- Thread starter
- #41
Nasikitika sana kuona mtanzania mmoja anafanya juhudi kila kukicha kuonyesha ugonjwa ni mkali na watu hawana amani,ila hizo dalili za kushindwa,haifai kunakili njia wanazotumia wenzetu,sisi ni sisi na wenyewe ni wenyewe;
tuamini akili zetu na miili yetu sio yao,siwezi kufunga nchi niombe msaada katika hali hii,hatuna hali mbaya ya ugonjwa kama unavyotaka kuaminisha watu;
huu ugonjwa unapata nguvu kwa media,kwani nikipimia watu kwa wingi ndio hakuna athari?,
kwani nikiwa na idadi ya visa ndio hakuna maaambukizi mapya wala vifo?,
je,hao wenye kujua idadi ya visa wamefanikiwa nini kutuzidi katika suala zima la ugonjwa huu?,
ebola hapo Congo inaua sana,je,imewahi kupata jina na nguvu za media kama hii nCOVID-19?,
kaka,tafakari vizuri, sio kila njia inayotumiwa na nchi fulani na sisi inapasa tuifate;
Corona ipo,ila hofu ilizidi,na wengi walienda na hofu;
Wakuu:
Bujibuji, blessedhope, residentura, jogi, lenie, kipangaspecial, kuhan noah, aun, owomkyalo, kinyungu, nk, nk, nk, nk.
mkuje mara moja mnaitwa huku.
Kwamba kuna mtanzania mmoja tu kila kukicha ndiye anayepiga kelele kuitisha kuwahami wazee wetu na watu wengine dhidi ya ugonjwa huu?
Kuwa hii mikusanyiko ambayo hainayo thamani ya maisha ya wazee wetu hawa ambao leo tunawalilia na hatuwezi kuwarejesha tena, kuwa hivi vilio ni vya mtanzania mmoja tu?
Mkuu utakuwa kweli umetuchoka au ni mgeni hapa jamvini au hapa nchini.