Barua ya wazi kwa Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE) Dar es Salaam Prof. Emaneul Mjema

LIVE THROUGH GOD

New Member
Nov 7, 2016
2
1
Mtanzania Makini

Box 0000

Dar Es Salaam

Tanzania.

Kwa Mkuu Wa Chuo

Chuo Cha Elimu Ya Biashara(CBE)

Mtaa Wa Bibi Titi

Kampasi Ya Dar Es Salaam

S.L.P 1968.

Dar Es Salaam,Tanzania.

Salaam Mkuu,

YAH: BARUA YA WAZI KWA MKUU WA CHUO CHA BIASHARA(CBE).

Kichwa cha habari hapo juu kinahusika,Bila ya kupoteza muda ningependa kuchukua wasaa huu kwanza kukupa pole ya kwa majukumu mazito uliyonayo katika nyazifa mbali mbali unazozitumikia ikiwa ni kuanzia ngazi ya familia,hadi ngazi ya utumishi wa umma,kiukweli na kwa kumuogopa MUNGU ni lazima tuwe wawazi kuwa nyadhifa ulizonazo zinakufanya upitie mambo mengi sana zikiwemo changamoto mbali mbali na mafanikio pia.

Dhumuni la barua hii ya wazi ni kutaka kuzungumza na wewe masuala machache kama sio mengi sana yahusuyo chuo chako unachokiongoza cha CBE(College Of Business Education).Hivyo dhumuni hasa la barua hii ni kutaka kujuzana,sambamba na kupashana habari mbili-tatu kuhusiana chuo chako.

1)MATOKEO YA WANAFUNZI WA INTAKE YA 2014/15

Kwa kuanza,ningependa kuzungumza suala la matokeo ya wanafunzi wanatakiwa kuingia mwaka wa tatu mwaka huu mpya wa masomo,kwa maana nyingine namaanisha wanafunzi wa intake ya mwaka 2014-15 na wale wa intake za nyuma ambao walikuwa na mitihani ya kukamilisha kabla ya kuingia mwaka wao wa mwisho yaani (Repeat Modules na wale wa Carry Forward pamoja na wale waliohairisha mwaka wa masomo kwa sababu mbalimbali).

Katika utafiti wangu nilioufanya,nimegundua kua matokeo ya mwaka huu hasa kwa wanafunzi wa digree wanaotakiwa kuingia mwaka wa tatu na wa mwisho wa masomo yao (intake ya 2014/15) hawajafanya vizuri.Takribani zaidi ya nusu ya wanafunzi wamekosa sifa za kuingia mwaka wao wa mwisho wa masomo kwa sababu kuu ya kuwa hawakufanya vizuri katika baadhi ya masomo yao makuu kwa kozi wanazosomea(Core Subjects),sina hakika juu ya idadi kamili ya wanafunzi wa intake tuizungumziayo hapa lakini kwa utafiti mdogo na wa haraka nilioufanya ni kuwa idadi ndogo kabsa ya waliopoteza sifa za kuingia mwaka wao wa mwisho haipungui wanafunzi mia sita(600) japo kuna habari nyingine ambazo hazijadhibitishwa kuwa idadi ni kubwa sana hata kufikia zaidi ya wanafunzi Elfu Moja na Mia Tano(1,500),lakini naamini idadi kamili unayo wewe,pia idadi hii ni kabla ya matokeo ya APPEAL(Rufaa) kutolewa.

Nimejaribu kuuliza baadhi ya watu,wakiwemo wanafunzi,viongozi walio katika serikali ya chuo,na baadhi ya walimu pia,wakiwemo walimu wachache ambao ni wakuu wa idara katika chuo chako juu ya suala hili la matokeo mabovu na ni jinsi gani chuo kimejipanga kukabiliana na matokeo haya,au kwa maana nyingine jinsi ya kutatua tatizo hili.Pia nilihitaji kujua sababu kuu zilizopelekea wanafunzi wengi hivi kufeli masomo hayo muhimu ambayo ndio yanayobeba kozi zao,na hapa ni baadhi tu ya majibu niliyokua nikipatiwa:

A: SABABU ZA KUTOFANYA VIZURI

i. Mfumo wa usahishaji.Kwa maelezo niliyokuwa napewa ni kuwa chuo chako kimebadili mfumo wa kusahisha mitihani.Awali mfumo wa usahihishaji mitihani ulikuwa mfumo huru zaidi japo uligubikwa na changamoto nyingi pia,mfano mitihani ilikuwa ikisahishwa na walimu mbalimbali kwa kutumia marking scheme inayokua imeandaliwa na waalimu wahusika wa somo hilo hivyo haikutoa mwanya kwa mwalimu mhusika au mwalimu mmoja kuwa ndie muamuaji wa mwisho wa jinsi anavyotaka matokeo yawe,ila usahishaji wa sasa ni tofauti kwa kuwa mwalimu mmoja wa somo ndie anaesahisha mitihani yote ya wanafunzi wake anaowafundisha,hivyo hapo kunakitu kama umakini unakosekana ukizingatia na muda mdogo wanaopewa kusahisha mitihani hiyo,pia mwalimu anakuwa na uwezo wa kuamua matokea ya mtu yaweje hasa kwa wale wenye kuwa na maelewano mabovu na walimu hao,mfano hapa kuna walimu wanatajwa kusahihisha kwa kuzingatia ni aina gani ya mahusiano aliyonayo dhidi yake na darasa analofundisha.Mfano wa waalimu waliotajwa hapa ni Mwl. Assey na mwalimu mwingine ambae inadaiwa kuwa na uswahiba mkubwa na Assey ambae ametajwa kwa jina la Mwl. Maige.Waalimu hawa wawili wanatajwa kuwa vinara wa kuwafelisha wanafunzi kwa kuzingatia mahusiano yao na wamafunzi hao na pia inadaiwa wanafunzi wamekuwa wakiwalalamikia mara kwa mara kwa wakuu wao wa kazi lakini uongozi umekuwa ukiyafumbia macho malalamiko ya wanafunzi kanakwamba wanachokifanya walimu hao ni sahihi.

ii. Ongezeko la alama ya ufaulu bila kuzingatia mazingira halisi ya ufundishaji.Hili pia limetajwa kama kikwazo kikubwa dhidi ya ufaulu wa wanafunzi,Kwa taarifa zilizopo ni kuwa awali alama ya ufaulu ilikua ni 18 na kuongezwa hadi 24 bila hata kufanyika kwa majadiliano na walengwa ambao ni wanafunzi pamoja na kuangalia hali halisi ya mazingira ya utoaji elimu wa chuo chako.Tunapozungumzia hali halizi ya mazingira ya utoaji elimu katika chuo chako ninamaanisha ufinyu wa vitendea kazi,ubora wa waalimu,ufinyu wa waalim,na mambo mengineyo yanayogusa suala la ufundishaji kwa ujumla.Aina ya waalimu ambao chuo chako kinawamiliki ni wa chache sana wenye uwezo wa kutoa ufaulu huo wa alama 24 kwenye mtihani wa mwisho,ila wengi wao bado hawana uwezo wa kwenda sambamba na ufaulu ambao chuo chako unakitaka na suala hili baadhi ya walimu niliofanya mahojiano nao wamelielezea kwa kina zaidi na kukubali kuwa uwezo wa waalimu walio wengi na hasa hasa hawa wapya ni mgumu sana kumfanya mwanafunzi afikishe alama hizo za ufaulu,pia uwepo wa waalimu wazee na wasiokua na nguvu tena ya kuandaa na kuhudhuria vipindi kama inavyotakiwa pia ni tatizo kubwa sana chuoni kwako.

