Clouds TV 360, kila atachosema rais ni ndio mzee?

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
3,862
4,091
Tangu mh Rais akipongeze hiki kituo hasa kipindi chao cha asubuhi cha 360,wamekosa meno ya kujadili jambo lolote la rais linalompinga badala yake wao ni kuunga mkono na kupamba.

Mfano katika magazeti yaliyoripoti hotuba ya rais pale udsm,kuwa jk amemuachia kazi ngumu jpm, ndugu sam hakuisoma hiyo habari tena ndiyo iliyokuwa kubwa.
Hii imekuwa ni tabia ya kuona rais ni kama malaika,wamekosa uwezo wa kuhoji kama waandishi.

Kwa kuwa rais ni mpenzi wa kipindi chao,ni vema wakasaidia kumfikishia ujumbe hata ule mchungu maana itakuwa rahisi kwake kuufanyia kazi. Panapobidi akosolewa kwa manufaa ya uongozi wake ktk kuipeleka Tanzania mbele zaidi kimaendeleo.
 
Hawajitambui wamepoteza kabisa sifa ya uandishi wanajikomba mpaka wanaudhi habari hususani za ukawa huwa wanaruka bila kusoma
 
Hawajitambui wamepoteza kabisa sifa ya uandishi wanajikomba mpaka wanaudhi habari hususani za ukawa huwa wanaruka bila kusoma
 
Iko siku nao wataisoma namba kwa maana awamu hii ina mwisho. Tena ukizingatia kuwa ba Jesca hana mpango wa kuweka msingi mzuri wa katiba ili kujenga mfumo imara; atakapokuja kiongozi mwingine, wale wote wanaoimba sifa za "mtakatifu ba jesca" huku wakijua kuwa naye kazaliwa na mwanamke, wataisoma namba.

Udhalimu una mwisho!
 
Labda ni mkakati wa kujivuta magogoni si unajua ni wazee wa fulsa
siku makonda kapewa ukuu wa wilaya kila kipindi kila mtangazaji alikua anamsifia kuanzia clouds tv mpaka redioni nikajiuliza hawa ni uhuru redio au!!!!
 
Hivi kuna watu mnapoteza mda wenu kusikiliza clouds tv poleni sn, hao jamaa toka wapigiwe simu na JPM sasa kila kitu kwao ni ndyo mzee.......
 
Wale 360 wamekuwa wajinga flani hiv tangu wajue Magu anawatazama wanachambua mambo kitoto sana na biased, muda wote wanafanya vitu wakijua Rais anawatazama.
 
Lini Tanzania Daima limewahi kuandika habari za kumkosoa Freeman Mbowe tangu kuanzishwa kwa gazeti hilo miaka zaidi ya 10 iliyopita?
Clouds Tv wako vizuri sana,mara nyingi wanajadili changamoto mbalimbali.Mnao ponda mmezoea kuponda na hamtaweza kuunga mkono hata kama ni jambo lenye tija.
 
Back
Top Bottom