Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,410
- 31,395
Kipimo cha ubaya ni uzuri, kwa waliokulia Dar, kwao Dar ni safi hadi pale watakapokwenda Moshi ndipo watagundua wanaishi mji mchafu na upo msafi hapa Tanzania. Dhana ya walio nje warudi kupambana na wasitoe mawazo ni hafifu kwani wao wameona nini tofauti na wanajaribu kuchangia.Kuchangia si lazima iwe pesa mawazo ni mchango mzuri sana. Lakini pia wamewahi kuchangia kwa hali na mali mambo mengi tusiyoyajua wengine kwa upungufu wa kutambua au habari.
Mavazi na matumizi ya beach ni jambo la mtu binafsi, mimi napenda sana beach lakini ukiniweka ndani ya karai la maji naweza kufa ninavyoogopa maji. Hii hainuzuii kubeba gazeti au kitabu changu na kwenda mahali tulivu na upepo mwanana kuburudika.
Napenda kwenda muziki lakini sipendi kucheza muziki zaidi ya kuangalia,kusikiliza na kuchanganyika na jamaa, je hizo ni sababu za kusema sijui matumizi ya kumbi za muziki au beach!. Muhimu ni mtu anajisikiaje akiwa katika eneo analolitaka na lililoandaliwa vema.
Maeneo ya burudani ni muhimu sana, katika miji yote mizuri dunia kila kata ina Park na sehemu za kuchezea wakubwa na wadogo, si siku za sikukuu bali kila siku. Dar es Salaam, park ya mnazi mmoja ni ya 'jeshi', eneo kama kinondoni na Temeke hakuna, angalia vurumai sinza hadi mwenge n.k. Wakati wa siku kuu japo basi nimtoe kijana akale 'shkrimu' kwa hiyo siku moja, dah! sijui ni wapi kama si kusimama dukani na baada ya hapo siku imekwisha. Umasikini hauna maana ya kushindwa kupata raha ya asili, au kufanya kile unachoweza japo kukupa tabasamu.
Uzembe wa beach ya coco ni zao la wananchi kwanza, kwasababu ndio wanachagua viongozi kwa rangi za vyama na si kwa maendeleo. Wakazi wa Dar wangewahoji madiwani waliopita wamefanya nini cha kuinua au kuboresha maisha yao miaka 5 iliyopita? na wakati wa kampeni walitakiwa waulize sera za diwani kuhusu mambo kama elimu, afya, burdani n.k.
Hili la beach ni kazi ya jiji lakini utashangaaa meya kila siku yupo magazetini akizundua vinywaji vya bia. Ujenzi wa beach ni mpango wa jiji kuweka taratibu zitakazomwezesha mwekezaji kutoa huduma na kupata faida bila kuwachaji wananchi(inawezekana) na wakati huo jiji linapata kodi "Quid pro quo"
Kazi ya serikali ni kusimamia sera na mipango ikiwa ni pamoja na halmashauri za miji na majiji. Tatizo la Tanzania si viongozi wasiojua, bali ni viongozi wasio 'innovative'. Kiongozi akiwa ofisini anafanya kazi kama ya yule aliyemkuta bila kubuni mbinu mbadala. Hakuna kiongozi anayetaka kuacha alama'mark', na ni hivyo hata kwa wananchi, kuna wakati kila mtaa una baa, wakati wa saloon. Hatuna innovation kuwa watu wakifuga kuku basi anzisha ka mradi ka chakula cha kuku n.k au tray za mayai n.k ni mifano tu tusivyo innovative.
Tatizo linalojadiliwa la beach ya coco ni muhimu ili ku 'set tone' ya jinsi gani tunaweza isaidia jamii yetu si kwa hili tu hata mengine. Tutavia akili tukidhani kila siku ni siasa tu, na tutakuwa wazembe tukidhani yapo mafanikio yasiyoanza na fikra na kwamba mpiganaji ni yule tu aliye msituni na sio mchora ramani au muongoza rada.
Coco beach ni uzembe wa Wananchi waliochagua madiwani na mameya wazembe wanaolelewa na serikali isiyo na ubunifu. Tutakuwa sehemu ya uzembe huu kama hatutasema, elekeza, pendekeza au kufanya. Hata mbuyu ulianza kama mchicha.