Crazy things you did in secondary school

Tulizinguana na kiranja mmoja mnoko sana yanii(labda ndo mana sa hivi ni afsa pale k/nyama) ...Akanchomea kwa displini masta,nkapewa kipande nchimbe shimo urefu wa yule kiranja...nkachimba for five days(nalegalega nsiingie klas). Sasa ule mchanga nlouto nkatengeneza kama kaburi na nkatafuta msalaba nkaandika jina lake nkauchomeka..nkaenda class, kama baada ya nusu saa tukaskia yowe kubwa uuuuuuuuwiiii jamani "kahawa ya njano" kaniuaaaaaaa.... Basi class zote zilizoskia zikatoka pamoja na walimu....

Kilichofuata ni SPAA na nlivorudi jina likaandikwa BLACK BOOK na viboooko vingi sana..

.na baada ya muda wakagundua tena mzazi nliemleta nimemnunua(mzee mmoja mishentown,)ambaye kwenye sekeseke lile alintoroka...

Ndo ukawa mwisho wangu pale kwenye ile shule ya KIKATOLIKI
😂😂😂😂😂Haki nataman ingekuwa mchana niachie cheko kubwa khaaa watu mna matukio
 
★Mimi hii ilinitokea kipindi nipo Form 4 (2012) ilikuwa Mocko Mkoa nikapiga Literature na English 20% kwa 22% na sio kawaida washazoea ni mtu wa 80~96 huko nikaitwa Staff nipigwe Collaboration nilipoona Fimbo zimezagazwa zakutosha na walimu wamekamia wanichape Nikaanza kutoa chozi nikasema Kipindi nafanya Mtihani nilifiwa na Wazazi wote wawili kwa ajari ya gari tena nalia haswa cha ajabu nilikuwa Boarding ko taarifa lazima zingeletwa waalimu bila kufikiri wakaachana na swala lakunichapa wakaanza kunipoza wakanipa na Rambi Rambi .
Kilichinisitua waliposema watangaze shule nzima wajue nikasema hiki kisanga sasa nikagoma nikasema ishapita achaneni nayo, nilipo enda likizo nyumbani nikamuomba MaMa samahani akauliza yanini nikamwambia nilikuuwa akasema kivipi? Nikajielezea Alicheka mpaka Kichomi kikamshika
Yaani nyie watu,nimecheka kwa sauti kabisa! Eti mama nilikuua
 
Nilichokigundua ni kwamba Watanzania haswa vijana tulipokuwa shuleni basi tabia zetu, mienendo yetu karbia yote ilikuwa sawa, nakumbuka enzi za shule siku za disco, ni ubishoo hadi basi, siku za mikusanyiko za sherehe za dini, za shule na pale shule X ilipokuwa inakutana na shule Y kwakweli hali ilikuwa ni tofauti(RUGAMBWA SECvs IHUNGO SEC) kwakweli hapa siwezi kusahau tulipokuwa tunakutana.
Mkuu kumbe umepiga chata

"mastery for services"

IHUNGO BOYS HIGH SCHOOL
 
Rum six mido pale Soweto (Ujamaa) palikuwa si pakwenda kwa wale nyoya (wenye baa nyekundu moja begani - fomu wani!!) wadau nadhani mtakuwa mnakumbuka kwamba Ujamaa ni bweni lililokuwa likiongoza kwa kutrotisha (kuwasumbua) fom nyonya miaka yote! Ikiwa pamoja na kumwagiwa bichi (maji machafu), kupigwa chaga usiku au kuingizwa lokani).

Lakini kilichonichekesha zaidi ni kumkumbuka UNYAMA UNYAMA (ticha wa mota vehicle) aliyekuja Soweto kuamsha watu alfajiri siku moja akiwa mwalimu wa zamu, halafu akasikia sauti ikitokea floor ya juu kabisa ikimwambia "Unakuja kutumbusua asubuhi yote hii kwa sababu nyumbani kwako hapakaliki, wakati wenzako wanachagua wake wazuri wa kuoa we ukachagua kipori, matokeo yake unashindwa hata kulala nyumbani kwako" UNYAMA UNYAMA akajibu "Wewe unaeongea hivyo kama kweli ni mwanaume na unajua wanawake wazuri kuliko mimi shuka hapa chini tuonane"

Kituko kilikuwa kitamu yaani mpaka ilibidi jamaa waigize siku graduu!!

