Comoro yatamani Muungano na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Comoro yatamani Muungano na Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MzalendoHalisi, Mar 24, 2009.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  JF,

  Raisi wa Comoro anatamani siku moja Kuwa na Muungano na Mainland kama ule wa Zanzibar! Pamoja na matatizo madogo2 Muungano na ndugu zetu wa visiwani kwa sasa je kuna haja ya Tanzania kufikiria jambo hili?

  Faida Comoro watakayoitapa ni kuwa Politically Stable na hii threat ya mapinduzi na visiwa vingine kujitenga mara kwa mara itaisha! Faida kwa Tz zaidi ni kisiasa kwani hawa ni ndugu zetu na kama kuna shida itabidi tu tukawasaidie!

  Tayari Exim Bank wamefungua tawi Moroni na Kiswahili kimeanza kufundishwa Chuo Kikuu cha Comoro! Pia kuna biashara kubwa tu kati yetu kwa sasa!

  Komoro sii mwanachama wa SADC wala EAC kwa sasa tofauti na visiwa vingine Madagaska, Mauritius na Ushelisheli ambapo ni wanachama wa SADC!

  My Take:

  Inaonekana hawa jamaa tayari wametuzimia sana Tanzania haswa huyu raisi wao!

  Je wakuu mnaonaje?  Source: HabariLeo | Kikwete awaonya wanasiasa Comoro
   
  Last edited by a moderator: Mar 26, 2009
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Alisema yeye na nani? Isije ikawa anatoa maoni yake binafsi halafu baadaye watu wanaungana unazuka mzozo, mzozo wetu na Zanzibar hatujamaliza wanataka kutuletea mwingine?

  Watu wa Comoro wanasemaje? Watu wa Tanzania wanasemaje?
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Welcome muungano wa Comoro ...kule kuna akina dada wazuri sana itasaidia kuongeza gene pool
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280

  Masanilo, toto NYEUPE. Hulipi mang'ombe yoyote. Usiku wala huhitaji kibatarai. Poa sana, Ngosha tutalowea huko :)
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sasa Muungano wa Comoro wakitaka wapige kura ya maoni na tuwaambie hadi asilimia 90 ya wapiga kura wakubali! Zanzibar sasa watajisikia vibaya tukiungana na Comoro.
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Duh huyo Rais wa Comoro hajajisemea tu..., Maana inabidi Bunge lao ndio lipitishe... Imekaaje hiyo wadau???
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  La kushangaza ni kwamba kuna mambo mengi sana yanayotuunganisha kuliko yale yanayotutenganisha na Zanzibar,kwa upande mwingine yale yanayotuunganisha na Zanzibar ni mengi zaidi ya yale yanaotuunganisha na Comoro,hapa ni pale tunapopima yanayotuunganisha VS yale yanayotutenganisha kama vile lugha,dini nk.
  Base on the nadharia hapo juu,nitashangazwa kama muungano wetu na Comoro utakuwa smooth zaidi ya ule wa Zanzibar.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwungano na Comoro utasaidia kupunguza malalamiko ya Wazanzibari. Kapu litakuwa limepanuka.
   
 9. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu liangalie wazo hili kwa Uwigo Mkubwa zaidi...Jambo hili la Muungano na Comoro ni gumu sana kwa sasa,na wala sidhani kama litakuwa na baraka za Watanzania....kama alivyodai Mdau hapo juu,uamuzi ufanywe kwa kura ya maoni ya watanzania."Tusije tukabeba kapu kubwa lenye matundu mengi"
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa Wangazija wanaifahamu CCM kisawasawa? Mimi nadhani kabla ya viongozi wao kufanya hivyo waend Visiwani (Zbr na Pemba) wakawaulize wananchi wa kawaida kama wamefaidika nini na Muungano.

  Visiwa hivyo vimenasa katika historia -- hali ngumu sana ya maisha, mabasi ya mninga, wanaume wazima wanajifunga misuri ya khanga na mambo mengine ya ovyo ovyo tu. Ni viongozi wao tu ndiyo angalau wanaishi ktk pepo.
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  Wakuu wanayotamani watu wa comoro no wengi wanatutamani lakini basi wanashindwa...kila mtu anataka muungano na tanzania,hata hawa wapwa zetu hapo unguja wanajisemea tu...lakini wote wanaopiga kelele wanazipigia wakiwa star light au oysterbay...ningewaelewa sana kama wangesusa na kuamua kupiga kelele wakiwa chakwani!

