CONFIDENTIAL: TANESCO, RICHMOND, DOWANS and BoT

CONFIDENTIAL: TANESCO, RICHMOND, DOWANS and BoT

kwa mazingira haya waziri wa wizara ya nishati na madini wakati huo anatakiwa auze ng'ombe na mbuzi wake alipe deni..ni upuuzi na ushenzi mkubwa kuingilia ishu zisizomuhusu..kulikuwa na maslahi yake hapa sio bure
 
Wasomaji,ukisoma nyaraka hizo angalieni maudhui na tarehe. Kudokeza tu, Richmond walihamisha mkataba kwa Dowans miezi mingi kabla ya kuijulisha Tanesco!!! Ni wazi sasa Dowans haiujulikani ni dudu gani na liliingiaje. Ni wazi kuwa kupanda kwa bei ya umeme chanzo chake kinajulikana na maumivu yanawagusa wote.

Suala sasa ni nani alipe, huku majukwaani tunaambiwa serikali haitaki kulipa. Nyuma ya pazia watumishi wa serikali wapo bize kutupiana mpira nani alipe. Sijui kauli ya rais inabeba heshima gani kwa haya tunayoyaona na sijui tumwamini au tuwe na shaka kila mara akitoa kauli.Serikali inatupa mpira kwa Tanesco kwasababu haitaki hesabu zake zionyeshe Richmond/Dowans kwani kufanya hivyo kutawakaanga vigogo na hasira za wananchi zitaibuka. Wanatupumbaza.!!

Suala hapa si nani alipe, kwasababu in the end ni pesa kutoka hazina. Kinachotakiwa ni kutolipa.
Kinachoshangaza kwanini watu watupiane mpira na serikali haiongelei wale waliotufikisha hapa wamechukuliwa hatua gani.
RA na EL wanatuchezea sana! wamefanikiwa kutuondoa kwenye Richmond/Dowans, sasa tunapigana vikumbo nani alipe na si nani achukuliwe hatua. Wanasiasa dhaifu nao wanatubabaisha, hatulipi kumbe wanalipa kwa siri. So so sad!
 
Dont worry mimi mlinzi wenu niliejiajiri mwenyewe nawa hakikishia mafisadi kiyama chao nilishakiona with my two eyes. Bado tu manifestation into physical lakini ground work tayari imesha kamilika (mission accomplished) watashika kila mahali watakuta moto na mwishowe wata surrender.

Mkuu kwa kauli hiyo, naamini ni ya kizalendo!Nimeipenda. Sijui utaendelea kuwa peke yako kwa muda gani?
 
Ama kweli... Pesa za kununulia mitambo unazo. unasitisha mkataba ..Zimetowekea wapi???
Kudos ....Bodi ya Tanesco na Utawala..nadhani paka kafungwa kengele!!! Atazinyamazishaje zisitoe keleel!!
 
Mapendekezo ya Ludovick Utouh ni uji mwepesi...

Anabainisha matatizo lakini hapendekezi hatua za kisheria kuchukuliwa wote wale ambao wamehusika katika ufisadi huu. Kama anaweza kujua makosa, yawaje ashindwe kuwataja wahusika jina baada ya jina na kubainisha ni makosa gani ya kuhujumu uchumi wameyafanya na wanapaswa kuchuliwa hatua gani?

Tatizo hapo ni kuwa ofisi ya CAG haiko huru na ndiyo maana Utouh anatoa majibu mepesi ya kumsaidia JK kufunika mashimo makubwa kama haya. This is why we need a new constitutional order to deal with all issues that are weakening our institutions of governance...

Haya mazingira ambayo Utouh kayabaini yatasaidia kwenye kesi ya kukataa kuwalipa DOWANS ya kuwa ile TUZO was fraudulently extracted.........and therefore can not be honoured in light of our own laws.....

Sidhani kama Utouh anaweza kulaumiwa hapo. Kazi yake ni ku-audit na sio kuchukulia watu hatua za kisheri. Tena aliarrange mpaka meeting kujaribu kuaddress the issue, hakuna aliyefika
 
Baada ya kusoma hizo nyaraka nashindwa kulewa how come TANESCO lost that case at ICC. Itabidi tena nikasome ile kesi in the light of the new information kwenye hizi nyaraka.

