Wakuu wanayotamani watu wa comoro no wengi wanatutamani lakini basi wanashindwa...kila mtu anataka muungano na tanzania,hata hawa wapwa zetu hapo unguja wanajisemea tu...lakini wote wanaopiga kelele wanazipigia wakiwa star light au oysterbay...ningewaelewa sana kama wangesusa na kuamua kupiga kelele wakiwa chakwani!
..watanzania wenzangu nyerere aliliandaa taifa letu kuwa super power ,alijuwa utajiri wa rasilimali tunao..akaulinda na akaamua kwanza ajenge utajiri wa roho....watanzania ni matajiri wa roho...tunafurahi pamoja katika umasikini wetu [watoto wa temeke wanasema kugawana umasikini]...kwani ukiwa uswahilini wakipika wanaombana chumvi na chakula kikiiva wanabadilishana mboga....jirani analeta maharage ,wewe unampa kisonzo cha kisamvu,yule analeta papa ,wewe unapeleka sangara.....hiyo ndio falsafa ya kugawana umaskini.....maskini anakula mboga saba meza moja wakati yeye alipika mboga moja tu!!!...upendo uloje watanzania!!
Ndio mwalimu alitulea hivyo ndio maana tulichanga hadi nguo zetu za ndani na zaidi damu kuchangia ukombozi kusini........!!!matajiri walio karibu yetu ambao leo karibu hali zetu zinalingana pamoja na kuwa walikuwa mbele yetu saana ....wao hawakuchangia lakini leo wote tupo!!!
Tanzania lazima iwe super power kwani baada ya mwalimu kumaliza ground work ..tunamuomba mungu tumpate joshua ....kwani mwalimu amekufa kabla hatujafika nchi ya ahadi,...Joshua hatujampata .....bado!!!...akipatikana tukijenga uwezo mkubwa wa kiuchumi ......utajiri wa mali na fedha ...ukichnganya nautajiri wa roho....sioni nchi ya kuzuia influence yetu ...hasa kwenye mataifa ya jirani ambako makaburi ya askari wetu ,damu na michango yetu ipo....!!..kikwete asikate tamaa anao uwezo wa kuwa joshua wetu akitaka na akiamua kuwa serious!!!!..
damu za ndugu zetu na michango yetu mikubwa ipo.........Uganda,zimbabwe,congo,namibia,angola,afrika ya kusini,msumbiji,re union,comoro,...etc.!!!
Tuwaandae watoto wetu kufika pale tunapotaka!!!..tutaweza..tu kama tutatokomeza ufisadi..na tamaa za wachache wanaotaka kula matunda kabla hayajaiva........mwalimu angeamua kupopoa maembe....nani angejuwa????