Crazy things you did in secondary school

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,876
~ Got chased by the headteacher and deputy head. A whole crowd of us in school uniform were in one area our school had forbidden to enter, otherwise could result in expulsion. Only 2 were caught; thank God I was not part of the two.

~ You used my camera to take photos of your sleeping friends, especially when they were drooling and posted it on the announcement boards.

~ Used to sneak out of school all the time as a day student and buy foodstuff that were all contraband.

~Would go to the dining hall before the lunch bell goes.

~ Used to write lyrics of the artists of your preference. (remember 2Pac, Bob Marley?)

~ Ulizoea kujiandikia barua ili uonekane wewe ni mpokeaji mzuri wa barua.

~ Ukitumiwa EMS au TMO basi wewe unaonekana baab kubwa!

~ Kuchomekea shati ilikuwa kero kwako, ulifanya hivyo wakati wa kukaguliwa Jumatatu baadaye 'unapiga chini'.

~ Kufua soksi ilikuwa kero sana kwako, ulikuwa unazivaa mara 5 kwa wiki kisha unazifua Jumamosi (ukiwa na pair moja).

Hizi ni baadhi, tena nyingi ni kwa upande wa wanaume. Ladies, tell us what you used to do (crazy ones pls).
 
Tehe tehe Tehee! Mkuu, mbona umenikumbusha mbali!

~Kwa kuwa mgao wa nyama mezani hautoshi, na nyama zenyewe ni mara moja kwa wiki, basi kiranja wa Bwalo akigeuka tu pembeni, umekwapua nyama kwenye dishi la msosi na kutia nyama kadhaa kwenye mfuko wa suruali !!! Kwikwi kwi...!
 
~Hata hizo barua unazojiandikia mwenyewe, hununui stamp hata siku moja! Stamp inafutwa muhuri na kutumika mara kadhaa! I think Shirika la Posta na Simu (jina la enzi hizo) halikupata chochote kwa barua kutoka mashuleni!
I see tulofanya hivi tupo wengi sana. Nilikuwa nikipata barua basi najua 'deal' hilo. Stamp itatumika kwenda kwingine... Ufisadi ulianzia huku :)
 
~Ulitengeneza water heater kwa kutumia spring za vitanda. Usiku wa manane unachemsha mahindi ya shamba la shule. Container la kuchemshia mahindi ni plastic la nje la chupa ya chai iliyoondolewa flask yake, inashikiliwa upside-down, i.e mfuniko ndo unakuwa base, na bottom yake inafunguliwa kuwa ndo mdomo wa 'sufuria' lako. Heater inawekwa kwanza katikati, then mahindi yanakatwa vipande na kupangwa around the heater.

Ukimaliza kuchemsha unarudisha waya wa umeme juu ya dari ambako ndiko connection ilikofanyika, kwani ni marufuku kutumia umeme wa socket!
 
~Ulitengeneza water heater kwa kutumia spring za vitanda. Usiku wa manane unachemsha mahindi ya shamba la shule. Container la kuchemshia mahindi ni plastic la nje la chupa ya chai iliyoondolewa flask yake, inashikiliwa upside-down, i.e mfuniko ndo unakuwa base, na bottom yake inafunguliwa kuwa ndo mdomo wa 'sufuria' lako. Heater inawekwa kwanza katikati, then mahindi yanakatwa vipande na kupangwa around the heater.
Ukimaliza kuchemsha unarudisha waya wa umeme juu ya dari ambako ndiko connection ilikofanyika, kwani ni marufuku kutumia umeme wa socket!
Ha ha ha,

Yani wewe umenirejesha enzi hizo kwelikweli. You kill my nerves!
 
Mkuu Invisible unanifurahisha lakini ndio ukweli wenyewe. Disco likipigwa na mademu jamaa wanapagawa wiki moja kabla.

Kwa shule za madume unaongelea wiki moja tu? Hata mwezi mzima mzee. Siku hiyo ni hatari. Ikibidi nguo zitaazimwa kwa washikaji town!

Ila ukiingia kwenye muziki ni kuwa mwangalifu ili blues ikipigwa usiwe single vinginevyo utaondoka ukimbini. Na mademu wasiotaka kucheza blues kibano ni halali yao. Kwanza kwa nini wamekuja disco kama hawataki kucheza. Ila blues yenyewe inavyochezwa du, ni hatari tupu. Hata hivyo disco ni mara moja kwa muhula so enjoying for 3 or more hrs was something you wouldn't want to miss hata kama una malaria!!
 
Mkuu Invisible unanifurahisha lakini ndio ukweli wenyewe. Disco likipigwa na mademu jamaa wanapagawa wiki moja kabla.

Duuh! Kweli mambo yanafanana! Kwetu pale mabrazameni walikuwa wananyoa nywele mtindo mtindo special for disco aka debe.

Halafu baada ya disco inabidi alazimike kuyoa tena kuondoa mtindo huo kwani darasani ni marufuku.
Mnakumbuka nguo za OPP ?? Siku ya disco OPP kibao!
 
kwa shule za bweni,madume watupu,siku ya disko ilikuwa ishu..matayarisho ni zaidi ya miezi miwili.....kuhusu viwalo ,kwenda library ilikuwa muhimu ie kuazima pafyumu na nguo...kachupa ka pafyumu huwa kanakuwa kamoja,mnapulizia kwa zamu...ukichelewa ukikuta imeisha, unavunja kale kamdomo ka chupa then unajaza maji ,unatikisa kidogo,nawe unapaka....ndo maana kuna kademu wakati wa bluzi kaliwahi kuniuliza mbona wote mnanukia harufu zinazofanana?

nikapata kigugumizi..nikabaki eeer ooh eerr...ndani ya disko ole wako usiopoe kademu hasa wakati wa bluzi...bwenini hautakaa...manake baada ya disko wenzio wataanza kuletewa barua zenye manukato ,wewe hola!!!

kuhusu stempu ...kulikuwa na kaujuzi ka kufuta ule muhuri nafikiri kwa kutumia sponji na sabubi flani....then una reuse......maisha yalikuwa raha sana jamani!!!
 
Kwa wale akina yakhe kama mimi bajeti ya sabuni ni mchii mmoja kwa mhula basi kufua shati ni mara moja kwa wiki na kuoga ni Jumapili (unatoka bafuni kama umejipaka unga).

Kutokuwa na pasi nako kulifanya ubunifu mkubwa wa kukunja nguo kiustadi na kuzilalia zikiwa chini ya godoro, aah no tandiko.

Mmmhh msinikumbushe mie yaliyotokea wakati huo!!
 
Nakumbuka siku ya kula wali J4 lakini viongozi wa chakula anajichotea wali wa kutosha anakulahadi Ijumaa

Umenikumbusha jamaa mmoja aliyekuwa anatafuta nafasi ya ku-serve siku ya wali na akiipata utakiona kivumbi chake maana siku mbili hadi tatu anakula wali tena bila hata kuchemsha.

Jamaa huyo aliendelea kuwa tabia yake maana nilipata habari kuwa kwenye harusi ya mdogo wake huko kijijini alijiwekea pilau kwa ajili ya safari kesho yake. kilichotokea ni kuharisha karibu njia nzima.

jamani tabia za shule zingine zafaa kuachwa uanpofika uraiani.
 
Back
Top Bottom