Corona: Shule Afrika Kusini zafungwa tena

Corona: Shule Afrika Kusini zafungwa tena

Mungu anajibu maombi kama hujamuomba anatulia kusubiri umuombe,ndo maana anasema ombeni mtapewa so Shari umwombe

Ulichoandika hapo ni kusema kuwa: "Mungu ni Athumani."

Umeeleweka mkuu.
 
Hii sio sawa,ni uongo,
serikali hii hii ndio ilisema maeneo kama masoko,kanisani,msikitini ni maeneo hatarishi,leo unasema "wamehodhi taarifa....."
yaani ungesema wazi,serikali ifanye A,B,C ... ningekuelewa ila naona sivyo,si neno jema kuwa hivi;
kuwa mkweli tu,serikali hii imejitahidi kuwaondoa hofu wananchi wake juu ya korona,kama vifo vingekua kiasi hiki unachokiweka hapa jukwaani,basi huku mtaani tusingekua tunaishi hivi tuishivyo.
siitetei serikali,ila tusimamie ukweli,uongo haulipi,haipaswi kushusha mioyo ya watu kwenye matatizo, bali kuwapa uimara.
mkuu unasema uongo.

Tulikubaliana hoja kwa hoja na bila jazba au sivyo?

Sasa haya ya wewe huyo huyo kuwa hakimu au jaji katikati ya hoja yanatoka wapi?

Serikali imehodhi taarifa za ugonjwa huu yakiwamo maeneo ambayo kwa sasa yanaweza kuwa ni hatari zaidi kwa ugonjwa huu kuliko mengine ikiwamo mikoa, wilaya, kata na hata vijiji.

Kama hali ya Dodoma ingejulikana wazi kwetu sote labda wazee wetu lulu kabisa hawa, tusingewaachia kwenda kwenye mikusanyiko ya vyama vyama hii isiyokuwa na thamani wala tija kulinganisha na maisha yao?

Wewe huoni hivyo, bali ghafla unaanza kuwa jaji na kuanza kuitana majina? Mara muongo, siyo muwazi nk. Mamlaka hayo unajimilikisha tu katikati ya hoja?

Nguvu ya hoja bro, hoja za nguvu kwenye jamii iliyostaarabika hazina nafasi.

Nini cha kufanya: Mara mbili nimekujibu.

Maswali yangu mawili comment #40 hujajibu hata moja. Kutokuwa na majibu nayo inaeleweka mkuu. Kama huna majibu hulazimishwi kujibu. Kistaarabu lakini.

Msidhani kuwa wenye macho hawaoni hadi muwape ruhusa hiyo nyie.

Tanzania ya leo mbona siyo ile. Alisema mzee baba. Heko kwake kwa kulitambua hilo.
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Afrika Kusini wamezifunga tena shule zote kwa mwezi mmoja wanapoendelea kupambana na ugonjwa huu.

Mapambano ni pamoja na tathmini ya wazi ya mirejesho pasipo na kujidanganya.

Korea kusini, China nk, nako wanapita katika hali kama hizo hizo.

Marekani ya Trump sasa kuvalia mabarakoa si hiari tena.

Antananarivo Madagascar hali si hali na mabarakoa sasa ni shuruti.

Tusimsubirie wa kumfunga paka kengele, lives of the people matter!

Hatumkomoi yeyote kwa kutozingatia masharti yaliyowazi ya kujikinga na kuwahami wengine na ugonjwa huu.

======


South Africa to Close Schools Again as Covid Infections Surge​

Loni Prinsloo and Paul Vecchiatto

South Africa plans to shutter schools for a second time as the number of Covid-19 cases surges, according to two people familiar with the matter.

South African President Cyril Ramaphosa may announce the decision in a televised addressed at 8 p.m. in Pretoria on Thursday, the people said, asking not to be identified because the information isn’t public yet.

The closing of schools will be scheduled to coincide with an already planned break in early August, to reduce the impact of the shutdown on the academic year, the people said. Proposals put to the president include shuttering campuses for three weeks or longer, they said.

The number of confirmed coronavirus infections in South Africa doubled over the past 17 days to surpass 400,000. More than 13,000 cases were reported for a second consecutive day on Thursday, bringing the cumulative total to 408,052 -- the world’s fifth-highest. The government has forecast that the country is expected to reach its peak-infection rate in the coming weeks.

All schools were closed in March when the government introduced one of the world’s strictest lockdowns to curb the spread of the virus. Since they re-opened on June 1, teachers’ labor unions and some members of the public have urged the government to close them again.

While South Africa’s privately funded schools are well-resourced, there has been a concern around space in classrooms for physical distancing, and even water and sanitation in some of the nation’s public schools.

Source: Bloomberg


Corona sio aids wala ebola. Inatafuna wasauzi kama haina akili.
 
jifunze kuwa mtu mkweli na muwazi;
naona wewe ni mbishi tu,ila ukweli kila mtu atauona,endelea kukinga familia uwezavyo,ila sio kuiambia nchi haiendi sawa na wengine;
hoja zako halisi kuhusu korona katika nchi hii sizioni,unatamani mabaya yatupate uone unabii wako umetimia,lakini hakika tutaishi hivi hivi,watakaokufa ni wale wale ambao wangekufa bila uwepo wa mafua haya;
naomba utuambie,wewe kama wewe umefanya nini kama njia thabiti ya kujikinga?,

Nimeandika mabandiko mengi sana na si humu jamvini tu. Uko wapi ushahidi wa kuonyesha popote ambapo sijakuwa muwazi au mkweli?

