Clouds TV 360, kila atachosema rais ni ndio mzee?

Clouds TV 360, kila atachosema rais ni ndio mzee?

Tangu mh Rais akipongeze hiki kituo hasa kipindi chao cha asubuhi cha 360,wamekosa meno ya kujadili jambo lolote la rais linalompinga badala yake wao ni kuunga mkono na kupamba.

Mfano katika magazeti yaliyoripoti hotuba ya rais pale udsm,kuwa jk amemuachia kazi ngumu jpm, ndugu sam hakuisoma hiyo habari tena ndiyo iliyokuwa kubwa.
Hii imekuwa ni tabia ya kuona rais ni kama malaika,wamekosa uwezo wa kuhoji kama waandishi.

Kwa kuwa rais ni mpenzi wa kipindi chao,ni vema wakasaidia kumfikishia ujumbe hata ule mchungu maana itakuwa rahisi kwake kuufanyia kazi. Panapobidi akosolewa kwa manufaa ya uongozi wake ktk kuipeleka Tanzania mbele zaidi kimaendeleo.
Hakuna mantiki ya kupinga for the sske of kupinga. Rais kachahuliwa na Watanzania wote anawatumikia Watanzania wote.
 
Tangu mh Rais akipongeze hiki kituo hasa kipindi chao cha asubuhi cha 360,wamekosa meno ya kujadili jambo lolote la rais linalompinga badala yake wao ni kuunga mkono na kupamba.

Mfano katika magazeti yaliyoripoti hotuba ya rais pale udsm,kuwa jk amemuachia kazi ngumu jpm, ndugu sam hakuisoma hiyo habari tena ndiyo iliyokuwa kubwa.
Hii imekuwa ni tabia ya kuona rais ni kama malaika,wamekosa uwezo wa kuhoji kama waandishi.

Kwa kuwa rais ni mpenzi wa kipindi chao,ni vema wakasaidia kumfikishia ujumbe hata ule mchungu maana itakuwa rahisi kwake kuufanyia kazi. Panapobidi akosolewa kwa manufaa ya uongozi wake ktk kuipeleka Tanzania mbele zaidi kimaendeleo.
hiyo habari ya jk kumuachia jpm kazi ngumu wals sio habari nzito kwa mtu anayewaza chanya kwa jpm
 
Clouds Tv wako vizuri sana,mara nyingi wanajadili changamoto mbalimbali.Mnao ponda mmezoea kuponda na hamtaweza kuunga mkono hata kama ni jambo lenye tija.

Vizuri sana ni relative term
 
kwakuwa UKAWA mnashuparia mambo ya kipuuuzi, wengine kusifia yalio mema mnawaona wapuuuzi. UKAWA mnasusia bunge ili mkeshee baa, hamna lolote
 
Wameharibu sana hicho kipindi....!! Sasa imekuwa sifa tupu!
 
Kama gazeti la MwanaHalisi sijawahi ona likiiponda Chadema na sasa UKAWA sijui hili ni gazeti la chama
 
Tangu Buhohela avutwe karibu na baba jesca basi hao vilaza wengine wote wanamwabudu kama Mungu , hebu uteuzi wa maDC upite maana tumechoka na minafki mitaani
 
wanafiki hao wanashiriki kumfanya Pombe azidi kuchemka kwakuwa wanaogopa kumkosoa.
 
siku makonda kapewa ukuu wa wilaya kila kipindi kila mtangazaji alikua anamsifia kuanzia clouds tv mpaka redioni nikajiuliza hawa ni uhuru redio au!!!!

Hivi hlikuwa hujui kwamba hawa ni Uhuru radio and Tv?
 
Ni kweli kabisa Clouds tv wamekuwa wakimsifia magufuli toka awapigie simu na kuwaambia kuwa ,anapenda kutazama vipindi vyao
 
Ni clouds walishawahi kwenda tofaut na ccm.. Hauitaji akili kubwa kujua Hilo

Kusikiliza clouds ni kupoteza Muda wako, na unaweza ukaathiri uwezo wako wa kufikir
 
Clouds wako kibiashara. Hawako pale kukufurahisha wewe halafu mwisho wa siku hutakuwa na faida yoyote kwao. Badala yake ni afadhali wamfurahishe mkuu kwasababu anaweza kuwasaidia kurahisisha mipango yao ya biashara.

Magufuli alipoingia madarakani, wengi walikimbilia kusema ooh huu ndiyo mwisho wao. Kikwete kaondoka ikulu kwahiyo wataisikia ikulu kwenye radio. Baada ya Magufuli kupiga simu, critics wote wakabaki midomo wazi.

Clouds wamefanikiwa kuappeal kwa mkuu kwa kutumia mbinu nyepesi sana ambayo inaweza kutumika katika level yoyote ya maisha. Walichokifanya ni kutafuta udhaifu wa Magufuli na hawajapoteza muda kuexploit. Udhaifu wa Magufuli ni kupenda kusifiwa, hivyo ukifanikiwa kumsifu kwa chochote anachokifanya, basi unakuwa umeshafanikiwa kumfanya awe mtumwa wako bila kujijua.

Recommendation: Tafuteni kitabu cha "48 Laws of Power" kilichoandikwa na Robert Greene na "How to Win Friends and Influence People" cha Dale Carnegie. Vitawasaidia sana kubadilisha mitazamo yenu juu ya maisha na vitawafanya always muone maisha on the positive perspective. Maisha ni mchezo wakuu. Hilo lazima mlitambue.
 
Halafu tukumbuke hii ni kampuni binafsi jamani. Ina uhuru wa kutoa maoni yoyote wanayoyataka as long as hawavunji sheria walizowekewa na TCRA.
 
Back
Top Bottom