Hatari ya Corona inafahamika. Jinsi inavyouwa inajulikana:
Vichomi na changamoto za kupumua huambatana nayo katika hali ya ghafla sana. Waathirika wake wakuu wazee na wenye magonjwa mengine.
Mgonjwa mlikuwa naye anaendelea vizuri siyo wa kufa, mara ooh!
Haya ni kama yale ya rais mstaafu wa Burundi. Kumbuka ya mtwara, ya wabunge wetu nk (rip). Kama binadamu yote haya yanapaswa kuwa mafunzo.
Uzi huu hapa haujitengi na vifo vya namna hiyo kwa ndugu zetu hawa waliotangulia (rip):
Corona: Orodha ya wahanga, sampuli
Uzi huo una kada ya wanasheria nguli tu. Hawa ni jamaa zetu, ndugu zetu, colleagues wetu nk. Wapumzike kwa amani.
List za wanafunzi, walimu, vigogo nk, zote zipo na zinaendelea kuhuishwa ((jambo la kutia moyo) hata kama wewe na miye na yule tutakuwa wahanga wa huu ugonjwa ambao kwa hakika ulikuwa ni ugonjwa mwingine tu kama malaria.
Malaria inataka kuondosha maji yaliyotuama kuyaondosha mazalia ya mbu kwa usalama wetu.
Corona inataka social distancing, mabarakoa, sabuni na maji tiririka.
Kwanini ramli ndugu zangu?
Tofauti za huko China na kwingine unakosema iko kwenye vifo vya vigogo, na hizi kada zingine ambazo naturally tunapaswa kutambua kuwa zilikuwa kwenye lower risk.
Haisaidii kuukimbia ukweli. Huu ugonjwa upo na watu wanakufa.
Tuchukue hatua kuwahami wazee wetu na mikusanyiko isiyokuwa na thamani ikulinganishwa na maisha yao.
Eeh mola wetu hebu ukatujalie ujasiri sisi waja wako wa kutambua kuhitajika kwa juhudi zetu dhidi ya magonjwa ya binadamu yanayoendelea kuongezeka.