Coco Beach siku ya Pasaka (Picha)

Coco Beach siku ya Pasaka (Picha)

Hao jamaa inakuwa kama wamekaa wanapunga upepo pembeni ya bonge la dimbwi flani la maji! Halafu cheki jamaa walivyochoka...yaani choka mbaya sana. Halafu beach gani hii yenye vichaka...angalia hiyo picha ya kwanza hapo juu juu kwenye picha...hiyo ni miti au vichaka?

Halafu mbona msongamano wa watu ni mkubwa hivyo? Au ni mimi tu macho yangu?
Vichaka ni remnants of mangroves, a protected species in Tanzania, together with "Mpingo"
 
Mkuu Gembe,

Nakubaliana na wengi hapa kwamba serikali imeshindwa kufanya mambo mengi ya maana, then what next? mambo mengine sisi wananchi tuna part ya ku play hata kama serikali inashindwa.

Mfano ni hili la mazingira. Utashangaa sisi wenyewe ndio mabingwa wa kuharibu hayo mazingira, viwanja vya kuchezewa vinaporwa tumekaa tu na tunasubiri serikali. Sasa kama serikali ni hiyo tutaishia wapi?

Mimi ningetaka watu watambue kuna tatizo na wawe tayari kuchukua hatua badala ya kupiga kelele kila siku ambazo hazitusogezi popote. Watu wawe tayari kuchangia harakati za kutengeneza miji yetu.

Kila nikiangalia wanasiasa wa pande zote waliopo naona kama mawazo yao ni karibu sawa tu. Wanafanana kwa visions na matendo, labda ifike mahali wananchi tuwe tayari kwenda hatua moja mbele badala ya kupiga kelele tu ambazo kwa kweli mpaka sasa hazijatusaidia sana.

Mimi mwenzenu ni mmbishi kidogo kuilaumu serikali tuuu wakati saa zingine ni taasisi zake ndizo zinazotuangusha!

Kuna nani ameshawahi kutembelea bwalo la magereza kule ukonga? Wafungwa wametengeneza mazingira poa sana, bwalo zuri sana na magereza taarabu wanatumbuiza kule na siku hizi naona hata video nyingi wanashuti kule. Kwa nini wazee wa jiji wasitumie magereza, yaani wafungwa, kutengeneza some of the mazingira na open parks in Dar and elsewhere in Tanzania? Tunaambiwa kuna msongamano wa petty thieves in our jails - why not start chain gangs and put these petty offenders to work in cleaning up or karabatiing open spaces and parks, neighborhoods, roads, schools etc? Nimekulia Oysterbay and kwa haraka haraka tu kuna parks tatu in dire needs to be create excellent rehabilitation - At the end of Karume road coming from Oysterbay beach as if going to Ali Bin Said; at the end of Msasani road pale tulikokuwa tunaosha mbwa, na mbele yake kidogo on Kenyatta drive. I think these can be turned into jogging paths, put a couple of miniature football goalposts, and a couple of basketball, volleyball and even tennis courts, contract one of the portable toilet companies for their service-for-a-fee and if it allows have a couple of parking spots for a fee - these fees will then be used to pay for the lights and piped water. All this Kimbisa can get from our vast prison population labor.

you can also build a jogging and bicycle from the lighthouse on one end of toure drive all the way to Coco beach and then from Golden Tulip all the way to See Cliff hotel - better yet: from Golden Tulip to Sea Cliff you can build a skateboard/Rollerblade path and/or park, put some benches facing the ocean and try and preserve the natural vegetation.

Sorry, just wondering aloud...........
 
jmushi1;42966"Tatizo ni viongozi ambao tayari wamesha safiri na wanajuwa kabisa hii si sahihi."[/QUOTE said:
This what I ask myself everyday and cannot understand.
 
chondechonde acheni kusema tumechoka, hapa tunakula upepo mwanana wa bahari, the only breeze we can enjoy which is scarcely poluted by ufisadi na siasa chafu, au kwa sababu hatusemi nyie mnabeba boksi na ku-wipe wazee wa kizungu?(nursing homes).Tuheshimiane tafadhali.
 
cocobeach.jpg

cocobeach2.jpg

Nimemuona kijana naye mtambua kwenye picha! Nikamuuliza, hivi ni kitu gani kinachokupeleka coco beach wakati madhari yake haina mvuto hata kidogo! Akanijibu, "mimi naijua coco beach! kuanzia naijua mpaka leo iko hivyo hivyo, kwani inatakiwa iwaje? Na mimi nikamjibu kwa swali iko hivyo hivyo manayake nini? watu kibao ila bei za vitu na usafiri ndivyo vinakuwa shida! Nikamuuliza vipi kuhusu mazingira unaridhika nayo? Akaniuliza kivipi yaani? Nikafafanua, na maanisha mahali pa kukaa, usafi, ulinzi? Akanijibu! Duh! hayo mambo yenu nyie sasa! Koko ni kivyako vyako na washikaji kula gudtimes basi, tena ukifanikisha kufika ni mtoko babukubwa, hayo ya mazingira mi siyaoni!