  ..watanzania wenzangu nyerere aliliandaa taifa letu kuwa super power ,alijuwa utajiri wa rasilimali tunao..akaulinda na akaamua kwanza ajenge utajiri wa roho....watanzania ni matajiri wa roho...tunafurahi pamoja katika umasikini wetu [watoto wa temeke wanasema kugawana umasikini]...kwani ukiwa uswahilini wakipika wanaombana chumvi na chakula kikiiva wanabadilishana mboga....jirani analeta maharage ,wewe unampa kisonzo cha kisamvu,yule analeta papa ,wewe unapeleka sangara.....hiyo ndio falsafa ya kugawana umaskini.....maskini anakula mboga saba meza moja wakati yeye alipika mboga moja tu!!!...upendo uloje watanzania!!

  Ndio mwalimu alitulea hivyo ndio maana tulichanga hadi nguo zetu za ndani na zaidi damu kuchangia ukombozi kusini........!!!matajiri walio karibu yetu ambao leo karibu hali zetu zinalingana pamoja na kuwa walikuwa mbele yetu saana ....wao hawakuchangia lakini leo wote tupo!!!

  Tanzania lazima iwe super power kwani baada ya mwalimu kumaliza ground work ..tunamuomba mungu tumpate joshua ....kwani mwalimu amekufa kabla hatujafika nchi ya ahadi,...Joshua hatujampata .....bado!!!...akipatikana tukijenga uwezo mkubwa wa kiuchumi ......utajiri wa mali na fedha ...ukichnganya nautajiri wa roho....sioni nchi ya kuzuia influence yetu ...hasa kwenye mataifa ya jirani ambako makaburi ya askari wetu ,damu na michango yetu ipo....!!..kikwete asikate tamaa anao uwezo wa kuwa joshua wetu akitaka na akiamua kuwa serious!!!!..

  damu za ndugu zetu na michango yetu mikubwa ipo.........Uganda,zimbabwe,congo,namibia,angola,afrika ya kusini,msumbiji,re union,comoro,...etc.!!!

  Tuwaandae watoto wetu kufika pale tunapotaka!!!..tutaweza..tu kama tutatokomeza ufisadi..na tamaa za wachache wanaotaka kula matunda kabla hayajaiva........mwalimu angeamua kupopoa maembe....nani angejuwa????
   
 12. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  May be iwe two step process!

  1st Step- Zanzibar waungane kwanza na Komoro au Komoro iungane kwanza na Zanzibar jumla kutakuwa na Visiwa vitano: Unguja, Pemba, Anjouan, Ngazija (Grand Comoro) na Moheli ambavyo vitakuwa ni Umoja wa Zanzibar na Comoro..something like that!

  2nd Step- Jumuiko la Visiwa hivi (about 2 million population) waungane na Mainland na kuwepo na kura maoni na mchakato wa jinsi Muungano litakavyokuwa! Then tunaweza kuwa na serikali tatu: Visiwani, Mainland na URT makao makuu Dodoma may be. Au mji Mkuu uamuliwe uwe wapi?

  Then sote kwa pamoja tunajiunga na Shirikisho la EA, SADC or AU!

  Taabu nayoiona na iwapo Komoro na Zanzibar watapenda kuungana kwanza na kuwa na raisi na serikali moja!

  Hii ina maana hata jina la Tanzania itabidi litabadilika!

  Zanzibar hapa sijui kama watapenda..na hii itapunguza mvutano wa Seif na SMZ!

  Je imekaaje?
   
  Last edited: Mar 24, 2009
 13. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I am Pan –Africanist, but a realist at the same time. The idea of Comoro Islands to part of the United republic of Tanzania doesn't shake my ground, weather in hypothetical or actual terms. In both ways I found it quite appealing, specifically I am touched with social conditions of Comoro, which has no significant departure from Tanzania reality. However, I shall be concerned with intentions of the union, if they are political reasons – making history, power questions- or Pan-African Motives, or ILLUSIONS – some people just sit somewhere, and said, "You know it will be cool to have a union?" "Yeah, men why not!"

  Well, if we think about Comoro, we should take our historical reasons from Zanzibar, making sure people of all parties are interested to be part of the United Republic of Tanzania. I am assuming that will Still be the name – of course I am interested on the autonomy of my nation still! How problematic is that! I wonder, weather Comoro will want their island name to be included in the Republic--- hapo kutakuwa na kucheza dede!

  My worry, Tanzania main land, will play the politics of "conquest", without doing though analysis and define its commitment or its responsibility to the Island, rather it will be glad to expand its territory. So, I find it important for people of Comoro and Tanzania to decide on the union question. My suggestion the union should start with social matters, for example, I love water, so I should go and swim there na kula madafu! That's will be fantastic! Then later, hard business should be in question – defining clear interests of the republic to include Comoro! Zanzibar should have a separate voice as well! Like wise Comoro should tell us what will be the benefit for us to be together.

  Kazi itakuja kwenye political power!
   
