Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi, elimishi na hamasishi uzalendo za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hutolewa kwa mfumo wa maswali, makala ya leo ni kuhusu utoaji wa taarifa za Corona, COVID-19: Nani Mkweli Kati ya Serikali Yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Jee Tanzania Tunawaogopa Sana Wamarekani?!. Kwanini Wamarekani Waseme Uongo Mkubwa kama Huu halafu Waachwe tuu hivi hivi?!.
Nimesoma with disbelief hii taarifa ya leo ya ubalozi wa Marekani, kwanini ubalozi unatoa taarifa ya uongo kuhusu hali ya COVID-19 nchini kwetu na wanaachwa hivi hivi?!, Jee hawa Wamarekani tunawaogopa?.
Taarifa yenyewe inapatikana hapa kwa wale wa kimombo
Tanzania International Travel Information
Kwanini Wamarekani waseme uongo waachwe?!. Kama serikali yetu itawanyamazia hawa Wamarekani bila kuwaonya au kuwachukulia hatua yoyote kwa uongo wao, then waelewa wataelewa nani ni muongo kweli na nani ni mkweli, na pia huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Mmarekani tunamuogopa, hata utusingizie uongo gani sisi, tunanyamaza tuu!.
Tanzania na rais wetu Magufuli na serikali yetu tumekuwa tukisingiziwa uongo mwingi na sometimes hata kutukanwa na kudhalilishwa na media za nje, lakini tunanyamaza ama kwa kuwapuuza, ama kwasababu Tanzania kwa sasa hatuna watu wenye the capacity kujibu tuhuma kama za The Economist, lakini enzi za Kikwete, aliposingiziwa na balozi wa Marekani kuwa amehongwa suti, Ikulu yetu haikunyamaza, baada ya kupiga kelele humu, Marekani walikanusha.
Lakini sasa leo rais wetu anasema ukweli, kesho Waziri wetu wa Afya anasema kweli, halafu kesho yake, ubalozi uliopo hapa hapa Tanzania unaibuka na taarifa za uongo kuonyesha serikali yetu inaficha ukweli!, ukificha ukweli maana yake unachoripiti ni uongo!. Sasa huu uongo unaosemwa nchini, na ubalozi fulani, usipokanushwa, itaamaanisha ama tunawaogopa Wamarekani, ama tunachoelezwa na serikali yetu ni .. na wanayoyasema Wamarekani ndio ukweli wenyewe, ilaikitokea hawa Wamarekani ni waongo, swali linabaki "Hivi hawa Wamarekani wanatutakia nini?!. Kwanini watutungie uongo na kuueneza dunia nzima?. What is their motive behind and what do they wish to achieve?.
Paskali

Kama rais Magufuli juzi kasema Corona imepungua, jana Waziri Ummy kathibitisha kwa data, leo Marekani inaibuka na kesema hizo taarifa zinazotolewa na viongozi wetu ni taarifa za uongo, na kutusingizia serikali yetu inaficha data, nani mkweli na nani muongo?.Kwavile taarifa yenyewe ni ya kimombo, kwa manufaa ya wenzangu na mimi, ninawawekea kakipande kadogo tuu ka mayai, na kukatafasiria kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
(Given the presumed ongoing community transmission in Dar es Salaam and other locations in Tanzania, the risk of contracting COVID-19 remains high. The Embassy has recommended that U.S. government personnel and their families reduce movement outside of their home except for essential activities and limit the number of visitors entering their home.
Healthcare facilities in Tanzania can become quickly overwhelmed in a healthcare crisis. There have been instances during the COVID-19 outbreak when hospitals in Dar es Salaam reached full capacity due to the high volume COVID-19 cases. Limited hospital capacity throughout Tanzania could result in life-threatening delays for emergency medical care)
Kwa kuanzia ni jana tuu, wakati kuna mwandishi wa habari wa kike gazeti wa gazeti la raia Mwema, ameozea jela kwa kushikiliwa kwa siku 14, kwa kusambaza ujumbe fulani wa Corona kwenye group la ofisi, jana hiyo nimepokea taarifa ya kifo cha mwandishi wa habari mkongwe mwenzangu katika fani ya upigaji picha za TV, nimefanya nae kazi DTV, kisha TBC, mimi nikatimuliwa kazi na kuingia mitaani, mwenzangu akaula na kuwa mpiga picha wa viongozi wakuu!, jana amefariki dunia hospitali fulani kwa ugonjwa fulani, leo tumemuaga, anazikwa kwao kesho!. Hatuwezi kutaja chanzo cha kifo kwasababu sisi sio familia yake, lakini tunakijua na kinazungumzwa wazi tuu msibani!.
Kama mpaka sasa update ya Corona kwa Tanzania ilitolewa mara ya mwisho tarehe 29 April wakati huo idadi ya vifo ni 16, na mpaka leo hakuna update hivyo idadi ya waliokufa kwa Corona Tanzania bara ni huo 16 tuu, na huu ndio ukweli wenyewe, kwanini Wamarekani
wanatusingizia uongo na kuitangazia dunia kuwa tunaficha data na wanaachwa hivi hivi?.
Rais wetu katangazia taifa kwa jiji la Dar es Salaam katika mahospitali wagonjwa wamepona na hakuna maambukizi mapya, kesho yake Waziri wetu wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu akatangaza Mlonganzila kumebaki wagonjwa 3, Amana amebaki mmoja Kibaha hakuna mgonjwa, hakuna kifo chochote, hakuna ambukizo jipya lolote, halafu leo, Ubalozi wa Marekani unatoa press release kuutangazia dunia kuwa Tanzania tunaficha data, wakati hakuna ambukizo jipya lolote, Wamarekani hawa wanatangazia dunia kuwa mahospitali yamefurika wagonjwa!, kwanini Wamarekani waseme uongo huu, waachwe, who the hell are they?!, au tunawaogopa?.
Kama Serikali ya Tanzania inasema ukweli, hakuna wanaokufa kwa Corona, hakuna maambukizi mapya na wagonjwa mahospitalini wamepona na kuruhususiwa na hakuna tena karantini yoyote, halafu Marekani akaitangazia dunia kuwa Tanzania tunaficha ukweli, dunia itawaamini nani kati ya sisi na Wamarekani?.
Tena taarifa hiyo ya Marekani, haijuishia tuu kutusingizia uongo kuwa serikali yetu inaficha data, wakati serikali yetu inasema ukweli, bali pia wametatishia mashirika yote ya ndege ya kimataifa yaliyotangaza kuanza safari za kuja Tanzania kuleta watalii, Marekani imewatisha kwa kutumia mtindo wa innuendo kwa kuyataja majina hayo mashirika, kuonyeshea wasipo cancel safari hizo, then hatua ya pili ni kuwataka Marekani na washirika wao, kuyasusia mashirika hayo.
Hivyo naomba kuwaanda kabla msije kushangaa, baadhi ya mashirika waliokubali kurejesha route ya Tanzania baada ya tishio hili la Marekani, wakafanya risk analysis kati ya kuleta abiria wa Tanzanians kupoteza soko la Marekani, au waitose Tanzania na kulinda soko la Marekani!.