Nilishtushwa sana na jibu lake, maana, unavyoona mabaya kila siku, kunawatu wanaochukulia kwamba ni hali halisi. Wanaizoe, na wanaacha kuiona!
 
Nilipoandika ile wakazi wa Dar waliozoea Kinyaa ndiyo sentiments kama hizo nilikuwa nafikiria...! Well unafikiri akiulizwa Mbunge anayewakilisha maeneo ya Coco Beach (sijui ni nani) unafikiri anaweza kuwa na majibu tofauti?
 
Hapo Maslow anakuwa applicable.

hamuwezi kuelewana kwa sababu wakati nyie mnaongelea level ya pili hapo katika jitihada za kupanda juu, wenzenu wako chini kabisa pale.

Huwezi kumfanya mtu ambaye anawaza "hela ya kula" kuhusu mazingira na habari za "beachcombing". Ndiyo maana wanasema "hayo mnajua wenyewe huko"

Granted, kuna wengine kihali (pesa) wameshatoka katika kundi la "hela ya kula" lakini mentality yao bado iko huko.You can get the kid out of the ghetto....

Sitetei, natoa analysis ya kwa nini kuna tofauti hii ya maoni.

400px-Maslow%27s_hierarchy_of_needs.svg.png
 
Nilipoandika ile wakazi wa Dar waliozoea Kinyaa ndiyo sentiments kama hizo nilikuwa nafikiria...! Well unafikiri akiulizwa Mbunge anayewakilisha maeneo ya Coco Beach (sijui ni nani) unafikiri anaweza kuwa na majibu tofauti?

Duh! Sijui hata atasema nini! La kwanza na uhakika koko haimsumbui kichwa kwani ndio anaona ni kawaida yake, na inawezekana hana msukumo wa kwenda hapo. Pili, itakapomsumbua kichwa ni pale tu ambapo mwekezaji anahitaji hilo eneo, na wananchi wakaleta ubishi. Basi hapo ataishia kusema eneo ni chafu, halijaendelezwa basi tuleta wawekezaji walete maendeleo! Sasa hayo maendeleo yanayokuja kwa kujenga beach sijui yatakuwaje! Ukimuuliza swali la tatu, je kunamuhimu gani wa coco beach kuwekwa katika madhari nzuri, akijibu kwamba leisure time is critical for state of mind and indication of economic status, tushukuru mungu! Atalosema ni sehemu ya kujiliwaza! why is it important, na kwanini iwe safi utakuwa umemchanganya.

The only thing we see today when came to leisure time is an indication of economic status, that all!
 
Hapo Maslow anakuwa applicable.

400px-Maslow%27s_hierarchy_of_needs.svg.png

If Maslow was right! our leaders were suppose to take us to change not vs verse! So Maslow is not applicable in this context, as those people who were to reach self actualization stage, are the one messing it up.
 
Nimemuona kijana naye mtambua kwenye picha! Nikamuuliza, hivi ni kitu gani kinachokupeleka coco beach wakati madhari yake haina mvuto hata kidogo! Akanijibu, "mimi naijua coco beach! kuanzia naijua mpaka leo iko hivyo hivyo, kwani inatakiwa iwaje? Na mimi nikamjibu kwa swali iko hivyo hivyo manayake nini? watu kibao ila bei za vitu na usafiri ndivyo vinakuwa shida! Nikamuuliza vipi kuhusu mazingira unaridhika nayo? Akaniuliza kivipi yaani? Nikafafanua, na maanisha mahali pa kukaa, usafi, ulinzi? Akanijibu! Duh! hayo mambo yenu nyie sasa! Koko ni kivyako vyako na washikaji kula gudtimes basi, tena ukifanikisha kufika ni mtoko babukubwa, hayo ya mazingira mi siyaoni!

Nilishtushwa sana na jibu lake, maana, unavyoona mabaya kila siku, kunawatu wanaochukulia kwamba ni hali halisi. Wanaizoe, na wanaacha kuiona!