  Last edited: Mar 24, 2009
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280

  ..kaka sema taratibu wake zetu wakisikia watapinga hili wazo la kuharakisha muungano na comoro..mimi nilikuwa pale mwaka jana ...ni watoto wabichiiii...Usifanye utani bwana ..wamanga si wamanga ,wahindi si wahindi ,wazungu si wazungu ,waswahili si waswahili...acha bana!!!!

  kama namuona JK sasa hiii...Guess akiambiwa achaguwe zawadi ..atachaguwa nini!! >
  kiddin
   
 15. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Taratibu kaka!

  Mapenzi yamejifunga sana katika mazingira rafiki yangu! mbona zanzibari ipo karibu tu, lakini bado wanaoana wao kwa wao kwa kiasi kikubwa tu! Hata hawa wengine tutatoa macho tu! Maana mimi nilipata kuhudhuria ndoa yao moja! ni siku saba! halafu hizo dhahabu si utani wa kwetu.

  Pili kisiwani humo sidhani idadi ya wanawake inafuka laki 500,000! sasa sijui nani atabahatika!
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mzee Phillemon Mikael,

  Mbona wengine sisi hatujaoa na unaanza kututamanisha mapema hivi?
   
 17. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Wadau nafikiri kabla ya kutoa au kushabikia muungano huu tujiulize Muungano
  nini/Union. Muungano ni pale nchi zinapoamua kuwa kitu kimoja,nchi zinaamua kuacha soverenity yake na kuwa kitu kimoja.Hapo hakuna serikali mbili, kinachoitwa Muungano wa Zanzibar na Tanzania si muungano haswa ni mfumo wa shirikisho/federal kwa maana kuwa nchi zinakuwa na ushirikiano katika maswala au wizara kadha hali mambo mengine kila nchi inayashughulikia kivyake,hilo ndo tatizo ambalo linatusumbua kati ya wanzanzibari na watanganyika.Zanzibar ni nchi ndani ya nchi maana ina rais na baraza la mawaziri, ina bunge lake au wawakilishi.Jambo hilo ndo linalotuyumbisha kila siku kwani hakuna muungano na wala hata hilo shirikisho nalo halipo kwani kuna serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hakuna serikali ya Tanganyika au ya bara.Sasa wacomoro wanachotaka ni muungano au ni shirikisho?muungano wetu wa Zanzibar bado una mgogoro sasa tunataka tatizo lingine tena, Tanzania hatujawa na uongozi makini unaoweza kushughulikia maswala ya nchi sasa tuwatwike mzigo mwingine ambao hawataweza kuubeba.je tamaduni zetu zinafanana? kwanini wasijiunge na jumuia kama hiyo ya Afrika Mashariki tuliyonayo. Hebu watanzania tujipe muda wakuwa tunafikiri na kutafakari tusiwe kama wanasiasa ambao hutoa maamuzi mara nyingi pasipo kufikiria (maana wana ahidi kujenga madaraja pasipo mito).
   
 18. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #18
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280

  ..teh mzalendo...kwahiyo una maoni gani kuhusu muungano na comoro kaka!

  ...lakini ujuwe hawa watu wa visiwa wana hila sana mbele ya wanawake ...zao..utaamini kati ya hofu kubwa aliyokuwa nayo karume wakati wa muungano ni uwezekano wa sisi wanyamwezi wa bara [watanganyika ]..kwenda kuwaolea wanawake zao na pesa zetu za ngombe????.....hata wazanzibar wazuri ati...lakini wabara wengi waishia kula na macho tu!!!!...comoro pia tofauti...

  ukileta ukware uende rwanda kuomba muungano ili tupate watoto wa kitutsi....basi ujiandae kulea watoto wa kufikia..hutapata wako hapo!!!,,,..utabakia kusema tu aah wanangu wamefanana na mama yao....!!

  Tujivunie tu hawa wake zetu....bahati nimeona mikoa tofauti...tunajivunia wanawake wa kitanzania[wamanyema-kigoma,chinga line,tabora[unapata mix pale],singida utapenda,mbulu,ngara,shinyanga,wahaya ,wachagga,nyakyusa,bila kusahau natural black beuty musoma...]

  Mama na dada zetu Tanzania wote ni warembo..wazuri!!!
   
 19. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kahinda,

  Watanzania watafakari nini!
   
 20. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Aah wacha wee...sisi ndio 'nchi huruma' mkuu.....Usishangae mkuu wa kaya kesho akaamka na kutaka kununua all ''toxic Assets'' kutoka Zimbabwean Banks ili nchi yao ijing'amue kiuchumi.... Sembuse Comoro....Kufika Mafia ni kimbembe lakini tutajenga daraja la kwenda Comoro, we subiri tu.
   
Loading...