Mabadiliko ya kweli ya kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo ni ndoto aliyokuwa nayo kila mtanzania na inatimia chini ya Rais Magufuli

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Wahenga wanasema ‘mnyonge mnyongeni haki yake mpeni’, Rais Magufuli watangulizi wake na CCM wapewe haki yao kwa kulifikisha taifa hapa tulipo salama. Wamelifikisha taifa mahali ambapo kila mtanzania alikuwa anategemea kuwepo siku moja na hapa tulipo ndipo tuko njiani kuelekea huko. Ndoto ya kila mtanzania ni kuona nchi yake inakua kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya ndani kama nchi na mahitaji ya nje kama ‘donor country’.

Nikinukuu kutoka katika biblia katika kitabu cha Yohan 8:32 inasema ‘mtaijua kweli , nayo kweli itawaweka huru’. Ni kweli tu itakayoiponya Tanzania, ukweli ambao mhe.Rais anatamani kila mtanzania aujue kwamba ndio kikwazo cha sisi kufika katika nchi ya ahadi, nchi iliyojaa wingi wa asali na maziwa, nchi ya ndoto ya kila mtanzania. Mhe. Rais anaitangaza kweli hiyo huku akiamini kwamba wenye nia na dhamira ovu hawatamani kuisikia ikisemwa lakini mhe.rais anataka watanzania wajue na watambue huo ukweli kwamba Tanzania ni nchi tajiri sana lakini tunaibiwa.

Kwa kuweza kuijua kweli hiyo kwa uwazi kabisa bila kificho,tunaona Tanzania ikinyanyuka kutoka kwenye kandamizo na gandamizo kubwa la fikra, ubunifu, unyonyaji na kuibiwa na kuwa huru kujilinda dhidi ya kila ovu dhidi yetu na dhidi ya rais wetu. Kweli ambayo Magufuli ameweza kuisema bila hofu ndio inaleta matokeo chanya na mabadiliko ya kweli ya kiuchumi, kisisasa na kimaendeleo.

Mabadiliko ambayo tunayaona leo ni matokeo ya juhudi, ujasiri na uzalendo wa rais wetu katika kutetea rasilimali na utu dhidi ya ubepari na manyanyaso ya muda mrefu ambao watanzania hasa wale wanyonge walikosa kwa kusemea pale ambapo jasho lao lilikuwa linaenda bure kwa kunufaisha wachache waliokuwa wanawatumia kwa manufaa yao binafsi. Kwa kufanya hivyo wanyonge hao wanaona ahadi ya mabadilko ya kweli iliyokuwa inanadiwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015 na mgombea wa CCM ikitimia na wao kuwa sehemu ya kufurahia mabadilko hayo.

Kisiasa, Rais Magufuli ameleta siasa za mgawanyo ulio sawa wa rasilimali za nchi kwa kujaribu kuweka usawa katika mishahara ya watumishi na kupunguza gharama kwa kupunguza posho na marupurupu ili kile kiasi kinachobaki kiweze kujenga uchumi na maendeleo yetu kama barabara ,reli, madaraja , shule na hopitali na miundombinu mbalimbali ambayo kila mtanzania ataitumia na atapata huduma sawa na mwingine ambaye hakubahatika kupata ajira rasmi ya serikali na kumfanya kuila keki ya taifa. Haya ni mabadiliko ya kweli ya kichumi yanayolenga kuleta usawa na mgawanyo ulio sawa wa rasilimali za umma.

Pia, Rais Magufuli atakuja kukumbukwa na vizazi vijavyo kwa kusaidia kuleta mabadiliko chanya kwa vyeo vya kisiasa, hasa kwa CCM kwa kusema kwamba mtu mmoja cheo kimoja. Kipindi kabla ya Rais Magufuli watu walitumia vyeo vya kisiasa kama silaha na mtu alikuwa na vyeo hata vitatu na kumfanya ‘untouchable’ lakini kwa Magufuli kila mtu anagusika kwa kwa sababu ana cheo kimoja na atatumia uwezo wake wote kukitumikia kwa sababu akitolewa hapo hana cheo kingine cha kumpa jeuri.

Ndoto njema za kuwa na siasa zenye kujenga uchumi na kuleta maendeleo ni ndoto ya kila mtanzania mpenda Amani na ndoto hiyo inatimia chini ya Rais Magufuli. Tanzania tumeweza kuvuka kutoka nchi kufanya kampeni muda wote hata baada ya uchaguzi kuisha na kuchagua kipindi Fulani cha kufanya kampeni. Siasa za maandamano yenye kuhatarisha maisha ya wengune zimefika mwisho na kujengwa siasa za kazi ni maendeleo.

