The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 7,382
- 8,437
Moja kwa moja kwenye mada.
Hatimaye Beberu USA ameirejesha tena Tanzania kwenye mpango wa kufaidi pesa za ruzuku(grants) kupitia programu ya "Millennium Challenge Corporation" -MCC ambapo Serikali ya Marekani hutoa pesa za ruzuku kama motisha kwa nchi ambayo inafuata Demokrasia, Uwazi, Haki za Binadamu na Uhuru wa Maoni.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani Nchini Sanjali na Tanzania,Nchi nyingine zilizorejeshwa ni The Philippines na Cabo Verde baada ya kutimiza vigezo vinavyotakiwa.
Hatua hii imekuja baada ya Tanzania kutolewa kwenye mpango huo Awamu ya 5 kwa kushutumiwa kukandamiza Haki za kiraia hivyo kuikosesha nchi mabilioni ya pesa za bure.
Ikumbukwe Tanzania ilikuwa inapokea Dola za Marekani Milioni 700 (Trilion 1.75) ambazo zilikuwa zinaelekezwa kwenye miradi ya kipaombele. Baadhi ya miradi ambayo ilijengwa Kupitia msaada huo ni miradi ya umeme Kigoma, Barabara za kutoka Songea-Masasi, Sumbawanga-Tunduma, Kigoma-Uvinza, Daraja la Kikwete Mto Malagarasi na baadhi ya miradi ya Afya.
View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1735938236332052571?t=Lvd1NCTWdI-HN5Ynd-hIeg&s=19
My Take
Hongera sana Rais Samia hatimaye juhudi zako za 4Rs na diplomasia ya Uchumi zimeleta matokeo.
Hakuna mtu anaweza kataa pesa za bure ambazo masharti yake ni Ustawi wa jamii yako.
View: https://www.instagram.com/p/C00by-aqGVO/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==
View: https://twitter.com/MCCgov/status/1735335152052572200?t=xtn0zND3v8EDARAZ2ITCFA&s=19