iii. Rushwa. Hili pia limeonekana kama tatizo kubwa sana linalochangia wanafunzi kufanya vibaya.Hapa nilipata hadithi japo sio ya kusisimua wala kufurahisha ila ni ya ajabu sana.Hapo awali nasikia waalimu walivuna kiasi flani cha pesa japo sio kikubwa sana ila kiliwawezesha kusukuma maisha yao na familia zao huku kikiwapa motisha kubwa sana ya kufanya kazi kwa uaminifu na kwa kuzingatia misingi na maadili ya utumishi wa umma,japo kwa sasa ni kinyume na hapo zamani.Huko nyuma mitihani ilikuwa ikisahishwa morogoro,na waalimu waliochaguliwa kwenda kusahisha walikuwa wakilipwa hela za ziada tofauti na mishahara yao na hivyo kuweza kujikimu kimaisha,ila kutokana na mfumo mpya wa kusahisha mitihani,amabo unamlazimu mwalimu wa somo ndio asahishe mtihani,tena akiwa nyumabni kwake au hata mazingira ya kazi yake(ofisini) kumeondoa hela yote ya ziada ambayo waalimu walilipwa kwaajili ya kazi hiyo hivyo kumlazimu mwalimu kufanya udanganyifu kwenye kusahisha mitihani au kufanya kila linalowezekana ikiwemo kutengeneza mazingira ya wanafunzi kufeli ili kujitengenezea mianya ya RUSHWA kutoka kwa wanafunzi ili waweze kuwabatilishia matokeo yao kutoka kwenye kufeli hadi kufaulu ili kufidia zile allowances zilizotolewa na wewe mkuu wa chuo.Suala la rushwa ni kubwa sana na pia wapo walimu wanaosemekana ni vinara wa rushwa chuoni kwako na uongozi umekua ukipokea kesi zao mara kwa mara ila huzifumbia macho kwa kigezo kuwa hakuna ushahidi.

iv. Course Work. Hili pia ni moja ya sababu zinazoelezewa kuwa chanzo cha wanafunzi kupata matokeo mabaya.Hapa pande zote mbili yaana waalimu ana wanafunzi wameonekana kuwa na tatizo.Upande wa wanafunzi ni kuwa watu wengi wemekua wakiingia kwenye mtihani wa mwisho na au Course Work(c/w) ndogo sana au C/W zisizo kamilika,mfano mwanafunzi anaweza kuwa anatakiwa awe na c/w 25 kulingana na alama zake za c/w zote ila unakuta mwl amemuwekea chini ya maksi alizozipata nap engine chini ya maksi 16 huku maksi nyingine za c/w zikiwa hazijajazwa.Pia wapo wanafunzi wanaopata technical failure kwa kuwa na ujumla wa maksi chini ya 16.Kwa upande wa waalimu ni kuwa unakuta mwalimu karekodi vibaya alama za baadhi ya wanafunzi kama C/W zao hivyo kupelekea mwanafunzi kupata Technical Supplimentary.Pia kwa kipindi ambacho mwanafunzi anakua na dharura na kushindwa au kuchelewesha kufanya moja za kazi anazotoa mwalimu ambazo zinachangia c/w yake,imebainika kuwa waalimu hushindwa au hugoma kabsa kuwapa tena wanafunzi hao kazi hata kama muda bado unaruhusu au hata kama wanafunzi hao wataonyesha vielelezo vilivyowafanya kushindwa kuhudhuria kazi hizo,hapa pia wanatajwa zaidi kuwa ni mwalimu Assey,Maige.Hizo ni baadhi tu ya zile sababu muhimu zilizotajwa kama chanzo cha matokeo mabovu ya wanafunzi wa CBE.



B:JINSI YA KUKABILIANA NA MATOKEO MABAYA.

Baada ya kuzijua sababu chache zinazochangia / zilizochangia wanafunzi kufeli nilijaribu pia kukaa na baadhi ya wanafunzi kutaka kujua ni njia gani ambazo chuo kitatumia au kimepanga kutumia ili kukabiliana na matokeo haya mabaya ya mwaka huu,pia nilijaribu kufanya mahojiano na baadhi ya walimu kutaka kujua wao wameyachukuliaje matokeo haya ya mwaka huu hasa baada ya mamia ya wanafunzi kushindwa kuingia mwaka wa tatu na kitu gani kifanyike ili kuwasaidia wanafunzi hawa waliokata tama na shule baaya ya ufaulu huu mbaya..Hapa ziliibuka hoja mbali mbali kama zifuatazo:

i) Programu Maalum.Hapa pande zote mbili(Waalimu & Wanafunzi) zilitoa ushauri unaofanana,walishauri kuwa uundwe mpango madhubuti au program maalum itakayowafanya wale wote wenye matatizo na masomo ya core waendelee mwaka wao wa mwisho huku wakibeba masomo yao waliyofanya vibaya.Mfano wa program hiyo ni kuruhusu angalau wenye idadi fulani ya masomo ya core kuendelea mwaka wa tatu huku wakiyarudia masomo hayo,mfamo walio na core chini ya tatu waruhusiwe kuendelea mwaka wa tatu huku wakiyarudia masomo hayo,au mfano mwingine ni kuwa waliofanya vibaya kwenye masomo ya core ambayo masomo hayo yanafundishwa semester ya kwanza ya mwaka wa masomo waruhusiwe kuendelea na mwaka wa tatu huku wakipewa sharti la kuhakikisha wanayafaulu masomo hayo pindi wanayafanyia mitihani ili waweze kuingia mhula wa mwisho wa mwaka wa tatu pasipo kuwa na masomo ya core ambayo watakua hawajayakamilisha. Kwanini program hii ni muhimu?

(a) Kupoteza Ufadhili. Programu hii ni muhimu sana kwa sababu wanafunzi wengi husoma chini ya ufadhili wa au taasisi au watu binafsi hivyo kushindwa kwenda mwaka wa tatu kutafanya watu wa aina hii kushindwa kuendelea na masomo kwani ufadhili wao hautakuwa tayari kuwalipia ada zaidi ya ile waliyokubaliana awali hivyo watu wengi watafikia ukomo wa masomo yao pasipo kufikia malengo waliyokua nayo.

(b) Kukata Tamaa. Pia kulingana na aina ya matokeo ambayo wanafunzi wamekumbana nayo,wengi wao wamekata tamaa,hasa wanafunzi wanaosoma huku wanafanya kazi,namaanisha (TNC) kwakua wengi wao hupewa ruhusa au kibali maalum na waajiri wao ili kuweza kujiendeleza na baada ya muda wao kuisha huitajika kupisha wengine ambao wanahitaji kujiendeleza pia,hivyo kushindwa kwao kuendelea na mwaka wa tatu ni moja kwa moja kuwa wamepoteza fursa muhimu ya kuongeza elimu na kuboresha taaluma zao.Hivyo uhitaji wa program maalum ni muhimu sana katika kuokoa elimu yao.

(c) Mapato ya Chuo. Suala hili ni moja ya mambo yanosababisha uundwaji wa program maalum,pengine sababu hii yaweza kuwa sio ya muhimu sana,kwakua labda chuo kiko vizuri sana kwa upande wa fedha na matumizi yake,lakini bado haitoshi kufanya uundwaji wa program maalum kutokuzingatiwa.Takriban mapato yasiyopungua shilingi za kitanzania Billioni Moja zitakosekana kama program maalum itakayowasaidia wanafunzi hawa kuoendelea na masomo yao ya mwaka wa tatu.Hivyo ni dhahiri kabsa kuwa matokeo ya mwaka huu yataleta athari sio tu kwa wanafunzi bali hata katika uongozi upande mapato na ndio maana uundwaji wa program maalumu unahitajika kwa hali na mali.