Ujenzi mkubwa wa miundombinu kama reli, bomba la Mafuta, viwanja vya ndege, barabara,vituo vya afya na hospitali za wilaya, shule na maji kunafanya mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo kuwa ni ndoto ya kweli na inayowezekanika chini ya Uongozi wa Rais Magufuli. Wahenga wanasema haba na haba ujaza kibaba ,msemo huu unaitimia chini ya uongozi wake mpenda mabdiliko ya kweli Rais Magufuli kwa sababu tunashuhudia kibaba kwa miundombinu ikijengwa kila uchwao.

Tanzania chini ya rais Magufuli ni ndoto ambayo kila mtanzania alikuwa akiifikiria na ni ndoto ambayo mabepari na wenye nia ovu na nchi yetu wanafanya juu chini isitimie kwa kuwa ni ndoto ambayo ikitimia itatuweka huru kwelikweli na hawataki tuwe huru ndio maana hawataki ukweli usemwe watu waujue na wanatumia kila njia kuuficha hata kuwatumia baadhi ya watanzania au kuwachonganisha ama kuwachochea waamini kuwa yanayofanyika ni uhusika wa serikali na viongozi wake wakuu hasa Rais.

Tanzania ya Magufuli na CCM mpya ni tumaini lenye kuleta furaha na linaloamsha watu kuona ndoto ya Tanzania yenye mabadiliko ya kweli ya kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo inawezekana. Tumuunge mkono.

Na Karlo Mwilapwa.
 
Hivi huwa mnapata wapi muda wa kutuaminisha kwamba nchi inasonga mbele huku hata vitambulisho vya taifa mmeshindwa kuvitoa? Vile viwanda mlivyoongopea wananchi viko wapi watu wakapate ajira?
 
yeah hujakosea ni 'ndoto' na itabakia kuwa hivyo.
alafu kwanini yule DED wenu alienda kudai kodi na askari wa wanyama pori???????
 
Ndoto ya kila mtanzania ni kuona nchi yake inakua kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya ndani kama nchi na mahitaji ya nje kama ‘donor country’.
Ili ndoto itimizwe ni lazima muotaji aamke na kuanza kuifanyia kazi, lakini mpaka sasa kuna mimilioni ya watanzania wamelala wanaota kwamba ni Rais ndiye atakayeleta maendeleo wanayoyataka na waotaji wengine wanajiona tayari wapo paradiso kwa "maendeleo" yaliyopo.

Deni la Taifa linavyopaa na matumizi ya hovyo ya fedha za umma si dalili kwamba si muda mrefu tutakuwa ni "Donor Country" , labda kwenye nyanja ya kugawa aina yetu ya kipuuzi jinsi tunavyotawalana!!
 
Wahenga wanasema ‘mnyonge mnyongeni haki yake mpeni’, Rais Magufuli watangulizi wake na CCM wapewe haki yao kwa kulifikisha taifa hapa tulipo salama. Wamelifikisha taifa mahali ambapo kila mtanzania alikuwa anategemea kuwepo siku moja na hapa tulipo ndipo tuko njiani kuelekea huko. Ndoto ya kila mtanzania ni kuona nchi yake inakua kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya ndani kama nchi na mahitaji ya nje kama ‘donor country’.

Nikinukuu kutoka katika biblia katika kitabu cha Yohan 8:32 inasema ‘mtaijua kweli , nayo kweli itawaweka huru’. Ni kweli tu itakayoiponya Tanzania, ukweli ambao mhe.Rais anatamani kila mtanzania aujue kwamba ndio kikwazo cha sisi kufika katika nchi ya ahadi, nchi iliyojaa wingi wa asali na maziwa, nchi ya ndoto ya kila mtanzania. Mhe. Rais anaitangaza kweli hiyo huku akiamini kwamba wenye nia na dhamira ovu hawatamani kuisikia ikisemwa lakini mhe.rais anataka watanzania wajue na watambue huo ukweli kwamba Tanzania ni nchi tajiri sana lakini tunaibiwa.

Kwa kuweza kuijua kweli hiyo kwa uwazi kabisa bila kificho,tunaona Tanzania ikinyanyuka kutoka kwenye kandamizo na gandamizo kubwa la fikra, ubunifu, unyonyaji na kuibiwa na kuwa huru kujilinda dhidi ya kila ovu dhidi yetu na dhidi ya rais wetu. Kweli ambayo Magufuli ameweza kuisema bila hofu ndio inaleta matokeo chanya na mabadiliko ya kweli ya kiuchumi, kisisasa na kimaendeleo.

