sauti Bwana NtYga kesho uje ofisini (Tʖ̯T).
Sitasahau kipigo kile asee
 
Tulizinguana na kiranja mmoja mnoko sana yanii(labda ndo mana sa hivi ni afsa pale k/nyama) ...Akanchomea kwa displini masta,nkapewa kipande nchimbe shimo urefu wa yule kiranja...nkachimba for five days(nalegalega nsiingie klas). Sasa ule mchanga nlouto nkatengeneza kama kaburi na nkatafuta msalaba nkaandika jina lake nkauchomeka..nkaenda class, kama baada ya nusu saa tukaskia yowe kubwa uuuuuuuuwiiii jamani "kahawa ya njano" kaniuaaaaaaa.... Basi class zote zilizoskia zikatoka pamoja na walimu....

Kilichofuata ni SPAA na nlivorudi jina likaandikwa BLACK BOOK na viboooko vingi sana..

.na baada ya muda wakagundua tena mzazi nliemleta nimemnunua(mzee mmoja mishentown,)ambaye kwenye sekeseke lile alintoroka...

Ndo ukawa mwisho wangu pale kwenye ile shule ya KIKATOLIKI
aisee nmecheka balaa... kweli kahawa ya njano ulitisha sana kwahyo wazazi walivojua ikawaje baadae
 
Kuna jamaa alikua kani udi kidato Shule moja kule iringa, maarufu kama Nyomo guy yani ni mtemiiii balaaa, pande moja la mtu, na mm that time ndo kwanza Nipo form 1 alinishika kola ya shirt yangu, mm bila kumfaham nkampayukiaa “we kaka vipii” aisee alinikata jicho balaaa. Nkanyweaa bas kuja kufatiliaa kumbe alikua anantafuta anifahamu kisa bwenini kwao huko natajwaa na wahuni kila leoo

Nilkua na matatzo ya kusikia, bas siku wkt natembea DH npo stejini kule juu akatokea mvulana mmoja maskini aliniita akachokaa mm sina Habar. Nxt day naingia class nasikia naitwa Binti kiziwi nilmtafuta alientunga hilo Jina kuja kumpataaa namkuta jamaa mwenyewe mweusi tiiii nkamwambia acha dharau we black mambo, alinuna mwaka mzima but tukaja kua good friends ad sasa hivi.

A level Nilhama Shule from Moshi to Zoo (iringa girls) siku ya kwanza nareport dadeki nakuta form6 wanachapwaa stick za maana Yan wadada wanagalagala chini aisee nilmshka mama mkono nakazana kuhama na hii Shule, aiseee cjawah kuenjoy life ya pale zoo hata kduchuu.

Kuna siku kipindi cha mfungo wa ramadhan pale zoo Muslims huwa tunajipikia viaz. Ss hyo week kukawa na kamata kamata ya simu by this time Nipo form6. Kumbe form 5 wakishirikiana na baadh ya form6 walikuwa na mpango wa chnchn kumcharaza mwl yyte atakae kuja kukamata simu aisee Mwl Nazareth alicharazwaa gizani Ile kapata upenyo katorokaa basi nusu saa hii Polisi cjuiii ffu hawa hapa wakwanza kubondwa virungu ni sie Muslims maana tulkua karbu tu jmn nililiaaa mm dah hii shulee sutaisahauuu
pole sana...
 
kugombania ugali.
kuvamia madisco ya mitaani na kuchukua mademu za watu.
ligi za kula chakula kingi.
 
Nakumbuka miaka ya 2016 nikiwa form three miaka hiyo.......
Shule ya boarding senti kunani huko mkoani
Hile shule bana kulikuwa Kuna miratiba ya kusali Mara nne kwa siku yani hadi kanisa linakuzoea jina....
So mzee baba la baba Kuna siku nikaamua kudoji Yan kutokuenda church asubuhi nikaendelea tu kuvuta shuka kilichonipata duhh hatari.
Kama kawaida maticha wanoko hawakosi kuwepo kila shule wenyewe tunawaitaga watumishi wa wenye mbinu za kijeshi so ticha katimba room kaanza kukagua wasioenda kusali ... Baba la baba si nikavuliwa Kama samaki ziwa victoria Mara paaaah!
Nipo macho kwa macho na mtumishi wa sherikali. Akaniamsha wewe? wewe?.... nikavunga kimtindo si mnajua tena..... Nikaona isiwe tabu wacha nijifufue. Ticha akanihuliza mbona ujaenda church ? Nikamjibu naumwa kidole. Ticha alicheka kinoma yani Alf baba la baba nikawa serious kinoma
Akaona isiwe kesi akanihuliza jina unaitwa Nani? Nikamjibu naitwa Paul Joseph...
Kumbe teacheri ananipata kinoma akaniambie wew si unaitwa ..... Mtu fulan
Nilipoona nishaumbuka nikamjibu Hilo ni jina langu la utotoni hahahahahahah et twende stafu akamwambia father recta uku akiwa anacheka
Tokea siku hile nikapewa jina la bashite mpaka namaliza shule siku ya graduashen niliitwa bashite upo? Nikaitika nipo father uku nikienda kuchukua cheti.
Sitosahau mkasa huu
 
Karatu high school..... Muda wa kulala Kuna jamaa alikuwa anatoa ushuzi balaa siku ya makande sasa siku moja alijisahau akawa amazungushia kitanda chake Na shuka Ile kutoa ushuzi harufu ikamzidia ndani ya shuka jamaa akatoka nduki...toka siku hiyo alikoma tabia hiyo
ii ii
hahahaha bweni gani hilo mwongozo au mapinduzi.

sema Anney mchizi sana
 
nikikumbuka karatu boys tulileta mgomo kisa simu zikiwa zimebaki siku tatu tupige necta form six daah wakafukuzwa watu ilibaki kidogo na mimi nisifanye necta asee.
 
Nilishachajia watu simu
Nilikuwa na access na funguo za duka, kila nikijaribu kuwakatalia wananilazimisha dah.. na hivi nilikuwa na huruma basi najikuta nimewasaidia ila kwa sharti moja!siku wakikamatwa wasinitaje kabisa kama wanachajia huku.

Siku Moto ukawaka sasa,mmoja si akaropoka kuwa anachajiaga dukani..Tumbo lilipata joto.
 
Kipingu alikuja kua headmaster wa makongo sec years ahead
Kipungu alienda kuianzisha Makongo sec kwa maombi ya JWTZ baada ya mafanikio ya Jite(JKT)
Alikuwa Sports Master Jite, Umiseta Dar es Salaam 1993, Tulishinda Football( Chanzo cha Tambaza Sec kufungiwa), Tulishinda Basketball, Tulishinda NetBall na Volleyball, kimkoa(Dar) tukapelekwa kula bata Mikumi National Park, duuuhh!! Jite ilikuwa miaka hiyo
Naona sasa Colonel Massawe ni RC Kagera, na Kipingu alieenda kwenye uongozi mambo ya Mpira sijui
 
Mkuu Invisible unanifurahisha lakini ndio ukweli wenyewe. Disco likipigwa na mademu jamaa wanapagawa wiki moja kabla.
Haha mimi piah nimmoj wap kabla disco kale ka wik upol kama wote ili nipate nafasi ya kucheza na manz mzur
 
Haha Kuna cku nlifukuzwa ada,so kuna cool kids flani wakanishawishi tuende kwao,tulipofika tukaanza kupiga gambe nikazingua nataka kurudi shule. Dah bahati mbaya nlirudishwa sema mlinzi anafungua geti nakutana ana kwa ana na hedimasta..asee nlichezea fimbo na sasipensheni juu
 
Back
Top Bottom