(d) Ushindani. Hili nayo ni sababu moja muhimu sana katika kusapoti uundwaji huu wa program maalum,hapa nilipata mawazo mazuri sana kutoka kwa baadhi ya walimu wa chuo chako juu ya mambo ya kiushindani.Hapa nilijua kuwa mfumo wa chuo chako kitaaluma uko kwenye Competitive Based ambao unahimiza mtu kutoingia mwaka wa mwisho wa masomo wakati amekamatwa somo la core,tofauti na vyuo ambavyo havipo kwenye mfumo kama huo mfano IFM,TIA,AIA nk.Lakini tuliliangalia suala hili kwa undani kabisa hata kufikia kulifatilia katika ngazi ya Nacte,huko pia nilipata ufafanuzi juu ya jambo hili la Competitive Based. Ila nilichogundua hapo ni kuwa bado chuo kina mamlaka ya au kukubali kupitia kwa mkuu wa chuo kama ilivyofanya huko nyuma kama sehemu ya utafiti au kuendelea kukataa kama ambavyo imeendelea kusimamia kwenye msimamo wake wa sasa.Nikirudi kwenye suala la ushindani,chuo kinabidi kiangalie jinsi ya kufanya ili kiweze kuendana na ushindani uliopo sasa,mfano kutokana na matokeo mabaya ya sasa ambayo yamesababisha umati wa wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo yao ya mwaka wa tatu, wanafunzi wameanza kutafuta sababu za kwanini vyuo vingine vinaruhusu watu kuingia mwaka wa tatu na vingine haviruhusu,hivyo basi wao hawatakuwa tayari kuwa mabalozi wazuri wa chuo chako pale wanafunzi wanaohitaji kujiunga na vyuo watakapowaomba ushauri juu ya chuo gani ni kizuri kwaajili ya kujiunga nacho,naamini wengi watasihi kujiunga na vyuo vingine kama IFM,TIA nk kwaajili wao wanatoa nafasi ya kuendelea na masomo hadi mwaka wa mwisho hata kama kuna somo lolote lile ambalo hukufanya vyema huko nyuma,ila kwa kuzingatia tu kuwa hutaweza kuhesabika kuwa mhitimu wa masomo yako hadi pale utakapokafaulu kwenye masomo yako uliyoyabeba kama supplementary na kuingia nayo mwaka wa tatu.Hivyo kuanzishwa kwa program maalumu ni muhimu kwa kuzingatia mabo tajwa hapo juu.

2.UTOLEWAJI WA TAALUMA KWA UJUMLA KATIKA CHUO CHA CBE.

Tukiachana na mambo ya matokeo ya wanafunzi hasa ya mwaka wa pili kwenda wa tatu,kuna mambo mengine ningependa kujadili nawe ili kama ulikua huyajui basi nikufahamishe,au kama ulikua unayajua basi nikukumbushe na kukuhimiza kuwa yanapaswa kufanyiwa kazi mapema kabla hayajaleta madhara makubwa katika chuo chako pendwa.Hapa ningependa kuongelea mambo kwa kugusa Nyanja mbalimbali zinazohusu utoaji wa taaluma katika chuo chako kama ufuatavyo

1.UFUNDISHAJI KWA UJUMLA.

Ukiondoa tofauti za kiufundishaji zilizoelezewa hapo juu bado chuo chako kinabaki kati ya vyuo bora kabsa vinavyotoa taaluma nzuri hasa kwa upande biashara hapa jijini Dar Es Salaam na kwingineko kwenye matawi yenu,vitu vya kuzingatia sana hapa ni uzingatiwaji wa kuhakikisha waalimu hasa wanaoajiriwa sasa wanakuwa wanauwezo wa kutosha wa kuendana na ufaulu ambao chuo unakihitaji na kuwaondoa waalimu wanaokwamisha maendeleo ya chuo chako kwa maslahi yao binafsi,chuki nk.

Pia waalimu wanatakiwa kuzingatia muda wa vipindi vyao japo kuna waalimu wengi ambao wamekua wakifundisha kwa mazoea na mwisho wa siku wanafuzi wake wanakuja kufanya vibaya kwenye mitihani yao ya mwisho,wapo waalimu hapo chuoni kwako wamekua na tabia ya kutokuingia vipindi vya mwanzoni na wakiona mhula unaelekea mwisho ndio huanza kuingia na kuanza kuwarundikia wanafunzi mikazi isiyo na kichwa wala miguu,ndio pale unapokuta mwalimu anafundisha topic tatu kwa siku moja ili kukimbizana na muda.

2.RUSHWA NA UPENDELEO.

Najua ni vigumu sana kwa kiongozi kukabiliana na kila jambo linalotendeka kinyume na sheria na kuweza kushinda kwa asilimia mia moja,ni dhahiri kuwa hapo katikati kunda changamoto nyingi sana pia ambazo kwa namna moja au nyingine hukwamisha vita dhidi ya uhalifu huo.Ila kwa kukwambia tu ni kuwa bado chuo chako kina tafunwa na rusha iliyokithiri tena rushwa hii huzaa upendeleo kwa badhii ya washiriki katika rushwa hiyo.Bado kuna rundo la waalimu ambao wamekua wakinufaika kwa wanafunzi kufeli,wamekua wakigeuza ufaulu mbovu wa wanafunzi kama njia ya pili ya kitega uchumi chao.Nimejaribu kulifatilia sababu zinazopelekea rushwa hiyo katika chuo chako na kuambia kuwa kwa sasa waalimu hawana njia nyingine ya kujipatia pesa toka mfumo mpya wa usahishaji mitihani ulipoanza kutekelezwa ambao ulikwenda sambamba na ufutwaji wa baadhi ya allowances ambazo huko nyuma waalimu walikua wakinufaika nazo.Hivyo ukiwa kama mkuu wa chuo tunaomba ulifatilie suala hili kwa kina.

