CoronaVirus: Hizi ndizo sababu kwanini Italia ina vifo vingi vitokanavyo na virusi vya Corona

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Licha ya safu kadhaa za hatua za karibu za kupungua au kusitisha kuenea kwa virusi vya Corona zikiwemo kufungwa kwa nchi nzima na kufunga kwa biashara zote ambazo sio muhimu, Italia haikuweza kuzuia kuenea kwa maambukizi

1. WINGI WA WAZEE
Ingawa virusi vya #corona vinaweza kuambukizwa kwa watu wa rika lolote, Watu wazee sana ambao kinga yao ya mwili imepungua kutoakana na umri, wapo katika hatari ya kuwa mahututi wanapopata maambukizi

Nchini Italia kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya nchi hiyo, asilimia 85.6 ya waliofariki kutokana na #Covid_19 walikuwa na miaka zaidi ya 70. Kwa ujumla asilimia 23 ya raia wa Italia ni Wazee, ikiwa ni nchi ya pili kwa Wazee wengi baada ya Japan

2. KUWA NA MAGONJWA MENGINE:
Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya Nchini humo, asilimia 48 ya waliopoteza maisha kutokana na #Corona walikuwa na wastani wa magonjwa mengine matatu

Taasisi hiyo imesema, "Tuna idadi kubwa ya Wazee wenye magonjwa mengine mengi walioweza kuishi muda mrefu kutokana na kuhudumiwa kwa umakini mkubwa lakini watu hawa ni dhaifu kuliko wengine"

Wazee wa Italia, wakati wengi wao wanaishi peke yao, hawajatengwa, na maisha yao yana mwingiliano mkubwa zaidi na watoto wao na idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na nchi nyingine.

Wakati mlipuko wa magonjwa kama huu unatokea [kama vile milipuko ya coronavirus] ni muhimu mwingiliano huu kupungua, kwa hivyo kuwatenga watu wazee ilitakiwa liwe jambo la kwanza kufanyika.

3. KUTOKUWA NA UTAYARI WA KUTOSHA:
Nchi ya Italia imekumbwa na Janga hilo kwa ukubwa baada ya China na Wataalamu wanasema njia wanazotumia sasa kujikinga ni vema zikafuatwa na watu ikiwemo kuwekwa karantini.

Madaktari wa Italia wameonya kwamba kusita kuchukua hatua haraka na kwa uadilifu kunaweza kuwa na matokeo mabaya sana. Nchi zichukue hatua kali zaidi.

Mkuu wa Magonjwa yanayoambukiza katika Hospitali ya Sacco, Massimo Galli amesema "Kama ningekuwa kichwa cha Waziri yeyote wa Afya katika nchi yoyote, ningeogopa sana na ningesogea haraka sana kuchukua hatua kali za kuzuia maambukizi".

"Katika hali hizi, sote hatujajiandaa milele: haiwezekani kuwa tayari kikamilifu kushughulikia matukio kama haya".

MAPAMABO YANAENDELEA ITALIA
Huku kukiwa na maombi wimbi lingine la Virusi hivyo lisitokee, Mamlaka zimeendelea kuwatenga watu. Hoteli ya nyota 4 ya Michelangelo huko Milani imegeuzwa kuwa jengo la Karantini kwa wa 300. Jengo la Maonesho limegeuzwa kuwa ICU
 
Hukusikia kipindi kile corona ilivyo shika kasi china waislamu walivyo kuwa wanasema

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui muislamu gani ulimsikiliza wewe,lakin waislamu hawaongozwi na matamko ya watu binafsi kwenye mambo kama haya,bali wale waliopewa mamlaka ya uongozi.

Gwajima aliposema Corona haitofika Tanzania,mimi simufikilii hata kidogo kuwa wakristo wamesema Corona haotofika Tanzania,Then again we think different,Stay safe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa maudhui haba mkuu RJ.

Ngoja nije nielezee sababu za Italy kuwa na wazee wengi (aging population) japo kwa maelezo machache.
 
Uchambuzi makini, ndio maana kwetu sisi tahadhari tungeweka kwa kuwalinda wazee sana na wenye kinga dhaifu. Wengine tutamudu kwa kinga ya mwili.

Kiukweli kwa stdvya maisha yetu hatuwezi kuepuka kuambukizana. Mfano mdogo usanii kuosha mikono, mtu anafika getini ama mgahawa anaweka simu kwa pochi ama mfukoni kisha anatakasa mikono, hatua chache anapakata tena simu yake, virusi corona vinaishi kwa siku 3-4 juu ya plastic. Hatuelezwi mbinu kutakasa simu,mifuko na pochi zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIZI ZOOOTE NI VIJISABABU TU ''FUNIKA KOMBE MWANA HARAMU APITE'' HEBU ONGELEENI SABABU HALISI.
 
Sijui muislamu gani ulimsikiliza wewe,lakin waislamu hawaongozwi na matamko ya watu binafsi kwenye mambo kama haya,bali wale waliopewa mamlaka ya uongozi.

Gwajima aliposema Corona haitofika Tanzania,mimi simufikilii hata kidogo kuwa wakristo wamesema Corona haotofika Tanzania,Then again we think different,Stay safe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ee mkumbushe huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom