Clouds, Mungu anawaona kwa hiki mnachotufanyia

Hakuna madudu siyapendi kama haya yanayoitwa fursa ,kama ubongo wako hauna fursa hata ukipewa fursa huwezi itumia
 
Ebu tuwe tunazungumza vitu vya ukweli kama kitu hujui undani wake kaakimya, darasa la fursa ni bure
Kama una mb na huna cha kuongea humu nenda download porno uangalie sio kudanganya watu mtoa mada!
 
Clouds ni mafia always.....wakiongozwa na Don Corleone ....Ruge.Wanatengeneza fursa za kupigiwa magoti kila leo.
 
Wanatoa risiti..? Kama ndivyo basi si vibaya..maana wameyaona mapungufu ya Serikali yao katika kutengeneza ajira kwa Raia pamoja na kuendesha hizo semina elekezi. Kwa namna moja ziwajengee uwezo kifikra, Clouds wameyaona mapungufu nadhani pia wanaweza kuwa na SPONSERS mbali na ada wanayotoza... ila kweli Mungu anawaona....
 
Ebu tuwe tunazungumza vitu vya ukweli kama kitu hujui undani wake kaakimya, darasa la fursa ni bure
Kama una mb na huna cha kuongea humu nenda download porno uangalie sio kudanganya watu mtoa mada!
kiongozi, hizi semina zinalipiwa na katika matangazo yao husema kabisa "wai kulipia ada mapema", hakuna uongo katika hili, wnatangazaga wenyewe on air
 
ushauri wangu kwa wajasiriamali wenzangu, jifunze kwa wanaofanya sio wanaoongea. hawa inspirational speaker wanakupa moto tu maelezo yao utaona fursa ziko wazi na hela zipo tu but hawakwambii the other side ya ujasiriamali amvayo imejaa changamoto za kila namna zenye kuhitaji uvumilivu na ubunifu wa hali ya juu kutatua ili ufikie malengo yako.

hao wanaongea fursa wengi wao hata sio wajasiriamali ni waajiriwa mahali ila wanakipaji tu cha ushawishi.

ushauri wangu tafuta mentor wa eneo unalotaka ufanye ujasiriamali wako
 
Clouds wanautunia "fursa" ya watu kuwa desperate na ukata kwa vitendo. Alfu kumi kumi si mchezo ila ukiingia humo unaweza ukatoka mtupu.
 
Hivi mm kwa akili yangu timam nitoke hapa niende nikawasikilize mandondocha ( kama wewe mwenyewe huzion fursa hutoziona hata ukionyeshwa )
 
Kutokana na ugumu wa maisha na mzunguko wa hela kupungua na kupelekea watu kutokua na pesa za kutosha mifukoni kumeibuka na hizi kampeni za FURSA zinazoendeshwa na hawa Clouds, tena wanajinasibu kuwa kutokana na hela kuwa ngumu, hela haipatikani mifukoni, wao wanatoa fursa na kukufanya uzitambue hizo fursa, uzitumie na ujikwamue katika huu mdororo wa uchumi kwa wananchi.
ila wanatoza 10,000 kama ada ya kushiliki hizo semina.

Sasa mi nauliza hivi awa wanatoa fursa au wanatumia fursa? Kama lengo ni kuwasaidia watu wazitambue hizo fursa kwanini wasitoe bure hizo semina?

10,000 kwa mtu asiye na kazi wala mtaji si uonevu huo? Na hivi tatizo kubwa hasa ni kuwa watanzania hawazijui fursa au watanzania wanazijua hizo fursa ila hawana mitaji ya kuwafanya wazitumie hizo fursa?
Hujalazimishwa mkuu
Huo ukumbi nani atalipia?
Watoa seminar wasipate hata nauli ya daladala?
Kaa tu nyumbani kwako ukisubiri maisha bora
 
Mmenikumbusha taarifa moja ya semina ya kubana matumizi ambayo ada yake ilikuwa laki moja kwa wiki, nikakata shauri kwamba kutohudhuria hiyo semina nitakuwa nimefaulu mtihani wa kwanza kubana matumizi.
 
Kutokana na ugumu wa maisha na mzunguko wa hela kupungua na kupelekea watu kutokua na pesa za kutosha mifukoni kumeibuka na hizi kampeni za FURSA zinazoendeshwa na hawa Clouds, tena wanajinasibu kuwa kutokana na hela kuwa ngumu, hela haipatikani mifukoni, wao wanatoa fursa na kukufanya uzitambue hizo fursa, uzitumie na ujikwamue katika huu mdororo wa uchumi kwa wananchi.
ila wanatoza 10,000 kama ada ya kushiliki hizo semina.

Sasa mi nauliza hivi awa wanatoa fursa au wanatumia fursa? Kama lengo ni kuwasaidia watu wazitambue hizo fursa kwanini wasitoe bure hizo semina?

10,000 kwa mtu asiye na kazi wala mtaji si uonevu huo? Na hivi tatizo kubwa hasa ni kuwa watanzania hawazijui fursa au watanzania wanazijua hizo fursa ila hawana mitaji ya kuwafanya wazitumie hizo fursa?
Kwao hiyo ni fursa. Na Kama mmegundua kumezuka wimbi wa madaktari wanaofundisha kujiamini, kujitambua na kuchangamkia fursa. Semina za kuleta watoto, semina za mahusiano nk. Ushauri wangu wa bure, mjitahidi kutafuta biashara zenye mtaji mdogo. M-Minimize risk!
 
Sielewi umeandika utumbo gani hapa hivi hata kwa akili ndogo uliyonayo unawez kuwaza kuandika utumbo kama huu hivi kwanini wtz mnapenda vya bure hiyo tsh elfu 10 umeiona nyingi sana kwa mtu anayekutengenezea future yako ya baadae.... Mbona mkienda kuomba kazi maofisini mnatoa na hongo kwenye vibahasha ili mpewe kazi na ungeambiwa kipo chuo cha fursa watu wakasome for 6month ada milion moja usingeenda? Ungesubiri vya bure? Usilete hadithi za FARU JOHN hapa vya kaisari mpe kaisari vya bure wakati mwingine vinaponza kulipa kodi/ ada/ ushuru. Sio dhambi
Yeye kaongea Kama yeye. Kama kunà watu bado wanatoa na kupokea rushwa peleka taarifa Takukuru usiongee kwa kuhisi.
 
Back
Top Bottom