Italia itaanguka katika mtego wa Marekani wa kuleta utengano katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111437973118.jpg


Hivi karibuni, Waziri wa Ulinzi wa Italia Guido Crosetto alisema, nchi hiyo ilfanya uamuzi wa ghafla na usio na mantiki wa kujiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), miaka minne iliyopita, na kudai kuwa, katika kipindi chote hicho, hakuna kilichofanyika kuongeza biashara ya nje ya Italia.

Kauli hii inaaminika kuwa ni ujumbe wa nguvu Zaidi kutoka kwa serikali ya Italia kuhusu hatma ya baadaye ya nchi hiyo katika mfumo wa Pendekezo hilo.

Tofauti na madai ya Bw. Crosetti, mauzo ya nje ya bidhaa za Italia nchini China yaliongezeka kwa asilimia 58 ikilinganishwa na mwaka jana katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu. Ni kweli kwamba ushiriki wa Italia katika Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja, kama anavyodai Bw. Cresetto, umeongeza mauzo ya bidhaa za China nchini Italia. Lakini hii si habari mbaya kwa nchi hiyo, kwa kuwa bidhaa za gharama nafuu za China zimewawezesha raia wengi wa Italia kuwa na chaguo Zaidi katika manunuzi, na hivyo kusaidia kupunguza athari za kuongezeka kwa gharama za maisha kwa raia wa kawaida.

Hivi karibuni, wakati akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua, Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uchukuzi wa Baharini ya China Ocean nchini Italia, Marco Donati, alisema serikali ya Italia inapaswa kutofanya kosa la kuchukulia faida za kujiunga na BRI kwa mtindo wa upande mmoja, na kuongeza kuwa, nchi hiyo inapaswa kuwa makini zaidi na kutumia BRI ili kulifanya soko la Italia kuwa la ushindani zaidi.

Tangu kusainiwa kwa makubaliano ya awali ya BRI kati ya China na Italia mwaka 2019, pande zote mbili zimepata mafanikio kadhaa Dhahiri katika biashara, uchumi, na ushirikiano wa kibiashara. Chini ya BRI, bidhaa za Italia zinaweza kuingia kwenye soko kubwa la China kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi kuliko awali. Maboresho katika sekta ya ugavi ni muhimu kwa Italia kuweza kuwa na ushindani zaidi katika soko la kimataifa, na pia, BRI ina maana ya fursa nyingi zaidi kwa kampuni ndogo na za ukubwa wa kati za nchini Italia.

Lakini licha ya mafanikio hayo, serikali ya Italia, katika matukio tofauti, imeonyesha dalili ya nia ya kujitoa kwenye Pendekezo hilo. Ikumbukwe kwamba, Bw. Crosetti alitoa kauli hiyo siku chache tu baada ya Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, kukutana na rais wa Marekani, Joe Biden, katika ikuli ya Marekani. Ni wazi kwamba, hatua ya Italia kubadili msimamo wake kuhusu BRI, kwa kiasi kikubwa, inatokana na shinikizo la Marekani.

Tangu Italia ilipoamua kujiunga na BRI, imekuwa ikipata lawama nyingi kutoka Marekani, kwa mfano, gazeti la New York Times la nchini Marekani lilikosoa Italia kuwa inaruhusu uwezekano kuongezeka kwa ushawishi wa China kiuchumi, kijeshi na kisiasa, katikati ya Ulaya, na kusema ikiwa ni nchi pekee ya Kundi la Nchi 7 (G7) kujiunga na BRI, Italia imepewa jina la msaliti wa nchi za Magharibi. Kutokana na shinikizo la Marekani, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi alisitisha makubaliano ya BRI mwaka 2021.

Sasa, kutokana na kuwa serikali mpya iko madarakani, Marekani imeongeza juhudi zake za kuishawishi Italia, ambayo ni mwenza wake, kujitoa kwenye Pendekezo hilo. Baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanaendelea kukumbatia nadharia ya “Vita Baridi”, na kulichukulia Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kuwa tishio la kiusalama na jaribio la China kuzigawanya nchi za Magharibi. Chini ya mvutano wa siasa za kijiografia dhidi ya China, Marekani imechukua kila fursa kuwavutia wenza wake katika kile kinachoitwa “klabu ya China”, na kuwaondoa katika Pendekezo hilo ni hatua ya kwanza.

Mabadiliko katika serikali ya Italia, huku wanasiasa wa mrengo wa kulia wa “Brothers of Italy” wakiwa na nafasi zaidi, Marekani haiwezi kukosa kutumia fursa hii kuleta mgawanyiko kati ya Italia na China.

Ikumbukwe kuwa, tangu kuanzishwa kwake, BRI imekuwa jukwaa la kujenga jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na maslahi pamoja na mahitaji ya pande zote kuzingatiwa. Hii ina maana kuwa, Pendekezo hilo sio klabu ya kupinga nchi za Magharibi ama ya siasa za kijiografia, au wenzi wa kijeshi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu wa nchi za Magharibi, bali liko wazi wa jamii ya kimataifa, zikiwemo nchi za Magharibi.

Sasa, wakati China ikijitahidi kutoa suluhisho la kivitendo la kujenga jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja kwa binadamu wote, Marekani yenyewe imekuwa ikilazimisha Italia na nchi nyingine wenza wake wa Magharibi kufanya uamuzi. Hatua hii inaonyesha kuwa, Marekani ina lengo la kuchochea mapigano, sasa kama Italia itaangukia kwenye mtego huu, ni jambo ambalo litajulikana siku zijazo.
 
Pole sana mkuu,USA itaendelea kuwatesa moyoni magaidi.
Imtese nani
Ila kama inaendelea kutesa iendelee tu kulikua na roman empire leo inasomwa tu kwenye vitabu
Nisuala la muda tu nguvu za milele ni za muumba pekeee
 
Back
Top Bottom