Pia nafikiri JF na vyombo vingine vya habari vinakabiliwa na changamoto kubwa sana on how to inform the public on what is going on. Otherwise, information muhimu kama hizi zitaishia humu humu jamvini. Although labelled as confidential, sioni how confidential this information is, b'se watu wamekuwa wakispeculate hivyo vijiweni. This is just confirmation of what was already on the public domain.

After all, this is a public issue. Whether TANESCO or serikali watalipa, sisi wananchi ndio tunalipa. We should therefore be entitled to hold accountable those who created this mess. But as I said before, how can we if only about 100,000 of the public or even less get hold of this credible information? Imagine what the wananchi would have done if they get hold of this information?
 
Wasomaji,ukisoma nyaraka hizo angalieni maudhui na tarehe. Kudokeza tu, Richmond walihamisha mkataba kwa Dowans miezi mingi kabla ya kuijulisha Tanesco!!! Ni wazi sasa Dowans haiujulikani ni dudu gani na liliingiaje. Ni wazi kuwa kupanda kwa bei ya umeme chanzo chake kinajulikana na maumivu yanawagusa wote.

Suala sasa ni nani alipe, huku majukwaani tunaambiwa serikali haitaki kulipa. Nyuma ya pazia watumishi wa serikali wapo bize kutupiana mpira nani alipe. Sijui kauli ya rais inabeba heshima gani kwa haya tunayoyaona na sijui tumwamini au tuwe na shaka kila mara akitoa kauli.Serikali inatupa mpira kwa Tanesco kwasababu haitaki hesabu zake zionyeshe Richmond/Dowans kwani kufanya hivyo kutawakaanga vigogo na hasira za wananchi zitaibuka. Wanatupumbaza.!!

Suala hapa si nani alipe, kwasababu in the end ni pesa kutoka hazina. Kinachotakiwa ni kutolipa.
Kinachoshangaza kwanini watu watupiane mpira na serikali haiongelei wale waliotufikisha hapa wamechukuliwa hatua gani.
RA na EL wanatuchezea sana! wamefanikiwa kutuondoa kwenye Richmond/Dowans, sasa tunapigana vikumbo nani alipe na si nani achukuliwe hatua. Wanasiasa dhaifu nao wanatubabaisha, hatulipi kumbe wanalipa kwa siri. So so sad!

Mpira umepasiwa kwa washambliaji Mwanakijiji kawaelekeza washambuliaji kutokufanya makosa, mshindwe wenyewe kufunga goli la ushindi winga katoa cross nzuri sana! Mkiotea basi yeye si wakulaumiwa atleast kafanya kwa uwezo wake. Tukicheza vizuri hapo hata kama tutashindwa unganisha basi tunaweza lazimisha penalt maana timu pinzani wamesha panic ndiyo maana wanarushiana mpira nani alipe.
 
Kwakweli tupo kwenye janga kubwa sana nathani umefika wakati wa kuwaeleza wananchi aya mambo yanayotokea with document apo wataelewa kwamba kunatakiwa mabadiliko. Halafu inabidi tupate support kutoka kwy vyombo vya habari ambavyo vinaweza kujitoa muanga kuweka wazi aya mambo.

Hii ni hatari sana kwa taifa letu tukikaa kimya tunaweza kuangamia kwa uzembe wa watu wachache wasiojali jamii yetu ya watu zaidi ya 28Milion.
 
Hapa ni viinimacho tu,hakuna uwajibikaji! Kama wizara/watendaji waliingilia michakato ya tanesco na kusababisha madudu,afu tena ndo tumewarudisha tena madarakani na kupewa kamati etc!!!?Walau mambo yamekuwa wazi zaidi.Tunahitaji kuchukua hatua sasa za nguvu!
 
Wananchi, tunaumiza vichwa bila sababu kwani ingawa ukweli umetukodolea macho, tunazunguka mbuyu tukijidai hatuuoni. Haya madudu yote tunayoyashuhudia hakuna namna yangeweza kufanikiwa ila kwa baraka (amri ?) za mtu moja tu naye ni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete !

Yabidi sasa malalamiko na mashambulizi yetu yelekezwe kunakohusika nako ni kwa Kanali Jakaya Mrisho Kikwete kama mhusika mkuu. The bull must be grabbed by the horns na anayetaka kumuua nyoka sharti amponde kichwa na si mkiani, the buck stops with the President.
 
mkuu hapo kwenye bold...

CAG hakusema hicho unachosema wewe bali katika hiyo barua yake ameanza kwa background behind the story....barua hii ya CAG kumbuka inakwenda kwa PS wa MOF mh. Ramadhani Khijja ambaye katika barua yake kwa CAG ndiyo anadai kuwa TANESCO ibebe hiyo contingent liability na iwe katika books za TANESCO.....

Msimamo wa CAG uko katika paragraph ya tatu kutoka mwisho ambayo inaanza hivi...

In view of.....I recommend....

mkuu...CAG Utouh ni mtu makini sana...hawezi kuingizwa chaka na watu wajinga kama viongozi wa serikali ya CCM

Mkuu Al Zagawi nakushauri usome tena barua ya CAG ya tarehe 7 January, 2011 kwenda kwa Permanent Secretary and Paymaster General quote "On the other hand, I am aware that the Government has agreed to pay the debt through TANESCO. However, ....." end of quote. Msimamo au maamuzi ya serikali hayamzuii CAG kuwa na recommendation, ndio maana kama ulivyotaka kumnukuu hapo juu anasema I recommend, this is just a recommendation. A piece of advice kwako ni kwamba next time kabla ya kucritisize make sure umejipanga vizuri. Mimi si Makamba wala Tambwe mpaka nikurupuke kiasi hicho.

Kuna thread moja humu nilimlinganisha CAG na mzee Yusuph mtaalamu wa taarabu though si kwa ubaya kwani ndivyo hali ilivyo. CAG ana reports nzuri sana na kwa kweli kwa sehemu yake anafanya kazi nzuri sana. Lakini uzuri wa kazi yake unaharibiwa na wanasiasa kwani reports zake hazifanyiwi kazi, si bungeni au kwingine kokote ni kama nyimbo za taarabu tu hakuna cha ziada.

Nimemfahamu CAG kwa miaka mingi sasa toka akiwa NBAA, alipoteuliwa kuwa CAG na kukubali nilisikitika sana kwani I knew for sure kwamba tumempoteza one of the gurus kwenye fani ya audit nikijuwa fika kwamba ataishia kufanya sanaa tu kwani serikali yote ni ya kisanii from top to bottom. CAG huyu angetusadia sana kama angefanya kazi na Nyerere au Sokoine sio hawa wasanii wa sasa.

May God help us!
 
Kumbe hata kupanda umeme sio uamuzi wa Tanesco bali ni serikali iliamua ili angalau TANESCO iweze kulipa Dowans halafu wao wachache wakagawane pembeni, lol...ni kamzunguko kidogo lakini tumekaona............TUKUTANE 2015
MUNGU wangu ni mbali mnoooo! tutakuwa tumeumia sana aiseee sasa ni 2011 duuuu!
 
Hivi mnavyosema serikali ndio ilipe mnamaanisha nini?.....ninavyofahamu mimi serikali inatoa hela zake kutoka katika kodi zetu.....kwa hiyo ukisema serikali ilipe, inachomaanisha ni kwamba wananchi walipe.

Hii ya nani alipe ni kupoteza dira tu.....sisi msimamo wetu uwe HAKUNA KULIPA......sio tunabidsha nani alipe.
 
Kinanchonishangaza hapa ni kwa nini Rex attorney waliwashauri Tanesco kuvunja mkataba halafu wakashindwa kuwatetea tena ICC? Kulikuwa na misingi gani Serikali kupitia wizara ya nishati na madini kushinikiza Tenesco kusaini mkataba huo? Serikali ilituambia teni halitalipwa kumbe ilikuwa ni janja ya nyani kula mahindi mabichi.
 
