Crazy things you did in secondary school

Dah ilikua form 2 nilisema kwa cube members wangu kuna kiatu cha jamaa mmoja Wa form six kinanuka ,wakaenda kunisemea ,kumbe jamaa alikua mtabe na anaheshimika kindakindaki ,muda Wa jioni unaingia kaanza kunitafuta dormitory ,nlienda kulala juu ya mti mpaka asubuhi nikanyoosha kwa headmaster kwa usalama wangu ,asubuhi naona jamaa anakuja kwenye office ya headmaster huku anapiga mluzi halafu katabasamu
Headmaster mwenyewe anazima fegi kwa jamaa akaniombea msamaha ,kweli jamaa akawa kaka wangu Wa shule hakuna aliyenionea Tena ,sema ndio hivyo kumfulia, anakupa sh 50 umletee mkate,soda na change ibaki ,ukiletewa nido sijui na blueband unanyoosha moja kwa moja kwake
Mkuu nimecheka hadi machozi.
 
Azania nadhani 2009 kuna dogo wa o level aligongwa akafa sasa zilikuwa zikipita daladala za tandika - muhimbili konda anashushwa ana kula kichapo basi ikawa fujo balaa sasa o level wanavaa suruali za blue kama za makondakta kuna dogo mmoja katika purukushani akachukua koti la konda akalivaa bila kujua katokelezea kama konda na suruali yake basi ile kajichanganya wakashindwa kumtambua ndani ya muda mfupi akale krebu za kutosha ile kaja kuvua kabaki na t shirt ya shule tayari ana nundu za kutosha
 
Ndanda boys hiyo watoto wa masasi girls wanakuja kwa ajili ya disco kipindi hicho kwenye holl letu likiiitwa MV Bukoba

Baada ya kuonekana kuna ugomvi wa kugombania vimwana watu wanachagua vimwana wakali ikabidi iwekwe sheria....demu anaaacha pair moja ya kiatu nje baharia anakichukua akiingia demu akigundua ndio kiatu chake basi atacheza na msela mwanzo mwisho basi kuna wana walikuwa na videmu vyao tayari so mademu wakifika wana wanawapa ndala then viatu mtu anachukua kimoja anampa demu kingine anakiweka mfukoni si unajua kipindi hicho mi jeans yetu ile bonge la dude lina bonge ya mfuko basi mzee baba high heel inakaa na haionekani lengo tu kimwana wako asibebwe
 
nakumbuka mwaka 2005 wkt npo kidato cha 4 ktk shule inaitwa Bismarck ipo mkoan Mwanza nlizushiwaga natembea na mwalim wang wa masomo ya biashara eti kisa kila pepa ya Book keeping na Commerce nlikua naongoza mim, pia nakumbuka mwaka 2007 wkt npo kidato cha 6 ktk shule ya wavulana ya Azania nlimpgaga ngum dereva wa daladala ya Temeke/Muhimbil baada ya mwanafunz wa kidato cha kwanza kusukumwa na kufarik, yan iyo fujo yake haikua ndogo kwa maana wanafunz wa Azania 2lizagaa ktk vitua shaz kufanya fujo

Aisee bro una hatari wewe kumbe kipindi hicho Ulikuwa ECA pale vipi mlipendelewa sana nyie kupewa hostel sijui kwann
 
Ivi jamani hakuna app mpya kama ya dent jamani hahahaha nimeimiss dent app;)
 
Azania nadhani 2009 kuna dogo wa o level aligongwa akafa sasa zilikuwa zikipita daladala za tandika - muhimbili konda anashushwa ana kula kichapo basi ikawa fujo balaa sasa o level wanavaa suruali za blue kama za makondakta kuna dogo mmoja katika purukushani akachukua koti la konda akalivaa bila kujua katokelezea kama konda na suruali yake basi ile kajichanganya wakashindwa kumtambua ndani ya muda mfupi akale krebu za kutosha ile kaja kuvua kabaki na t shirt ya shule tayari ana nundu za kutosha
uwiiiiii
 
Kuna jamaa alikua kani udi kidato Shule moja kule iringa, maarufu kama Nyomo guy yani ni mtemiiii balaaa, pande moja la mtu, na mm that time ndo kwanza Nipo form 1 alinishika kola ya shirt yangu, mm bila kumfaham nkampayukiaa “we kaka vipii” aisee alinikata jicho balaaa. Nkanyweaa bas kuja kufatiliaa kumbe alikua anantafuta anifahamu kisa bwenini kwao huko natajwaa na wahuni kila leoo

Nilkua na matatzo ya kusikia, bas siku wkt natembea DH npo stejini kule juu akatokea mvulana mmoja maskini aliniita akachokaa mm sina Habar. Nxt day naingia class nasikia naitwa Binti kiziwi nilmtafuta alientunga hilo Jina kuja kumpataaa 🤣🤣🤣 namkuta jamaa mwenyewe mweusi tiiii nkamwambia acha dharau we black mambo, alinuna mwaka mzima but tukaja kua good friends ad sasa hivi.

