Edwin Mtei
R I P
- Dec 13, 2008
- 181
- 342
Invisible,
Nini sababu ya ku remove docs? Mimi nadhani njia bora ni kuziacha kila mtu azione ili majadiliano na uelimishwaji kwa wengine wasio na access na mtandao iwe rahisi. Kama hakuna sababu za kiusalama za ku remove please ziweke tu mkuu.
Hans Lottering
"Kwa barua hii Serikali inaiagiza TANESCO iingie mkataba na Kampuni ya Richmond ili mitambo iletwe na kuanza kuzalisha umeme haraka iwezekanavyo. TANESCO inawajibika kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Richmond na Kamati ya Majadiliano ya Serikali (GNT)."
Ijumaa ya tarehe 23 Juni 2006, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa TANESCO, Bwana Johannes .G. Lottering, aliitwa Wizara ya Nishati
na Madini na kuagizwa kusaini Mkataba huo kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC. Pamoja na kusita kwake,
hatimaye alisaini mkataba huo.
.............................
Aidha, Kamati Teule ilipata tetesi na baadaye ushahidi kuwa Richmond Development Company LLC ilikuwa na wapambe ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waliokuwa wanaipa taarifa (insider dealing). Mfano mdogo tu ni wa Ndugu Mohamed Saleh, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usambazaji wa TANESCO na rafiki wa karibu wa wamiliki wa Richmond Development Company LLC. Alishiriki kwenye Kamati ya Wataalam na Kamati ya Serikali ya Majadiliano. Alipostaafu tu TANESCO, akawa mmoja wa wahandisi waandamizi wa DOWANS HOLDINGS S.A iliyochukua majukumu ya Richmond Development Company LLC.
.............Mheshimiwa Spika, tarehe 19 Juni, 2006, Bodi ya Zabuni ya TANESCO ilikutana na kupitisha uamuzi rasmi wa kufuta zabuni waliyokuwa wanashughulikia awali na kutangaza kuwa "TANESCO isihusishwe na mkataba wowote utakaotokana na nyaraka za zabuni waliyoifuta".
Lakini siku hiyo hiyo ya tarehe 19 Juni 2006, Waziri wa Nishati na Madini alimwandikia Waziri Mkuu dokezo kuwa majadiliano ya awali na Richmond Development Company LLC yamekamilika hivyo Serikali iiteue kampuni hiyo kwa lengo la kuingia mkataba na TANESCO wa kuzalisha umeme wa dharura kwa miaka miwili. Sehemu ya barua hiyo inasomeka:
"Kamati ya Serikali ya Majadiliano (GNT) inayojumuisha wataalam kutoka Wizara Fedha, Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Benki Kuu na TANESCO ilifanya majadiliano na Richmond Development Company LLC ya Houston, Marekani kutoka tarehe 8 hadi 16 Juni 2006, kwa kuzingatia maelekezo yako."
Mheshimiwa Spika, tarehe 21 Juni 2006, Katibu wa Waziri Mkuu Ndugu B. Olekuyan aliiandikia Wizara ya Nishati na Madini kuitaarifu kuwa Mhe. Waziri Mkuu amekubali mapendekezo na ushauri wa Waziri wa Nishati na Madini kama ulivyokuwa umeletwa.
Siku hiyo hiyo tarehe 21 Juni 2006, Waziri wa Nishati na Madini akamwandikia dokezo Katibu Mkuu wake aiagize TANESCO iingie mkataba mara moja na Richmond Development Company LLC baada ya Waziri Mkuu kuidhinisha mapendekezo ya Wizara. Muda mfupi baadaye, kwa kutekeleza agizo la Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akamwandikia barua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO Balozi Fulgence Kazaura kumwagiza ahakikishe kuwa TANESCO inasaini mkataba na Richmond Development Company LLC.
Mheshimiwa Spika, Ijumaa ya tarehe 23 Juni 2006, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa TANESCO, Bwana Johannes .G. Lottering, aliitwa Wizara ya Nishati na Madini na kuagizwa kusaini Mkataba huo kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC. Pamoja na kusita kwake, hatimaye alisaini mkataba huo.
.............................
tarehe 4 Disemba 2006, TANESCO ikapokea barua kutoka kwa Richmond Development Company LLC ikielezea makusudio ya Richmond kuhamisha majukumu yake yote ndani ya Mkataba huo kwenda kwa Dowans Holdings, S.A.
Siku hiyo hiyo TANESCO ikaijibu Richmond kwamba haikuwa tayari kuridhia pendekezo hilo kwa sababu kuu tatu:
(i) Kifungu 15.12 cha Mkataba kinataka kuwepo kwa makubaliano ya pamoja ya kimaandishi (written mutual agreement) kutoka kwa wahusika wote wa Mkataba (Parties) kabla ya kufikiwa uamuzi wa kuhamisha Mkataba.
(ii) Richmond Development Company LLC haijatoa sababu zozote za msingi kwa pendekezo hilo la kuhamisha Mkataba.
(iii) TANESCO haifahamu historia, uzoefu wala uwezo wa kifedha wa hao wanaopendekezwa kuhamishiwa Mkataba.
Aidha, TANESCO ilikumbushia barua zake za awali ilizoiandikia Richmond Development Company LLC kuhusu ukiukwaji wa masharti ya Mkataba, lakini Richmond haikuzijibu. Hivyo, TANESCO ikataka ipate kwanza majibu ya masuala yote iliyoyaainisha kabla ya kufikiria kuridhia pendekezo la kuhamisha Mkataba huo.
Mheshimiwa Spika, kama kawaida ya Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO ikashinikizwa kukubaliana na ombi la Richmond hata kabla kampuni hiyo ya Kimarekani haijajibu hoja za msingi za TANESCO. Tarehe 21 Disemba 2006 TANESCO ikaiandikia barua Richmond Development Company LLC kukubali pendekezo la kuhamisha majukumu yake kwa Dowans Holdings, S.A..
Tuendelee Kujikumbusha
Hapo ndipo Tanesco waliingia MKENGE...........
Kamati ya Mwakyembe ilisema hivi:
Zitto sidhani kama ni Lottering aliyesaini mkataba wa Disemba 23, 2006. Alisaini wa Richmond na Tanesco lakini si wa Tanesco na Dowans. Niko tayari kusahihishwa.
Pia amesema jana PM, Alafu tunabeza ujenzi wa bwawa la Nyerere kisa chuki kwa JPM. Its obvious chuki kwa JPM ziko very personal achilia mbali mapungufu yake.Mkuu hujatoka nje ya mada; suala la gesi nalo ni suala la kuangalia, linaongeza mzigo mzito kwa TANESCO ilhali inatoka hapahapa kwetu. Inazua shaka kuwa hata tukichimba mafuta bado hali itakuwa mbaya kwa nishati hiyo Tanzania, watakaonufaika ni wachache kwa michezo yao ileile