Hivi mnavyosema serikali ndio ilipe mnamaanisha nini?.....ninavyofahamu mimi serikali inatoa hela zake kutoka katika kodi zetu.....kwa hiyo ukisema serikali ilipe, inachomaanisha ni kwamba wananchi walipe.

Hii ya nani alipe ni kupoteza dira tu.....sisi msimamo wetu uwe HAKUNA KULIPA......sio tunabidsha nani alipe.

Mkuu kwanza ninakushukuru kwamba umeonyesha kilichojificha ndani ya kauli hizi za TANESCO au SERIKALI kulipa. Mimi binafsi sikumwelewa sawasawa mwenyekiti wa POAC aliposema serikali ndiyo ibebe mzigo wa kuilipa DOWANS. Maana yake ni kwamba, Mh Zitto na kamati yake walikuwa wanahalalisha malipo kwa DOWANS yafanyike. Kimsingi walikuwa wanasema watanzania wailipe DOWANS.

Kuna vitu vya kuviangalia tunapotazama utendaji wa Bunge na serikali. Ukichukua taifa kama kampuni ambayo inamilikiwa na wana hisa utaona kwamba:
(i) Taifa la Tanzania linakaliwa na Watanzania wenyewe ambao kimsingi ndiyo kama wanahisa wa Rasirimali zilizopo Tanzania.
(ii) Serikali ni Utawala- Management katika taifa letu. Hapa ni sawa na kuwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni pamoja na wasaidizi wake, ambao ni wakuu wa Idara mbalimbali katika kampuni. Rais wa tanzania ni kama Mkurugenzi mtendaji wa kampuni na mawaziri wake ni kama wakuu wa idara wa kampuni.
(iii) Bunge ni kama Bodi ya Wakurugenzi iliyopewa dhamana ya kuhakikisha (a) Serikali yaani management inatimiza wajibu wake wa kuhakikisha rasirimali (Amana) za nchi zinatumika ipasavyo na kuongeza tija. (b) Bunge linakuwa ni kama vile NOn- Executive Directors wa kampuni. Sasa basi, Bunge haliwezi lote kuwalinafanya kila kitu, ndipo zikawepo kamati mbalimbali kama za akina Zitto na wengine kwa lengo la kurahisisha wajibu wa Bunge katika kuwatumikia wanahisa wa nchi ya Tanzania.

Sasa basi, Mh Zitto na wenzake wanaposimama kwa niaba ya Bunge kusema Serikali ndiyo iwalipe Dowans, inamaanisha kwamba Utawala utumie amana za taifa kuwalipa DOWANS jambo ambalo TUNALIPINGA NA CHADEMA kikiandamana kupinga hilo. Hapo ndipo ninajiuliza maswali kwamba hivi Mh Zitto na wenzake hawakupata kuona kwamba wanajichanganya na kwamba hawaelewi vizuri majukumu yao???

Zitto na wenzake watoe hoja zinazoeleweka badala ya kuanza kujikanganya!! Tunahitaji utendaji wa Bunge wenye tija siyo kuzungumza zungumza vitu ili mradi kupata media coverage!!
 
Wakuu, sisi wengine hatujabahatika kuziona hizo docs, please mods mnaweza kuziweka tena kwa faida yetu members!
 
Tunavyoongea sana ndo tunawa-awake hawa jamaa na ndo wanaanza kutuibia kwa njia mpya za kisasa, njia nzuri ilikua ni ku2mia bunge kumtoa ikulu JK lkn bunge lenyewe ndo lile nadhani mliliona ni mkusanyiko wa vilaza waliokusanywa na wananchi waenda kujifunza kuishangilia taifa stars kwa kuzomea.

Jamani hawa sio viongozi kama mnavyowaita, hili ni genge la wauni lililofanikiwa kuteka dola, na tusijidanganye eti kula zetu zinaweza kuwatoa ikulu, madikteta na magenge kama haya utolewa kwa nguvu ikulu (historia).
 
Back
Top Bottom