hali hii huwa inajirudia wakati wa siku kuu zozote kubwa za kidini. Picha hizi ni kutoka kwa
Mroki za siku ya ya Pasaka iliyopita. Wakati wa Dar ambao wamezoea kinyaa wanaendelea kuwachagua watu wale wale ambao wameshindwa kutafuta suluhisho la ukosefu wa maeneo ya kupumzika lakini maeneo ya mahoteli ya kitalii yanapatikana kwa urahisi!
Nimechambua hili katika makala yangu mojawapo ya kesho nadhani iko Tanzania Daima au MwanaHalisi.
Nimegunduwa jambo moja,kwamba kuiangalia Tanzania kwa ndani,ni tofauti sana na kuiangalia kwa nje. Sijui kama kuna tuna share the same view.
Wananchi walio wengi wamechoka mbaya....Lakini kwa opportunity by nature,wanapata upepo mwanana wa baharini. Tuna tatizo a kutokujua thamani ya tulichonacho kutokana na umasikini na level finyu ya kimaendeleo tuliyofikia,wanaoitwa viongozi wetu wanajuwa hayo lakini hawajawahi kufanya mkakati wa maana licha ya kwamba ni watu wale wale walioko miaka nenda rudi kwenye system,at least ungesema hataimaye wangejifunza,kubadilika na kuibadilisha Tanzania. Hatujui thamani ya kile tulicho nacho na ndio maana hata huwa najiuliza,hivi almasi na madini mengine ya thamani tuliyonayo,wakizira tutavifanyia nini? Si ni kama hapo juu kwenye picha,ni serikali inataka tujiulize swali kama hilo hapo juu? Kwamba beach isipouzwa basi ni kama hivi? Kweli sijui nani wa kulaumiwa kwasababu hata matumizi ya beach yenyewe sijui kama yanajulikana ama sijui kama ni culture yetu ni tofauti. Kwa mfano kwenye picha ya juu kabisa,hao jamaa waliokaa hapo mbele ukiondoa hiyo back ground,then duh,huwezi kusema ni beach kwamba hawa watu wako beach,labda walitoka kanisani ama kazini(kama wanafanya kazi siku ya pasaka)na kuamuwa kwenda kupunga upepo,swali ni kwamba sasa hapo wanachofurahia ni upepo ama maji? Wanaofurahia maji inaonekana ni wachache sana,sasa kwanini wasitafutiwe pahala pakawa oraganized wananchi hao wapunge upepo?
Nimeshawahi kufika coco beach,na sikuliona tatizo kama hili,niliona pouwa tu,sana sana upepo mzuri wa baharini ulikuwa safi sana....Lakini looking at it from outside,then you would think it should be better than that.
Kuwaletea wananchi maendeleo ni muhimu na wananchi wakiwa na uwezo wa kipato basi hata mwekezaji wa ndani anaweza kuwekeza kwenye ufukwe huo na kuufanya uwe organized na wa kuvutia zaidi.
Mwanakijiji nadhani umesema hiyo makala yako ni kesho. Nitajitahidi niisome ili niweze kuona ulichoandika kuhusiana na picha hizo. Natumaini baadhi ya maswali niliyonayo yatapata majibu humo,maswali ni mengi sana kwenye picha hizo,je tatizo ni ufukwe wenyewe kutokuwa maintained,ama ni wananchi wenye pia kutokujuwa matumizi yake? Je fuko hiyo iuzwe ili iweze kuendelezwa kutokana na kipato kitakachokuwa generated?
Najua ni wakati wa sikukuu na ndio maana kumefurika,hata hivyo si huwa panafurika wakati wa kila siku kuu hapo bongo? Na tunavyojuwa sikukuu bongo ni mara nyingi tu kwa mwaka,na hivyo ni wazi kwamba ufukwe huo ulitakiwa uendelezwe ili kukidhi mahitaji hayo. Je ufukwe huo umebinafsishwa? Na kama bado,je juhudi hizo hazitakwamishwa na wananchi hao ambao wanaonekana wao wanachotaka ni kusema tu tuko beach?
Na ndio maana huwa najiuliza sana,do we really know what we have? Na je tunajuwa thamani yake? Nasikia hata waganda wanatuzidi kwa chakula,sasa bila ya kuwaendeleza hao wananchi waliojichokea hapo,tutajikuta tunarudi utumwani,kwani viongozi wanaposafiri hawajifunzi ama ni tatizo ni nini?