Ebwana nimekumbuka mambo mengi sana,

Big up sana kwa mameni KABOTA, MAGERE, MSASA, KATUNZI, mzushi TETE, KAMEME, mchungaji ISHENGOMA.
Ah ah aha h nimecheka sana
 
Ah! Azaboy, ubabe ubabe nlikutana na konda mbavu nkaipandishia kibezi af na mwili mdogooo, konda akatupa ngumi nkakwepa nikazama mfukoni nkatoka na buk10 nkaichana chana, kuna mjeda pembeni kanidaka "unachana pesa?" Kantia bonge la kofi dah nlichoropoka mbioooooo dadadekiiii
 
Nakumbuka kipindi nipo form1 nilikuwa Mzee wa kudodge vipindi mda mwingine naenda kucheza kamali na washkaj. Basi kuna siku tulienda kudodge na washkaj tukasahau muda wa kurudi kuitika jina washkaj nlioongozana nao waislam mm na jamaaang m1 ndo wakrsto bac tukakubaliana twende msikitini kufika kule yule mkrsto mwenzang akaenda playstation me nkaingia msikitini washkaj wakanambia niwaige wanachofanya bac ikawa wakiinama nainama wakipiga magoti napiga wakiangalia pemben vyote nafanya. Tumerudi class madam akatuulizia tukasema tulikuwa masjid madam akanikomalia mm muongo me c mkrsto akanambia twende assemble nkakupe adhab daah nkasema assemble kudhalilishwa mwenyw uongo nkampanga madam tulikuwa wakrsto wawl yule jamaa alikuwa anaitwa said Lakin ni mkrsto alivyoulizwa we mkrsto alivyokuw muoga akakubal bac tukaenda assemble ila madam alitupigisha attiz attention bac akatusamee.

Ila Kamar tumecheza sana tena akiwepo ticha wa field tunacheza mpk class. Sometime madam wa field akiwa anafundisha tunampiga vitunda vya ubuyu kwenye makalio akigeuka tunamcheka apo ni ss tu watu wa backbenchers. Hyo yote form1
 
Form 2 kufika kamali na matukio mengin yakaendelea nakumbuka tulishawah kutembeza daftal la rambirambi kwa msiba usio wa kwl na watu wakatoa.

Kulikuwa na mwenzet alikuwa mwizi kinoma kuna day tukamuibia na yy cowbell yake alitangaza fom2a mpk f kuwa kaibiwa. Kuna siku tulikuwa tunamtania mshkaj m1 hv kama tunamkaba mm na uyo jamaa mwizi weee! Jamaa akamchomolea hela yake(elf5) kwl akakimbia nayo hakuja wiki nzima. Nachoshkru nilikuwa na akil kila mtihan ukija nmeperform vzr toka form1 mpk madam akawa ananifatilia ananipa sana wosia nitulie me wap.

Form2 kuna washkaj zng walienda kufanya ugomv shule nyngn walokamatwa wakataj majina fake m1 alikuja kujulikana akapewa SPA nkaenda kumpa pole mida ya saa 4 hyo baadae break kengele ya break imeish me nkabak nacheza kamar nakuja kushtuka saa6 naenda class nkakutana na madam NA ticha wakanipeleka staff wakanipiga wakanpa SPA na mm nkamfata mshkaj wangu tulopew wote SPA kwenye Kamar tukaenda Kwny harusi maeneo ya jiran na shule tukala mpunga then tukarud makwetu kutumikia matatzo yalotukuta

Ila nlifaul kwenda Advance mm tu wenzang wote walifel l.Advnc matukio yaliendelea mpk kuna day tulirudishwa home na difenda mkuu alituchoka

NB:JKT na Chuo nilitulia sana mpk Sasa.
 
Back
Top Bottom