Petu Hapa washangaza ! sasa ulitaka kijana akujibuje?
Yeye hajafika hata Morogoro au Tanga anapopajua ni Dsm.
Wewe umesafiri sana hadi ukajua sehemu nyingine duniani.Hapo Coco Beach au OysterBay kama ilivyokuwa ikifahamika ndo kafika, ndio mtoko wake.Sasa mwenye tatizo ni wewe maana ungeweza kabisa ku initiate mabadiliko pale ili wengine waone.
 
kaka! sijawake jukumu la maendeleo juu ya mwananchi wa kawaida ila nachosema mtu anapozea matatizo unaweza ukaona ni hali ya kawaida. Lakini mahojiano yangu yalikuwa ni ya mtu mmoja tu, ambayo siwezi kuyafanya ndio hali halisi, kwani yawezekana kabisa asilimia kubwa ya vijana waendao koko beach inawakyera sana.

Ila hofu yangu, ni kwamba unapokuza mtu katika mazingira mabovu, haitakuwa jambo la kushangaza akiona hakuna faida ya kutunza mazingira. Ndio wapo watakaojitokeza kupingana na hali hiyo, lakini ndio wapinde misuli kweli!

Pili kusafiri, ambako umenipachika, sio njia peke ya kuleta mwanga wa mabadiliko. mbona ukienda vijijini unakuta viwanja visafi kuliko vya mjini? Uwajibikaji unakuwa mbovu pale mifumo inapotenganisha majukumu ya watu na serikali bila serikali kutokuwa na uelewa wa majukumu yake.
 
kingeweza kufanywa kitega uchumi kizuri kama kingewekwa vizuri na kuiingizia serikali mapato
 
hali hii huwa inajirudia wakati wa siku kuu zozote kubwa za kidini. Picha hizi ni kutoka kwa Mroki za siku ya ya Pasaka iliyopita. Wakati wa Dar ambao wamezoea kinyaa wanaendelea kuwachagua watu wale wale ambao wameshindwa kutafuta suluhisho la ukosefu wa maeneo ya kupumzika lakini maeneo ya mahoteli ya kitalii yanapatikana kwa urahisi!

Nimechambua hili katika makala yangu mojawapo ya kesho nadhani iko Tanzania Daima au MwanaHalisi.

cocobeach.jpg

cocobeach2.jpg

Mie ssioni haja ya serikali kupoteza pesa, eti kuweka mazingira safi beach! Sasa hiyo beach unamtengenezea nani? Cheki hao walioko hapo, haaaa bichi wanafanya nini..... wapi ulishaona watu beach na mijigwanda michafuu, kandambili rangi tofauti. halfu mwisho wa siku kaangalie... uchafuu umetapakaa kila kona hapo. Tatizo raia bado sana wako nyuma. Labda ndo umasikini unachangia.

Lakini laazima sote tukiri kuwa Watanzania sote bado hatujawa na utamaduni wa usafi. Nakumbuka kunakuwapo na mapipa ya takataka mitaani, lakini hayakai hata siku mbili, watu wanayapiga teke. Watu wanaptupa taka nje ya pipa. na wengine wanayapeleka makwao. Badala ya kutupa taka kwenye sehemu mmoja watu wanatuma kwenye mtaro wa maji taka. Mwisho wa siku kero ikizidi tunailaumu CCM.
 
Jamaa wamechoka sana. Inaelekea wanawaza watakula nini baada ya kutoka hapo. Wengi wao wametembea kwa miguu kutoka maeneo mbalimbali ya jiji kwenda hapo kwa kukosa nauli.
 
Jamani tatizo hapa ni uchafu na sio kinyaa. Uchafu ni uchafu tu iwe unauangalia ukiwa nchini ama nje ya nchi kwa kutumia picha. Haupaswi kuwepo. Unapaswa kuondolewa. Tumeona picha za coco beach, lakinio yeyote atakayetembelea masoko yetu kama Kariakoo, Mwananyamala, Tandale, Buguruni nk. atashuhudia uchafu wa ajabu (si tatizo kama utapata kinyaa ama hutapata). Tazama mifereji ya maji machafu imeziba kwa uchafu. Sijui sisi wananchi na mamlaka zinazohusika wanahitaji kuchangamka zaidi
 
Hiyo ni nice pic rafiki !!!!! Nini kingine cha kufanya ... Angalau tuna beach nzuri na watu! Kuishi Tanzania
 
bongo iyo bwana

kweli hiyo ni bongo, mambo mengi yanahitaji kufanyiwa kazi, ukarabati wa coco beach kuifanya iwe user friendly ni mojawapo ya madogo yanayohitajika kufanyiwa kazi. hata mimi huwa najiuliza hawa viongozi wetu wa serikali na hizo safari zao nyingi za nchi za nje, hivi maendeleo yanayoyaona huko kwa wenzetu hivi huwa sio darasa kwao? na motivation tosha kuwafanya watake kufanya mazuri hayo kwa nchi yao? ewe mola tusaidie wabongo tuwe na uraia wa kuipenda nchi yetu, labda hapo ndipo tutaweza kuibadilisha
 
Back
Top Bottom