Imezoeleka kuwa utawala wa Rais Magufuli umetia umma woga. Kwamba anachokisema Rais Magufuli ndio fainal hakuna wa kupinga au kutenda kinyume.
Msimamo wa Rais Magufuli ni kwamba hakuna Corona maana tutatishwa sana. Kilichopo ni changamoto ya kupumua ambayo dawa yake ni kujifukizia, kufanya kazi kwa bidii "na ndio maana hatuvai barakoa". Alisema mbele ya dunia huko Chato.
Hata hivyo umma mpana umemgomea Rais Magufuli na badala yake unawasikia viongozi wa dini na Shirika la Afya Duniani, WHO. Magufuli amegomewa, hasikilizwi maana watu wameamua kuvaa barakoa, wananawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni, ulaji wa matunda ya asili kwa sana, vitunguu swaumu, limao, ukaaji kwa nafasi nk. Hakuna cha nyungu wala vyungu. Huu ni mgomo wenye kheri!
Endeleeni hivyo hivyo maana Corona ipo. Tupambane nayo kama Jakaya Kikwete alivyoamua kuvunja ukimya na kuvaa barakoa hadharani. Akili ya kupewa changanya na zako.
Maisha yako hayako mikononi mwa mtu yeyote ni wewe. Vaa barakoa kujiokoa na kuokoa wengine. Ugonjwa upo!