Clouds, Mungu anawaona kwa hiki mnachotufanyia

Clouds, Mungu anawaona kwa hiki mnachotufanyia

Kutokana na ugumu wa maisha na mzunguko wa hela kupungua na kupelekea watu kutokua na pesa za kutosha mifukoni kumeibuka na hizi kampeni za FURSA zinazoendeshwa na hawa Clouds, tena wanajinasibu kuwa kutokana na hela kuwa ngumu, hela haipatikani mifukoni, wao wanatoa fursa na kukufanya uzitambue hizo fursa, uzitumie na ujikwamue katika huu mdororo wa uchumi kwa wananchi.
ila wanatoza 10,000 kama ada ya kushiliki hizo semina.

Sasa mi nauliza hivi awa wanatoa fursa au wanatumia fursa? Kama lengo ni kuwasaidia watu wazitambue hizo fursa kwanini wasitoe bure hizo semina?

10,000 kwa mtu asiye na kazi wala mtaji si uonevu huo? Na hivi tatizo kubwa hasa ni kuwa watanzania hawazijui fursa au watanzania wanazijua hizo fursa ila hawana mitaji ya kuwafanya wazitumie hizo fursa?
Clouds wenyewe wameona fursa ndio maana nao wameitumia fursa kwa kuwakamua watu hizo kumi kumi zao.
 
Wajinga ndio waliwao. Ivi swala la fursa limeonekana mwaka huu tu? Miaka ya nyuma walikuwa wapi? Je,hapo awali hapakuwa na fursa? Hapo awali hapakuwa na wajasiliamali?
Mawingu ni wajanja sana wanachokifanya wao kwa sasa ni kutumia ukosefu wa ajira ba mdororo wa uchumi nchini na kuuita fursa kwao. Hyo elfu kumi yangu bora nimetumia nauli kwenda kariakoo kununua bidhaa za duka langu kuliko kuipoteza kwa kinachoitwa fursa
Nenda kko ukaibiwe na hiyo simu yako ya mkopo utupunguzie jam huku.
 
Mpk uone mtu kafanikiwa basi ujue kashinda vikwazo vingi sana. Ukatishwaji tamaa upo kila sehemu, cha msingi inategemea na uimara wa akili na mitazamo yako.

Usiruhusu mawazo ya watu wanaoshindwa,,, kukuchagulia maisha ya kuishi.

Leo yako unaitengeneza ww mwenyewe na si watu walioshindwa.

Jamii yetu imejaa wakatisha tamaa na wasio jiamini. Kwao kufeli na kulalamika ni sehemu ya maisha yao toka shule mpk ktk maisha ya kawaida.

Unachoingiza kichwani ndicho utachokitoa ktk maongez mpk vitendo vyako.

Ww mpenda mafanikio jiepushe sana kuambatana na watu walioshindwa na hawaamini kushinda kma kupo.

Mafanikio ni nipe nikupe theory. HONGERENI SANA CLOUDS FM.

Jamii Forum itaishi kupitia watu wenye fikra chanya tu. Wengine tutabaki kukosoa vya watu bila uthubutu.

WELL DONE CLOUDS.
Hawa ndo critical thinkers
 
Hivi kuna mtu huwa anafuatilia maendeleo ya hawa vijana wanaouhudhuria semina hizi? MONITORING & EVALUATION? au utaratibu upoje?
 
Kuna watu wanapenda tu kulalamika bila kufikiria critically kuhusu mambo. Hatutoendelea kwa roho za malalamishi
 
Kwani ulilazimishwa mkuu swala hill ni la hiyali tatizo la watanzania tunaanza kufikiri hasi mi nimefatiria kupitia tv nimenufaika sana
 
"WE OPEN UP THE WORLD FOR YOU TO BE WHAT YOU WANT"
-formular 1 katika kupiga dili ni kumtia mtu tamaa ya kipato cha haraka.
-Ili upigike(utapelike)kirahisi,penda vya bure au kipato kikubwa bila.jasho au.akili.
Karibu kwenye EDU-ENTERTAIN MENT group.
 
Ruge amekanusha madai yako.
Kiungwana ungeutoa uzi wako ingependeza zaidi
sasa huyo muliomtaja anausika nini na hoja yangu, mi sijamtaja na wala sijaitaja kampuni yake, kwani yeye ana hati miliki na hilo jina?, clouds (mawingu) ni jina tu kama majina mengine, mimi nimesema tu clouds yeye kampuni yake inaitwa clouds media!!, nyinyi ndio mmemtaja yeye ila mimi nimewataja clouds camp wa huku kwetu nanjilinji aka wazee wa FURSA.
Chezea Ruge Mzee wa Fursa?? Mazwazwa Lazima wataliwa Buku 10 zao,Nitoe elfu 10 nikamsikiliza Max Malipo au Mpoto anielezee jinsi alivyotoka? Hao wanajua siri ya mafanikio yao hawawezi kukwambia,wanaeleza juu juu tu ila figisu walizofanya hawawezi kukwambia.....ANgalieni Mpoto anavyotembea Peku huku ana VX Kilimo Kwanza ndio mambo yale unakuwa bilionea lakini unalala chini na kugonga mkeo haugongi.
 