A level Nilhama Shule from Moshi to Zoo (iringa girls) siku ya kwanza nareport dadeki nakuta form6 wanachapwaa stick za maana Yan wadada wanagalagala chini aisee nilmshka mama mkono nakazana kuhama na hii Shule, aiseee cjawah kuenjoy life ya pale zoo hata kduchuu.

Kuna siku kipindi cha mfungo wa ramadhan pale zoo Muslims huwa tunajipikia viaz. Ss hyo week kukawa na kamata kamata ya simu by this time Nipo form6. Kumbe form 5 wakishirikiana na baadh ya form6 walikuwa na mpango wa chnchn kumcharaza mwl yyte atakae kuja kukamata simu aisee Mwl Nazareth alicharazwaa gizani 😂😂🙌🏽 Ile kapata upenyo katorokaa basi nusu saa hii Polisi cjuiii ffu hawa hapa wakwanza kubondwa virungu ni sie Muslims maana tulkua karbu tu jmn nililiaaa mm dah hii shulee sutaisahauuu
 
😂😂😂
 
Na siku ya kula wali unavaa nguo za mapigano. Uji ukiwa hauna sukari na maharage yamejaa wadudu lakini mnagombania!
Big up hii nimeifanya sana Kahororo Secondary Bukoba, nadhani tulikuwa wote! sufuria inapigwa juu kwa juu! punje za Dona zinamwagika lkn zinadakwa zote kijanja, iliitwa ''scrumble'' ilikuwa inatokea km wapishi wameiba sana Unga waugali na kupikia maandazi maarufu bukoba ''Vibaragara''

Wageni wetu maarufu ni kutoka Rugambwa Sec school, hapo mtapika mpaka basi! utaombwa mtembelewe!
 
Kutengeneza Rafiki Muislamu kwa nguvu zote km Zefania Yakobo, Adalah Nyekobora, ili ufaidi Daku na Futari ya waislamu wakati wa mfungo wa Ramadhani.

Matajiri waislamu wa Bukoba mjini kama Kugis, walikuwa wanawafturisha wanafunzi waislam si kawaida.

Sijui bado ni hivo hivo au wameacha siku hizi? daaa! safisana, siyo km mzee Mohamed maneno meeengi!
 
Hivi yule kiranja wa Bwalo mnoko sana anaitwa TURUHAGA BABISHAKIRAO yuko wapi? alitusotesha sana huyu jamaa, Form one maarufu km wagogo tulideki Bwalo kwa migongo tena usiku! Mshenzi sana yule jamaa! hawa viranja hawa? nyoko sana!

Mwanya Ramsi alikuwa mstaarabu nitafute upige maji bure!
 
Nakumbuka galanos sec tanga tulitotoka Na washkaji watatu,tukazamia kwenye harusi mtaani ,watu kibao wa ukwel plus totoz za kifa mtu bhas kwenye msosi kila mtu Na kadi yake(kumbuka tulizamia,),tukasema kwenye foleni tukae mbalimbali means mmoja nyumba mwingine katikati Na mwingine mbele(kumbuka hatuna kadi),Kwa kiherehere changu cha msosi nilikuwa wa mbele.
Nafika pale naulizwa kadi ipo wap najidai bubu af msosi unanukia kinyama(mambo ya kitanga,nikawekwa pembeni
Washkaji wakashtuka lkn hawawez kutoka coz geti zote zimefungwa ili wazamiaji wasiingie(sherehe za uswahilini kimtindo)
Baada ya dkka 5 msela wangu nae kapigwa ban ,hapo siongei wa kucheka coz mm ni bubu Ila kicheko kinakuja hadi machozi yanakaribia kutoka
Baada tena ya dkika5 msela nae kapigwa pembeni.
Wenye harusi wakaanza oh oh mnatutia aibu sijui nini Na nini ,mwishowe wakasema tukiendelea kusimama pale ndio tunawatia aibu mara dufu so tupitishwe Kwa mlango wa nyuma ambapo huku kuna masufuria.
Kufika huko tukakuta vitu vya kumwaga(misosi)
Dah huwez amini ububu ukaisha ,piga kinyama then tukaweka kwenye mifuko had skonga tukaingia prepo kila mtu alionja ,nikikumbuka mbavu sina
Msocha hakuwakamata kweli?
 
