Serikali ya Rais Samia imeinua morali ya kazi kwa Watumishi wa Umma

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu watanzania,

Kwa hakika serikali ya Rais Samia imeinua kwa kias kikubwa Sana morali ya kazi kwa watumishi wa umma,hii ndio maana ya kuona uchumi wetu ukiendelea kukua na kufanya vizuri,hii ndio maana watanzania wakienda katika ofisi za umma wanapokelewa na kuhudumiwa vizuri Sana,hii ndio maana watanzania wakienda mahospitalini wanapokelewa, kusikilizwa na kupata huduma Bora na stahiki,hii ndio sababu watumishi wa umma Wana utulivu mkubwa Sana makazini na maofisini mwao,hii ndio maana husikii habari za migomo makazini.

Kwa Sasa nimeshuhudia licha ya kuwa Ni kipindi Cha rikizo lakini walimu kwa morali kubwa Sana na upendo na uzalendo mkubwa kwa wanafunzi wakihudhuria na kuwahi kazini kwenda kuwafundisha wanafunzi ambao ndio viongozi wetu wa kesho, madaktari wa kesho, wanajeshi, polisi usalama wa Taifa letu kwa kesho, wabunge na mawaziri wetu wa kesho, wanasheria na wahandisi wetu wa kesho.

Watumishi wa umma wamehamasika kutokana na namna serikali ya Rais Samia inavyowajali katika maslahi yao yote.,. serikali ya Rais Samia imefanya hivyo kwa kuwa inajuwa kuwa ili kila secta ya umma iende na kufanikiwa Ni lazima watumishi wa umma wafanye kazi kwa uzalendo,bidii,weledi na kujitoa na kujitolea kwa mioyo Yao yote.

Sasa watumishi wa umma wanaona mchango wao ,juhudi zao na jasho lao likitambuliwa na kuheshimiwa na serikali yao ,ndio maana wameamua kuchapa kazi kwa juhudi ,maarifa na bidii ya Hali ya juu Sana kuwahudumia watanzania wenzao wanaofika katika ofisi zao.

Hii ndio sababu hata watanzania wanaendelea kufurahishwa na uongozi wa serikali ya Rais Samia kwa kuwa wanapata huduma Bora na stahiki kutoka kwa watumishi wa umma,wanaona namna wanavyoheshimika wafikapo ofisi za umma.

Hii ndio sababu watanzania wapo bega kwa bega na serikali na hawapo tayari kusikiliza upotoshaji Wala kupandikizwa chuki mioyoni mwao ,Wana mwamini Rais Samia na serikali yake na wanatambua dhamira njema aliyo nayo Rais Samia kwa Taifa letu. Wanatambua uzalendo mkubwa alio nao Rais Samia katika kifua chake kwa Taifa letu, ndio maana hawataki kumsikiliza yeyote anayeleta maneno ya kibaguzi kwa misingi ya udini, ukabila na ukanda

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Madaraja yapo kwa mujibu wa sheria, annual increment ipo kwa mujibu wa sheria vilevile but ongezeko la mshahara kwa takwa la Rais ni ridhaa yake. Bado hajatumia ridhaa yake vizuri
 
Madaraja yapo kwa mujibu wa sheria, annual increment ipo kwa mujibu wa sheria vilevile but ongezeko la mshahara kwa takwa la Rais ni ridhaa yake. Bado hajatumia ridhaa yake vizuri
Palipo Baki naamini mh Rais ataendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma kwa kadli Hali ya uchumi itakavyokuwa inaruhusu.
 
Kuna wakati huwa najiuliza hivi wewe una akili timamu kweli? Una familia? Aise kama una mke au mpenzi basi ajue bwana yake ni zoba
 
Walimu mnasemaje?😂😂
Walimu wameridhishwa na utendaji na uchapa kazi uliotukuka wa serikali yoa,wanafurahia namna serikali inavyoendelea kuwaboreshea maslahi yao,kulipa malimbikizo ya madeni Yao na kuwapandisha madaraja pamoja na kuwalipa stahiki zao kulingana na madaraja husika bila kuchelewa .
 
Mama samia anafeli sana kama kiongozi
Rais Samia kafanikiwa na kufaulu Sana Kama kiongozi katika kuongoza Taifa letu na kuleta matumaini katika mioyo ya watanzania,ndio maana anaendelea kuungwa mkono na kuaminika kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom