copy & paste ya Clouds TV

copy & paste ya Clouds TV

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
ubunifu ni kitu pekee kinachoweza kuitofautisha brand moja hadi nyingine/kampuni nyingine ambazo/yo inatoa huduma zinazolingana/fanana.

Nirudi kwenye topic,sina shaka na uwezo wa clouds media Group katika ubunifu na mambo mengine linapokuja suala la burudani hapa Tanzania, ila kwa hili niseme Clouds TV wamekosa ubunifu na walichoishia kufanya ni kukopy na kupaste vipindi vyao kutoka TV stations nyingine mfano EATV.Vifuatavyo ni baadhi ya vipindi ambavyo Clouds TV wamekopy na kupaste kutoka EATV....

1.Siz kitaa- City sound (kilichokuwa kikiendeshwa na Seki)

2.Take One-Bongo movie (kilichokuwa kinaendeshwa na Joyce Kiria).

3.Ongea na Janeth-The Mboni show (kinachoendeshwa na Mboni)

4.Wazee wa Madebe-Friday Night Live(kinachoendeshwa na Sam Misago).

5.kipindi cha Paradise cha Irene uwoya nayo ni programu ambayo inendeshwa na TV stesheni nyingi za nje katika mtindo wa documentary,lakini kipindi hiko kinafanana kabisa na kipindi ambacho hufanywa huko Nigeria na moja ya TV stesheni,so sio kitu kipya pia.

Mdau unaweza kuongeza vipindi unavyovijua ambavyo jamaa wamecopy ila si kwa nia mbaya.
 
Yeah mkuu Dero umeniwahi,student corner wamefanya plagiarism EATV..wamekosa ubunifu wa kuwa unique katika vipindi vingi vya television yao
 
Hata kile cha student corner wameiga skonga...ujue issue sio kuiga bali wanapwaya mno!.. Taarifa ya habari ndio usiseme inaboooa!

lakini tunategemea mtu aje na kitu kipya kitakchowavutia watazamaji,kama unakuja na vitu ambavyo wenzako wanavifanya tena kwa ufanisi mkubwa hautafanikiwa.
 
Vichaaa tu wale,,,,, hata redio
XXL n kipindi maarufu sana State kule nawao wamecopy kama kilivo
Power Breakfast kama kawiz mtu keshasema hapo juu
..Kilie kipind cha kimbea nacho hakuna kitu pale
Kifupi n kwamba wanaAnza kabidhi kijiti sun tu watakuwa kama ilivokuwa RFA,Redio One,na RTD
 
Namnukuu hayati Bob Marley aliposema "Sisimami upande wa Mungu wala upande wa Shetani,bali nasimama upande wa Haki".
Clouds media wameharakia sana kuanzisha TV station huku wakiwa hawana watangazaji wa uhakika,wenye vipaji mbali na elimu ya uandishi wahabari,mvuto (namna ya kumvutia mtazamaji atizame kipindi chako) na vingine vingi tofauti na EATV.Wakati anaondoka Salama ktk kipindi cha planet bongo,mtangazaji ambaye aliteka hisia za watu na kukamata mashabiki wengi wlompenda na waliomchukia,waliamua kufanya mchakato wa kumpata mrithi wake na katika huo mchakato wakapata vipaji vingine ambavyo vilikuja na mawazo mapya mfano Allan Lucky!
Cloudz inabidi wajifunze kupitia kwa watu na si kujiona wanajua kila kitu!
 
Clouds ndio habari ya mujini bana acheni majungu

hakuna anayefanya majungu ila tuasema uhalisia,wao wanajisifu sana kwa creativity iweje sasa kila kitu wanacopy?au ndio mambo ya kutumia fursa?mimi binafsi napenda waje na vitu vipya vitakavyotuvutia watazamaji na kututushawishi tuache kuangalia TV stesheni nyingine.
 
Namnukuu hayati Bob Marley aliposema "Sisimami upande wa Mungu wala upande wa Shetani,bali nasimama upande wa Haki".
Clouds media wameharakia sana kuanzisha TV station huku wakiwa hawana watangazaji wa uhakika,wenye vipaji mbali na elimu ya uandishi wahabari,mvuto (namna ya kumvutia mtazamaji atizame kipindi chako) na vingine vingi tofauti na EATV.Wakati anaondoka Salama ktk kipindi cha planet bongo,mtangazaji ambaye aliteka hisia za watu na kukamata mashabiki wengi wlompenda na waliomchukia,waliamua kufanya mchakato wa kumpata mrithi wake na katika huo mchakato wakapata vipaji vingine ambavyo vilikuja na mawazo mapya mfano Allan Lucky!
Cloudz inabidi wajifunze kupitia kwa watu na si kujiona wanajua kila kitu!

ni kweli kabisa na kuna vijana hku mitaani wana idea nzuri sana za vitu vipya ila ndio nafac hawapati wao wanachofanya ni kupeana nafac kwa kujuana bila kujua wanaharibu image yao katika jamii.
 
Everything in Clouds media is copy and paste. Poleni kwa mnaoliwa huku mkijiona, mie wala simo huko. Nikienda kwa washikaji nikisikia tu station ya Clouds, nawaoamba wabadilishe haraka kwani sitaki masikio yangu yaharibike kwa sauti zao na lafudhi zao feki za kujifanya hawajuwi kiswahili wakati wakiwa na wazazi wao wanaongea kiswahili tena fasaha ila redioni hawajuwi.
 
Clouds tv kuifikia EATV ni safari ndefu.
Ukiangalia EATV ni kama unaangalia channel za mbele!!

EATV level za mbali sana,wamejipanga na wanajua wanachokifanya,I salute them
 
Back
Top Bottom