Duu kwa hiyo factor ya kwamba unaua watu wangapi una neglect?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwa hiyo mtu akigundulika tu kwenye office mnafunga ,so mnafunga office kwa mda gani manake ugonjwa hauleweki na haijulikani utaisha
lini,sasa utafunga mpaka lini?Hata chanjo haijulikani itapatikana lini,chanjo ambayo ipo kwenye majaribio UK ambayo kidogo naona itawahi kutumika,wanadai mpaka mwakani mwezi wa 10 WANAWEZA (just probability) wakaitumia kutibu Corona,sasa TUFUNGE MPAKA oct 2021.
Nchi zote zilizofungua nchi zimelazimisha mf Italy,Spain hata UK Boris wakati anafungua nchi alipata upinzani mkubwa bungeni,Spain mpaka Italy kote walipata upinzani na pamoja watu wanakufa lkn wameamua KUISHI NAO HUU UGONJWA na sasa wanaamua kufanya shughuli zao.
Sasa ikiwa nchi za dunia ya kwanza zinafungua wakati kwao kuna vifo vingi sana,je wewe huku dunia ya tatu ambaye uchumi wako mbovu ambaye una vifo vichache sana UNAFANYAJE ? au UTAFUNGA?
Uganda wale wana walazimisha kuwafungia ndani watu wao,mpaka sasa askari polisi kwa mujibu wa BBC washawaua watu 12,mtu aliye kufa kwa Corona Uganda 1,hapo manake watu unawafungia wana njaa,sasa hapo bado hutajapiga hesabu waliokufa kwa njaa?.
Kenya mpaka sasa walimu wa shule binafsi hawalipwi mishahara yao manake familia zao hazili,kuna wengine kwa mujibu wa Citzen tv hawana pakulala wanefukuzwa na baba wenye nyumba,Kaunti ya Machakos mpaka sasa kwa kipindi cha miezi minne watoto waliopata mimba kuanzia age 12-20 wamefikia 4000 na hapo kiyo kaunti moja na shule zinafunguliwa January.Hebu angalii hili jedwari (Kenya) wanafunzi walivyo pewa mimba kipindi hiki cha lockdown kwenye kaunti zote hapo hawaja fika jan2021.
View attachment 1517630
View attachment 1517630
Kenya nao kwa mujibu wa BBC polisi wanewaua raia kwa kuwalazimisha wakae ndani wakati hawana chakula wana njaa, Kenya mwaka huu wamepata mapigo mawili Mafuriko na Nzige na kwa mujibu wa shirika la chakula la UN inakadiriwa idadi watakao kumbwa na JANGA la njaa itaongezeka kutoka 1.3m mpaka 3m. Manake mnapoomba idadi ya vifo vya Corona ombeni vya WANAOKUFA KWA NJAA,manake kwa kuziangalia Kenya Uganda unaweza ukakuta wanakufa kwa njaa tu ni wengi zaidi kuliko hata Corona.
Sifa ya kiongozi kwanza unaangalia watu wako uwezo wao na uwezo wa nchi yako,je nikifunga nina uwezo wa kupatia mahitaji yao raia wangu kama chakula na hela za kuwa boost?,pili vipi impact ya ugonjwa huu ni mbaya au tunaweza ishi nayo(rate yake ya vifo) huku tukichukua tahadhari ?
Usifanye eti kwa sababu US ,UK,France wamefanya ,usitumie baadhi ya solution ya dunia ya kwanza na ukaiapply kwa dunia ya tatu utafeli na utawaua raia wako kama afanyavyo Kenya na Uganda.Najua utasema RWANDA,Rwanda kwa nchi za UG,KE na TZ ni kama mkoa mmoja ambao kuumanage rahisi.
Huu ugonjwa upo hamna anayekataa cha msingi tuishi kwa tahadhari huku tukiendelea kufanyashughuli zetu za kila siku.
NARUDIA TENA HUSIFANYE KITU ETI SABABU US,UK,FRANCE,GERMANY KAFANYA,UTAWAUA RAIA WAKO,SIO KILA SOLUTION ILIYOTUMIKA ULAYA UNAWEZA UKAIAPPLY AFRICA UTAFELI.
HAPA AFRICA RAIA WENYE UHAKIKA WA KUPATA MILO KAMILI MITATU SIZANI KAMA WANAVUKA 25% ,sasa unafunga huku raia wako wanakufa kwa njaa kwa ugonjwa ambao impact yake ni ndogo mno.