3.KAULI ZA VITISHO KUTOKA KWA WAALIMU.

Kumekuwa na baadhi ya waalimu ambao wamekua wakitoa kauli za vitisho kwa wanafunzi pale ambapo wanafunzi hulalamika kwa viongozi wao wa darasa juu ya ama ufundishaji mbovu wa walimu hao au juu ya mahudhurio yao darasani.Kama haitoshi waalimu hao huwatamkia maneno ya kuwaahidi wanafunzi juu ya kuwafanya wafeli mitihani yao ya mwisho kama njia kuwathibishia kuwa wao ndio watu muhimu sana na mwisho walioshika hatima zao za kimasomo chuoni hapo.Nilibahatika hapa kupata mifano ya walimu hao ambao nimepata habari kuwa wamekuwa wakilalamikiwa na na wanafunzi ila bila ya uongozi kuchukua hatua zozote zile.Baadhi ya walimu waliotajwa hapa ni mwl.Assey ambae pia alitajwa hapo juu ya waraka huu na mwalimu mwingine alietajwa ni Maige ambae anasemekana kuwafelisha kwa makusudi wanafunzi wa mwaka wa pili kuingia wa wa tatu wa intake ya 2014/15 na baadae kwneda kuwarubuni wanafunzi hao kuandika barua na kusema kuwa walikuwa hawaingii darasani kama njia ya yeye kuwasaidia ili awafaulishe kwa njia ya standardization na wanafunzi hao kukubali kufanya hivyo pasipo kujua kuwa mwalimu aliwarubuni ili kutengeneza defensive mechanism linapokuja suala la uongozi kutaka kumchukulia hatua.

Pia mwalimu Assey amekua akilalamikiwa kwa kutoa vitisho dhidi ya wanafunzi wanaomkosoa juu ya ufundishaji wake,amekuwa akilazimisha watu kukariri anachokiandika yeye ndio hicho hicho wanafunzi wakiandike kwenye mitihani yake kwa maneno mengine tunasema “copy and paste”.Hafundishi watu kuelewa bali anafundisha watu kukariri na mifano mizuri iko hata kwa kuangalia ufaulu wa masomo anayoyafundisha.

Assey pamoja na Maige wamekua watu wasiotaka hata kumsikiliza mwanafunzi pale anapokua na shida na hasa wanafunzi wa kiume,hawa watu wawili wamekuwa ni watu wakutoa lugha za kasha na kuudhi pale mwanafunzi anapowafata ili kuweza kupata msaada kutoka kwao,wamekua watu wasiolewa kwa nini wako hapo walipo.

Ila waalimu hawa Assey na Maige wamekua ni watu ambao hutoa misaada hata wasiyoombwa kwa watoto wa kike kwa lengo la kujiweka karibu na kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.anaweza akaenda mwanafunzi wa kiume mwenye shida ya kimasomo na hata wasimsikilize au hata wakamtolea maneno ya kashfa na kuudhi kabla ya kumuamuru atoke ofisini kwa haraka,ila cha kushangaza anaweza kwenda mwanafunzi wa kike muda huo huo na shida ileile iliyompeleka mwanafunzi wa kiume wakamkaribisha kwa ukarimu wa hali ya juu na kumtafutia hadi kiti cha kukaa na kuketi nae huko kwa muda mrefu huku wakimsikiliza na kumsaidia hata na shida nyingine ambazo hata hata hazikuhitaji usaidizi wao.

Sasa jambo hili limekuwa ni kero kubwa sana kwa wanafunzi na wanahitaji msaada wako wa hali na mali ukiwa kama mkuu wa chuo ulitafutie ufumbuzi.