Mabadiliko ambayo tunayaona leo ni matokeo ya juhudi, ujasiri na uzalendo wa rais wetu katika kutetea rasilimali na utu dhidi ya ubepari na manyanyaso ya muda mrefu ambao watanzania hasa wale wanyonge walikosa kwa kusemea pale ambapo jasho lao lilikuwa linaenda bure kwa kunufaisha wachache waliokuwa wanawatumia kwa manufaa yao binafsi. Kwa kufanya hivyo wanyonge hao wanaona ahadi ya mabadilko ya kweli iliyokuwa inanadiwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015 na mgombea wa CCM ikitimia na wao kuwa sehemu ya kufurahia mabadilko hayo.

Kisiasa, Rais Magufuli ameleta siasa za mgawanyo ulio sawa wa rasilimali za nchi kwa kujaribu kuweka usawa katika mishahara ya watumishi na kupunguza gharama kwa kupunguza posho na marupurupu ili kile kiasi kinachobaki kiweze kujenga uchumi na maendeleo yetu kama barabara ,reli, madaraja , shule na hopitali na miundombinu mbalimbali ambayo kila mtanzania ataitumia na atapata huduma sawa na mwingine ambaye hakubahatika kupata ajira rasmi ya serikali na kumfanya kuila keki ya taifa. Haya ni mabadiliko ya kweli ya kichumi yanayolenga kuleta usawa na mgawanyo ulio sawa wa rasilimali za umma.

Pia, Rais Magufuli atakuja kukumbukwa na vizazi vijavyo kwa kusaidia kuleta mabadiliko chanya kwa vyeo vya kisiasa, hasa kwa CCM kwa kusema kwamba mtu mmoja cheo kimoja. Kipindi kabla ya Rais Magufuli watu walitumia vyeo vya kisiasa kama silaha na mtu alikuwa na vyeo hata vitatu na kumfanya ‘untouchable’ lakini kwa Magufuli kila mtu anagusika kwa kwa sababu ana cheo kimoja na atatumia uwezo wake wote kukitumikia kwa sababu akitolewa hapo hana cheo kingine cha kumpa jeuri.

Ndoto njema za kuwa na siasa zenye kujenga uchumi na kuleta maendeleo ni ndoto ya kila mtanzania mpenda Amani na ndoto hiyo inatimia chini ya Rais Magufuli. Tanzania tumeweza kuvuka kutoka nchi kufanya kampeni muda wote hata baada ya uchaguzi kuisha na kuchagua kipindi Fulani cha kufanya kampeni. Siasa za maandamano yenye kuhatarisha maisha ya wengune zimefika mwisho na kujengwa siasa za kazi ni maendeleo.

Ujenzi mkubwa wa miundombinu kama reli, bomba la Mafuta, viwanja vya ndege, barabara,vituo vya afya na hospitali za wilaya, shule na maji kunafanya mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo kuwa ni ndoto ya kweli na inayowezekanika chini ya Uongozi wa Rais Magufuli. Wahenga wanasema haba na haba ujaza kibaba ,msemo huu unaitimia chini ya uongozi wake mpenda mabdiliko ya kweli Rais Magufuli kwa sababu tunashuhudia kibaba kwa miundombinu ikijengwa kila uchwao.

Tanzania chini ya rais Magufuli ni ndoto ambayo kila mtanzania alikuwa akiifikiria na ni ndoto ambayo mabepari na wenye nia ovu na nchi yetu wanafanya juu chini isitimie kwa kuwa ni ndoto ambayo ikitimia itatuweka huru kwelikweli na hawataki tuwe huru ndio maana hawataki ukweli usemwe watu waujue na wanatumia kila njia kuuficha hata kuwatumia baadhi ya watanzania au kuwachonganisha ama kuwachochea waamini kuwa yanayofanyika ni uhusika wa serikali na viongozi wake wakuu hasa Rais.

Tanzania ya Magufuli na CCM mpya ni tumaini lenye kuleta furaha na linaloamsha watu kuona ndoto ya Tanzania yenye mabadiliko ya kweli ya kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo inawezekana. Tumuunge mkono.

Na Karlo Mwilapwa.
njaa iishie tumboni ikipanda kichwani ni balaa
 
Back
Top Bottom