Clouds TV 360, kila atachosema rais ni ndio mzee?

Clouds TV 360, kila atachosema rais ni ndio mzee?

Mtoa mada unajua kusoma watu sana siku hizi wameanza kusoma hadi gazeti la uhuru ambalo lilikuwa halisomwi ukuu mbalimbali
 
Tangu mh Rais akipongeze hiki kituo hasa kipindi chao cha asubuhi cha 360,wamekosa meno ya kujadili jambo lolote la rais linalompinga badala yake wao ni kuunga mkono na kupamba.

Mfano katika magazeti yaliyoripoti hotuba ya rais pale udsm,kuwa jk amemuachia kazi ngumu jpm, ndugu sam hakuisoma hiyo habari tena ndiyo iliyokuwa kubwa.
Hii imekuwa ni tabia ya kuona rais ni kama malaika,wamekosa uwezo wa kuhoji kama waandishi.

Kwa kuwa rais ni mpenzi wa kipindi chao,ni vema wakasaidia kumfikishia ujumbe hata ule mchungu maana itakuwa rahisi kwake kuufanyia kazi. Panapobidi akosolewa kwa manufaa ya uongozi wake ktk kuipeleka Tanzania mbele zaidi kimaendeleo.
Wangeisoma wewe na umma ungefaidika nini na walipoacha kuisoma umma na wewe mmeathirika nini? Nieleze nami niwe katika mazingira mazuri kuchangia.
 
Wanasema ukitaka kumfaidi mpumbavu basi wewe msifie tu
 
siku makonda kapewa ukuu wa wilaya kila kipindi kila mtangazaji alikua anamsifia kuanzia clouds tv mpaka redioni nikajiuliza hawa ni uhuru redio au!!!!
Hao ni wazee wa fulsa huwa wanalenga maslahi yao,wako tayali kufanya loloye ili wafanikishe mahitaji yao
 
Na bado sindano zitawaingia sana, kenge nyie.Si mumwambie mzee wa kipaumbele cha kwanza elimu,cha pili elimu na cha Tatu elimu awafungulie clouds TV 360 yenu.
 
Lini Tanzania Daima limewahi kuandika habari za kumkosoa Freeman Mbowe tangu kuanzishwa kwa gazeti hilo miaka zaidi ya 10 iliyopita?
ndio leo nimejuwa kuwa Clouds ni ya CCM......................Tz Daima ni ya Chadema.
ahsante mkuu
 
Wangeisoma wewe na umma ungefaidika nini na walipoacha kuisoma umma na wewe mmeathirika nini? Nieleze nami niwe katika mazingira mazuri kuchangia.
Hiyo ilikuwa ni moja ya habari kubwa,tena ndiyo iliyobeba gazeti hilo na mengineyo,achilia mbali kukusaidia,sijui habari zote zinazosomwa kama huwa zinakusaidiaa ama laa. hapo hoja ni namna walivyoamua kuwa wamapambio wa rais na kukwepaa ama kumtetea kwa habari inayomtatiza.
unajua kuwa gazeti la uhuru ndio linachambuliwa zaidi kuliko mengine.
 
Ha hahahaha nyumbu bhana wanaumia Sana kila mahali chema chajiuza Na kujitangaza oooh wanajikomba hlf bado Unangalia tena. Raisi anajitahidi kwenye ukweli tuweni wakweli.
 
Labda ni mkakati wa kujivuta magogoni si unajua ni wazee wa fursa
Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana, hawako huru kumkosoa Rais. Wanapenda sana kumpamba Rais. Siwalaumu sana kwa kuwa ni aina yao ya uandishi wa habari.
Yuko Mwandishi anaitwa Asbert Ngurumo ana makala yake inaitwa Maswali Magumu. Yeye uandishi wake umejikita katika kuikosoa ikulu. Jamaa huwa harembi mwandiko. Na yuko kivyake, nyinyi wakati mnahangaika kuisifia ikulu yeye anaishughulikia ipasavyo. Alikuwa gazeti la Mwananchi akahamia Tanzania Daima hivi sasa sijui yuko wapi.
 
Clouds Tv wako vizuri sana,mara nyingi wanajadili changamoto mbalimbali.Mnao ponda mmezoea kuponda na hamtaweza kuunga mkono hata kama ni jambo lenye tija.
Ngoja niwakumbushe Hawa watoto,Obama alisaidiwa sana na CNN kuingiw madarakani,je Leo republican hawawezi kuichukia CNN,tatizo la Tanzania bado tupo nyuma kwa kila kitu,kula,kuoga,kutembea,maoni,arakuishi katika ndoa,sasa itakuwa kwenye maoni,clouds 360 pigeni Kazi wana mpo vema sana,achaneni na maskio yao
 
Muda wa kupindi cha clouds TV 360 kama wanavyojiita wazee wakujipambanua kukubali kukosolewa ili wasonge mbele.
 
Back
Top Bottom