Tulizinguana na kiranja mmoja mnoko sana yanii(labda ndo mana sa hivi ni afsa pale k/nyama) ...Akanchomea kwa displini masta,nkapewa kipande nchimbe shimo urefu wa yule kiranja...nkachimba for five days(nalegalega nsiingie klas).

Sasa ule mchanga nlouto nkatengeneza kama kaburi na nkatafuta msalaba nkaandika jina lake nkauchomeka..nkaenda class, kama baada ya nusu saa tukaskia yowe kubwa uuuuuuuuwiiii jamani "kahawa ya njano" kaniuaaaaaaa....

Basi class zote zilizoskia zikatoka pamoja na walimu....

Kilichofuata ni SPAA na nlivorudi jina likaandikwa BLACK BOOK na viboooko vingi sana..

.na baada ya muda wakagundua tena mzazi nliemleta nimemnunua(mzee mmoja mishentown,)ambaye kwenye sekeseke lile alintoroka...

Ndo ukawa mwisho wangu pale kwenye ile shule ya KIKATOLIKI
 
Nakumbuka nipo AZANIA SEC ,,
kipindi hicho asubuhi tunapewa SKONS NA CHAI....
basi ikifika SAA NNE ,,tunajisogeza canteen kwa ajili ya kupata skons,,

monitor anakwenda dirishani anatoa ID anakabidhiwa fuko la mikate ,
nakumbuka ilikuwa scons flani za njano njano hivi...basi kichekesho ni kwamba,,
darasa zima lilikuwa na wanafunzi 37 hivi..
lakini Mara nyingi huwa halitimii wote,,,
tunakuwa wengine hawana muda wa kusubiri scons,,
muda wa break wanakimbilia nje kwenye mihogo ya kukaanga na juice za ukwaju..
kwahyo sometimes tunakuwa wanafunzi kumi au si zaidi ya 15... Lakini scons tunapewa idadi ile ile 37 hata kama tupo wawili ,,,

Sasa basi yule monitor ataanza kugawa scons,,
kama watu watatu wanne hivi,,
halafu fujo zinaanza kugombea ule mfuko wa scons,,

yaani vumbi tupu..
sasa ukiuliza chanzo cha fujo ni nn? wanasema scons za kupewa bila kugombea zinakuwa sio tamu,,

duu..basi baada ya fujo zile za kugombea scons kwisha,,
ndy baadhi ya wanafunzi wanapata head lines za kwenda kuandika ubaoni,,
mfano amng'ata mwenzie sikio wakigombea scons,
,halafu wanaacha hivyo ubaoni,,
basi mwalimu akija anaona yaliyoandikwa pale ubaoni ,,
na baadhi ya wanafunzi wamejaa vumbi tupu.
tena ule udongo mwekundu..
basi darasa zima ilnakuwa ni vicheko,,
kumcheka yule aliyekosa,,au aliyechafuka na vumbi wakati wa kugombea scons..
Dah,,,aisee shule ni kipindi cha mpito.....
na siku tusipogombea mikate wanasema ya le sio mitamu kabisaa...
 
hahahaaa mm nakumbuka mwaka 2008 niko form 4 galanos tanga, kuna mwalim mmoja alikuwa anaitwa macmaster Luziro, alinidaka mtaani..., Sasa akajifanya mjanja et ananiita ananiuliza kijana unasoma wapi, nikamwambia nguvumali sec. Akasema bas nimekufananisha na mwanafunz wang nilimfundisha Ecknford.., Nikamuambia umenifababisha... Sasa hapo wote tukawa tumedanganyana wakat mm nilikuwa namsoma...

Ila alikuja akajua akaniambia we dogo ulinichezea sana akili
Umenikumbusha mbali saaana.

Mac master alikuwa anatoa hotuba zake siku ya jumatatu yani kila siku anatykumbushia you cant change galanos. But galanos will change you.

Kuna jamaa yule alikuwa mwalimu wa physics o level mlevi hivi. Yani siku moja alitunyaka tunatoroka mtu kama nane hii njia ya msikitini akatuambia sasa mnatoroka wengi hivi then shule inabak na nan??

Haya akawa akikupoitn unageuka unarud shule huk akipoint mwingine anaendelea na safari

Mtu nne zikarudi. Mtu nne zikaendelea kutooroka.

Kuna kipind kuna jamaaa walichanga hela wakanunua mfuko wa sukari kilo 30. Yani watu wote siku za kande walikuwa wanajaaaa bweni la chai. Kugongea sukari.

Nakumbuka hata week haikuisha.sukari ikaisha.
 
47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom