Compare between Dar Lux na ndege za panga boi

Compare between Dar Lux na ndege za panga boi

Kwenye ndege unakaa saa moja tu angani! Anasa zote za nini?
Basi waweke anasa hizo kwenye mabehewa ya treni reli ya kati maana hii hutumia siku mbilikutoka Dar hadi Mwanza, Kigoma na Mpanda.
 
Wabongo mmezoea kubeza kila kitu.. kumiliki luxury bus sio sawa na kumiliki luxury plane.. Hizo ndege wanatumia hadi 1st world countries.. luxury plane utaeza kulipa nauli yake..? Mmeletewa ndege zinazotumia mafuta kidogo angalau na walala hoi tusafishe tongo tongo bado mnaongea..
 
Basi waweke anasa hizo kwenye mabehewa ya treni reli ya kati maana hii hutumia siku mbilikutoka Dar hadi Mwanza, Kigoma na Mpanda.
Yale mabehewa mampya yana 'anasa' za kutosha... Ukisema uwekewe AC na anasa zingine je mteja yuko tayari kulipia additional costs? Shida ya Wabongo tunapenda kulipia the minimum cost possible...
 
Q400.jpg

Pateni knowledge kidogo..
 
Kwa hali hii acha Mkuu wa kaya aombe malaika ashuke kufungia mitandao tu
 
Yani kuongoza wa tz ndugu yangu ni mtihani mkubwa kuliko kuswaga ng'ombe.
Walau ng'ombe wanajua kuwa wanataka majani mazuri na maji lakini watz hawajui wanachotaka.
Wao kazi kumsifia aliyepita na kuponda kila anachofanya aliyepo.
Enzi za mwinyi walimsifia nyerere wakamponda mwinyi, enzi za mkapa walimsifia mwinyi wakamponda mkapa, enzi za jk walimsifia mkapa wakamponda jk, now enzi za jpm wanamsifia jk wanamponda jpm, hope akimaliza muda wake watamsifia pia.
Kwan ww unamsifia nani bro...
 
Ndege za mapangaboi zimeletwa ili kuwahudumia wananchi wanyonge na masikini wa kitaa, wacheni ziwahudumie walalahoi na wadanganyika.
Kuna mpango na mchakato kwa kila mkoa kupatiwa ndege 2 za mapangaboi. Siri-kali hii ina fedha za kutosha, kaeni mkao wa kutumbuliwa tu. Hapana kazi tu.
Kwani shida ni kufika ama "mbwembwe za seat ulipokaa"??? Anyway wahudumu wa ndege zetu hawana "sura za mvuto/atractive face" kama wa ndege za ETHIOPIA OR RWANDAN AIR OR EMIRATES.
 
we kama unataka kupanda luxury nenda kakodi private jet si unataka starehe kadodi private jet kweli.Kila kitu mna criticise sasa mfanyiwe nn hzo pesa ya kuajiri watu hakuna then unataka luxury kweli we huoni nchi ilipo the unataka luxury mbona zipo nyingi tu kakodi msheni kweli.

Ndo ujue sisi waga hatutaki ujingaaa.
 
Yale mabehewa mampya yana 'anasa' za kutosha... Ukisema uwekewe AC na anasa zingine je mteja yuko tayari kulipia additional costs? Shida ya Wabongo tunapenda kulipia the minimum cost possible...
Comment yangu ilijiegemeza kwenye dhana kwamba hayo mabasi ya Dar Lux yamekuja kwa ajili ya matumizi ya matajiri ilhali ndege za hapa kazi tu zimekuja kwa ajili ya walalahoi. Nilikuwa najaribu kulinganisha uwezo wa walalahoi wa Tanzania kulipa nauli kwenye ndege hizo (za walalahoi). Ngoja tusubiri nauli zitangazwe. Ila kwa kuwa tulishapewa mlinganisho kuwa nauli Dar-Mwanza ni laki nane kwa ndege zilizopo sasa, na Rais akaahidi kuweka nauli ya chini ya hapo, basi walalahoi wajiandae kusafiri kwa nauli ya punguzo kati ya laki 6 hadi 7...(assuming ni kweli kwamba nauli ya sasa ni lakini nane)

Pamoja na kuongelea mabehewa mapya yaliyokuja, lazima ujue kuwa hadi sasa asilimia kubwa ya wasafiri wanatumia yale mabehewa chakavu ambayo hata uteretibu wake wa kusafirisha abiria ni mbovu kwa sababu ya mbanano. Sitaki hizo AC ulizosema, ila nataka "improvement" ya hali iliyopo sasa kwenye usafiri wa treni daraja la tatu, ifikie kiwango cha kusafirisha binadamu...basi! Maana sasa hivi ni kama binadamu wanalazimisha kusafiri kwa kutumia usafiri usioandaliwa kwa ajili yao.
 
Back
Top Bottom