Kutokana na ugumu wa maisha na mzunguko wa hela kupungua na kupelekea watu kutokua na pesa za kutosha mifukoni kumeibuka na hizi kampeni za FURSA zinazoendeshwa na hawa Clouds, tena wanajinasibu kuwa kutokana na hela kuwa ngumu, hela haipatikani mifukoni, wao wanatoa fursa na kukufanya uzitambue hizo fursa, uzitumie na ujikwamue katika huu mdororo wa uchumi kwa wananchi.
ila wanatoza 10,000 kama ada ya kushiliki hizo semina.

Sasa mi nauliza hivi awa wanatoa fursa au wanatumia fursa? Kama lengo ni kuwasaidia watu wazitambue hizo fursa kwanini wasitoe bure hizo semina?

10,000 kwa mtu asiye na kazi wala mtaji si uonevu huo? Na hivi tatizo kubwa hasa ni kuwa watanzania hawazijui fursa au watanzania wanazijua hizo fursa ila hawana mitaji ya kuwafanya wazitumie hizo fursa?
TAHADHARI;,
HII MADA HAIUSIANI NA CLOUDS MEDIA.
 
Screenshot_2016-12-12-22-20-20.png
hakuna kitu kibaya kama kuwa mtoto wa kiume alafu unavitabia vya umbea umbea, na ni Kazi ngumu sana kumchukia mtu aliyekuzidi almost kila kitu, sijajua lengo haswa la mtoa mada, ila atakuwa anaendeshwa sana na chuki tu.
 
Watanzania tuna wehu fulani. Umenikumbusha enzi za kakobe, muumini mmoja alinisimulia kwamba walikuwa wakiambiwa mda wa sadaka watoe kila walicho nacho mpaka mifuko igeuzwe nje ndani eti Mungu kasema hivyo. Sasa ishu ilikuwa inakuja aliyetokea mbagala na tegeta, baada ya ibada walilazimika kunyoosha msuli hadi makwao bila hata senti mfukoni na kila wiki ikawa inakuwa hivyo, kilichofata wenye pesa za madafu walianza kuishiwa mitaji wakadhoofu na kugeuka omba omba mpaka kufirisika. Hii ndo bongo, deci kila pembe ya nchi
 
Ukipata ujuzi bure hautaupa thamani maana hauja utolea kitu, ukilipia kidogo utaona umuhimu na thamani yake.. Wabongo tuache kupenda vya kupewa bure bure
Kumbe n.a. hii elimu bure ni tatizo
 
Kutokana na ugumu wa maisha na mzunguko wa hela kupungua na kupelekea watu kutokua na pesa za kutosha mifukoni kumeibuka na hizi kampeni za FURSA zinazoendeshwa na hawa Clouds, tena wanajinasibu kuwa kutokana na hela kuwa ngumu, hela haipatikani mifukoni, wao wanatoa fursa na kukufanya uzitambue hizo fursa, uzitumie na ujikwamue katika huu mdororo wa uchumi kwa wananchi.
ila wanatoza 10,000 kama ada ya kushiliki hizo semina.

Sasa mi nauliza hivi awa wanatoa fursa au wanatumia fursa? Kama lengo ni kuwasaidia watu wazitambue hizo fursa kwanini wasitoe bure hizo semina?

10,000 kwa mtu asiye na kazi wala mtaji si uonevu huo? Na hivi tatizo kubwa hasa ni kuwa watanzania hawazijui fursa au watanzania wanazijua hizo fursa ila hawana mitaji ya kuwafanya wazitumie hizo fursa?

Waliosema kuwa Wajinga ndiyo waliwao wala hawakukosea!
 
sasa huyo muliomtaja anausika nini na hoja yangu, mi sijamtaja na wala sijaitaja kampuni yake, kwani yeye ana hati miliki na hilo jina?, clouds (mawingu) ni jina tu kama majina mengine, mimi nimesema tu clouds yeye kampuni yake inaitwa clouds media!!, nyinyi ndio mmemtaja yeye ila mimi nimewataja clouds camp wa huku kwetu nanjilinji aka wazee wa FURSA.
Hauwezi Kuzungumzia Clouds na Fursa bila kumtaja huyo Jamaa,Jamaa kila issue yupo,wewe angalia hadi zile tamthilia zilizokuwa zinarushwa Clouds 69 ana mikono yake na alikuwa analamba gawio.
 
Back
Top Bottom