Wewe ni nani kujipa mamlaka ya kuhukumu?

Uko wapi ushahidi wako kuwa ninaitakia nchi hii mabaya? Ndoto za mchana tu?

Hivi huwa mnafikiria rationally tu kama binadamu wengine kweli?

JF, tuko huru huna mamlaka hayo ya kuhukumu wengine:

"It's here, where we dare to talk freely."

Kongole kwenu JF.

Kwamba watakaokufa kwa Corona ni wale wale ambao wangekufa tu hata kama Corona isingekuwapo? God forbid!

Wanawaona wahanga wale ambao kwa hakika hatua zingechukuliwa wangali kuwa hai leo.

Eee mola wetu utusamehe waja wako sisi tulio wakosaji.

Kwa kukosa taarifa sahihi za ugonjwa huu hapa nchini, binafsi nipo confused. Sijui wapi nipaepuke wala nimshauri nani aepuke wapi.

Kuninyima taarifa za mikoa, wilaya, kata, na vijiji kuhusiana na prevalence ya ugonjwa, nimenyimwa taarifa za lazima katika kuniwezesha kujikinga na hata kusaidia kuwakinga wengine.

Actually kwa hilo najisikia kutelekezwa na watu niliodhani tumewapa dhamana ya kutulinda.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Mkuu kwani wewe una corona mwanao je, mama ako au ndugu zako ? ukisikia kifo cha gafla hicho kilipangwa na Mungu mm najuan hamna corona kama ipo mashuleni watoto wangedondoka na kufa vyuoni , tuna ndugu zetru huko hamna hata aliye na mpango wa barakoa ila maisha yanaenda tu
Wajinga wa mitandaoni hawa huwa wana upumbavu mwingi sana chief!
 
Wajinga wa mitandaoni hawa huwa wana upumbavu mwingi sana chief!

Mwerevu ndiyo wewe?

Kwa hakika nyani kuona *undule ni karama.

Hongera mkuu kwa kuliona la kwako.
 
Tunabishana kwenye Corona kwa sababu hii hapa:

"Corona imefanywa siasa. Eti kuwa ni security issue huku watu wanakufa."

Eboo, security issue ya Tanzania peke, wakati ugonjwa upo hata kwa Putin, Trump, nk, China, Ulaya ya kusini, Africa, kote?!

Corona ni ugonjwa wa mwili kama malaria, typhoid, kaswende nk.

Tatizo liko hapo tu.

Tungepanyoosha hapo vita hivi tungewachia madaktari wa binadamu front line.

Umenisoma hapo mkuu?
Ujing ujinga mtupu.

Unang'ang'ania au unataka kuufungulia NGO upige hela.
 
Watanzania tutumie fursa ya uchaguzi kuuondoa utawala wa magufuri madarakani. Kinachoendelea nchini mwetu ni mchezo wa bahati nasibu.
ni hatari sana kuwa na uongozi unaofuata misingi ya namna hiyo kuongoza.

na cha hatari zaidi, inapaswa tujiulize ni kwa nini uongozi umechukua risk kubwa namna hii? lazima kuna sababu ambayo sio nzuri.
Mtizamo wako ila reality ugonjwa huu impact yake haujafikia hata robo ya Malaria.

Malaria ipo lakini watu bado wanaishi nayo pamoja na impact yake kubwa lakini watu wanaendelea kupiga kazi kama kawaida.So lazima maisha ya endelee.

Yaani Corona nayo ishakua ajenda ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2020,huko ni kufilisika kwa sera na mawazo.
 
Mkuu hivi niko msibani, kumradhi lakini.

Kuwepo Corona au kutokuwapo hakuwezi kulazimishwa. Wala si suala la imani.

Hilo ni suala la vipimo, suala la kitaaluma. Yaani sayansi.

Hayo unayobwabwaja ni maneno matupu ambayo hayavunji mfupa.

Maneno matupu hayo ndiyo 'siasa' zenyewe zikiwamo zile za security issue, si ya Uganda, Kenya, UK, China, Russia, nk, bali eti ya Tanzania; ninayokwambia inaingizwa kwenye huu ugonjwa kama porojo tu.

Wewe ulidhani siasa nayo sema ni u-TLP, u-NCCR, u-CCM, uCDM au u ACT?

Hiii bagosha!
Hivi unavyohusisha vifo vya watu na corona hali ya kuwa huna ushahidi tuseme hiyo ni sayansi au unatumia imani? kama ni siasa ni wewe ndio unaleta siasa unailazimisha hiyo corona, mfano sasa unahusisha kifo cha mzee wa watu na corona hali ya kuwa hata hujui Mzee wa watu alikuwa anasumbuliwa na maradhi gani.

Basi tufanye kwamba haya Mzee wetu kafa na corona na hiyo ni kutokana na ule mkutano wa dodoma,hivyo tutarajie kuona wengine wakifuatia. Maana mule wazee walikuwepo na wengine afya zao sio nzuri.
 
Watanzania tutumie fursa ya uchaguzi kuuondoa utawala wa magufuri madarakani. Kinachoendelea nchini mwetu ni mchezo wa bahati nasibu.
ni hatari sana kuwa na uongozi unaofuata misingi ya namna hiyo kuongoza.

na cha hatari zaidi, inapaswa tujiulize ni kwa nini uongozi umechukua risk kubwa namna hii? lazima kuna sababu ambayo sio nzuri.
Dah but anyway kila MTU anauhuru wa kuongea.
 
Back
Top Bottom