Comoro yatamani Muungano na Tanzania

Muungano hauna tatizo. viongozi wetu ndo wanachangia watu wa tz wasiupende muungano.
 
Tanganyika haina haja ya kuongeza mke wa pili,huyu mmoja anatosha,kwanza anavyosumbua balaa,ooh mara anadai talaka......aaaaahh!
 
Kuvunja muungano na Zanzibar nawakati huohuo mnatamani muungano tene ni ulimbukeni na kufirisika kwa akili, mwenye mawazo hayo na akome!!
 
JF,

Raisi wa Comoro anatamani siku moja Kuwa na Muungano na Mainland kama ule wa Zanzibar! Pamoja na matatizo madogo2 Muungano na ndugu zetu wa visiwani kwa sasa je kuna haja ya Tanzania kufikiria jambo hili?

Faida Comoro watakayoitapa ni kuwa Politically Stable na hii threat ya mapinduzi na visiwa vingine kujitenga mara kwa mara itaisha! Faida kwa Tz zaidi ni kisiasa kwani hawa ni ndugu zetu na kama kuna shida itabidi tu tukawasaidie!

Tayari Exim Bank wamefungua tawi Moroni na Kiswahili kimeanza kufundishwa Chuo Kikuu cha Comoro! Pia kuna biashara kubwa tu kati yetu kwa sasa!

Komoro sii mwanachama wa SADC wala EAC kwa sasa tofauti na visiwa vingine Madagaska, Mauritius na Ushelisheli ambapo ni wanachama wa SADC!

My Take:

Inaonekana hawa jamaa tayari wametuzimia sana Tanzania haswa huyu raisi wao!

Je wakuu mnaonaje?



Source: HabariLeo | Kikwete awaonya wanasiasa Comoro
hawa hawafai-hawana tofauti na wazenji-kifupi wote ni mzigo-wanatubebesga mzigo sana-hawafai-wanataka wao wapate maendeleo at our expense-nazan siku tukiwatoa wazenji ndo hawa watajua kuwa tupo serious
 
Nadhanii huyo rais wa Comoro ameupenda Muungano wetu kutokana na kujionea na kujifunza hali halisi ya huku Bara na sio Zenji. Nashauri kama Muungano anautaka kwanza tungeuvunja huu uliopo halafu waungane Comoro na Zenji hata kwa miaka kadhaa ili wapate nchi moja tofauti na sasa hivi vitongoji viwili vya Zenji vimeungana na nchi ya Tanganyika. Baadae ndipo waje kuungana na Tanganyika ila nina wasi wasi huyo Rais anaweza kubadilika na kuchukia hii habari ya Muungano jinsi atakavyokutana na chuki, ubaguzi, unyanyasaji na ukorofi wa Wazenji wengi ambao ni watu wa kulalamika na kujihisi wanaonewa kila kukicha. Yetu macho lakini sitaki itokee kuungana na Wacomoro maana hadi sasa hivi hii ndoa tuliyonayo na hawa wazenji inakuwa ndoano, ni heri hata tungeungana na hao Comoro tokea zamani kuliko hawa jamaa wa Zenji.
 
mh,ama hapa wacomoro wanataka kuingia choo cha kike,watajuta maishao yao yote,wajukuu na vzazi vyao watawalaumu wazazi wao,
watanganyika c waaminifu,wanafik,matapeli,wezi,mbwa weuc hawa,washenz wenye kujiendesha kishenzi na kitapeli,
c wa2 wakufanya nao mahucan nao,
mcjaribu mtajuta maishani mwenu
 
Wakuu wanayotamani watu wa comoro no wengi wanatutamani lakini basi wanashindwa...kila mtu anataka muungano na tanzania,hata hawa wapwa zetu hapo unguja wanajisemea tu...lakini wote wanaopiga kelele wanazipigia wakiwa star light au oysterbay...ningewaelewa sana kama wangesusa na kuamua kupiga kelele wakiwa chakwani!

..watanzania wenzangu nyerere aliliandaa taifa letu kuwa super power ,alijuwa utajiri wa rasilimali tunao..akaulinda na akaamua kwanza ajenge utajiri wa roho....watanzania ni matajiri wa roho...tunafurahi pamoja katika umasikini wetu [watoto wa temeke wanasema kugawana umasikini]...kwani ukiwa uswahilini wakipika wanaombana chumvi na chakula kikiiva wanabadilishana mboga....jirani analeta maharage ,wewe unampa kisonzo cha kisamvu,yule analeta papa ,wewe unapeleka sangara.....hiyo ndio falsafa ya kugawana umaskini.....maskini anakula mboga saba meza moja wakati yeye alipika mboga moja tu!!!...upendo uloje watanzania!!

Ndio mwalimu alitulea hivyo ndio maana tulichanga hadi nguo zetu za ndani na zaidi damu kuchangia ukombozi kusini........!!!matajiri walio karibu yetu ambao leo karibu hali zetu zinalingana pamoja na kuwa walikuwa mbele yetu saana ....wao hawakuchangia lakini leo wote tupo!!!

Tanzania lazima iwe super power kwani baada ya mwalimu kumaliza ground work ..tunamuomba mungu tumpate joshua ....kwani mwalimu amekufa kabla hatujafika nchi ya ahadi,...Joshua hatujampata .....bado!!!...akipatikana tukijenga uwezo mkubwa wa kiuchumi ......utajiri wa mali na fedha ...ukichnganya nautajiri wa roho....sioni nchi ya kuzuia influence yetu ...hasa kwenye mataifa ya jirani ambako makaburi ya askari wetu ,damu na michango yetu ipo....!!..kikwete asikate tamaa anao uwezo wa kuwa joshua wetu akitaka na akiamua kuwa serious!!!!..

damu za ndugu zetu na michango yetu mikubwa ipo.........Uganda,zimbabwe,congo,namibia,angola,afrika ya kusini,msumbiji,re union,comoro,...etc.!!!

Tuwaandae watoto wetu kufika pale tunapotaka!!!..tutaweza..tu kama tutatokomeza ufisadi..na tamaa za wachache wanaotaka kula matunda kabla hayajaiva........mwalimu angeamua kupopoa maembe....nani angejuwa????
Ndugu yangu. Just be realistic. Si kitu kidogo kwa taifa kuwa Superpower, na hasa taifa kama Tanzania lililojaa viongozi wazembe wenye kupenda matumbo yao wenyewe kuliko maslahi ya taifa. Hata Japani ni tajiri sana lakini haijafikia mahali pa kuitwa Superpower. Kwa sasa superpower tuliyonayo hapa duniani ni Marekani tu. China nayo haiko mbali sana kufikia hatua hiyo. Mataifa mengine yote yaliyosalia hayajafika huko. Tanzania ndio kabisaaaa. Hata hapa Afrika kuna nchi zinazotuzidi, mfano South Afrika, Misri na hata Nigeria. Tunahitaji kukaza buti na kuacha uzembe. Tusijifariji kwa vitu ambavyo kiuhalisia havipo.
 
Back
Top Bottom