4.UWAJIBIKAJI WA MKUU WA SHULE

Hapana shaka ukiwa kama mkuu chuo una mambo mengi sana ya kufanya kwa siku,elimu yako na nyazifa ulizonazo zinakufanya uwe mtu ulietingwa na mambo mengi sana nap engine una mambo mengi sana ya kufanya kuliko hata muda uliotengewa kuyafanya majukuku hayo.Ila kuhusu uwajibikaji wako kumekua na vijilawama vidogo vidogo sana ambavyo pia vikiendelea kukua vinaweza vikazaa tatizo kubwa zaidi.Kuna malalamiko kuwa wanafunzi wanapokua na shida ya kukuona wewe wamekua wakiwekewa vikwazo vingi sana ili wasipate wasaa huo,hivyo shida zao nyingi hubaki bila kutatuliwa na wasione au wasipate mtu mwingine wawezae kumwambia shida zao.

Ni dhahiri kuwa shida za wanafuzi zinakuwa na sehemu husika ya kuanzia lakini nini kifanyike kama sehemu hizo husika zimeshindwa kutatua matatizo hayo ya wanafunzi?Pengine labda hawajakwambia ila wakuu wa idara hushindwa kutatua shida za wanafunzi zinazohusu matatizo ya waalimu kwa sababu za kuoneana huruma,kujuana au hata kuoneana aibu.Watu wamejitahidi kukuandikia barua ila huwa zinazuiliwa zisikufikie hata kugongewa mhuru wa” received” inakua shida.Hivyo wanafunzi wanakuomba angalau utenge siku maalum walau mara mbili tu kwa mwezi ili kwa wale wenye shida ya kukuona waweze kupata fursa hiyo na uwekwe utaratibu usio naurasimu katika kukuona wewe.Ukiweza kufanya hivyo,niamini utajua mengi yanayotendeka katika chuo chako na itakuwa ni rahisi mno kwa wewe kuthibiti jambo lolote lisilo la kimaadili na lisilokubalika kwa mujibu wa sheria chuoni kwako.

5.MASEKRETARI WA WAKUU WA IDARA.

Moja ya vitu ambavyo vimeonekana kuwa kero chuoni hapo ni huduma zitolewazo na masekretari wa wakuu wa idara.Mara nyingi wamekua wakitoa lugha za dharau pasipo hata kujali umri wa mtu.Wanawachukulia wanafunzi kama ni watu fulani mambumbu sana pasipo kujua kuwa pasingekuwa na uwepo wao kama pasingekuwa na wanafunzi,wanashindwa kujua kuwa wanafunzi ndio mabosi zao kwakua hata huyo mkuu wa idara hawezi kulipwa pasipo uwepo wa wanafunzi.

Moja wa masekretari wanaozungumziwa hapa ni sekretari wa sasa wa idara ya Usimamizi wa Biashara (Business Administration) chini ya mkuu wa idara Mwl. Mackanja.Sekritari huyu amekua na dharau sana kwa kipindi kirefu sasa pasipo hata kubadilika,ni mtu mvivu sana na asiyejua mambo mengi pale unapoenda na shida kwake.Anajibu kwa kiburi,pasipo hata kuzingatia umri wa mtu anayemjibu,muda mwingi hujifanya yuko bize kiasi kwamba anakosa hata mda wa kukufanulia au kukutatulia shida iliyokupeleka kwake ambayo kwa mujibu wa kazi inakuwa iko ama ndani ya uwezo wake au shida hiyo ni lazima ipitie kwake kwenda kwa mhusika mkuu ambae mara nyingi ni mkuu wa idara.

Hivyo tunaomba kupitia wewe mkuu wa chuo uwasaidie wanafunzi katika kuongea na wasaidizi hao wa wakuu wa idara ili wajue wajibu wao kwa watu wanaowatumikia ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo zaidi juu ya utoaji wa huduma bora “good customer service”

6.UDHOOFU WA UHUSIANO KATI YA SERIKALI YA CHUO NA UONGOZI WA CHUO.

Kumekua na lawama za hapa na pale dhidi ya uhusiano au kuwepo kwa ufinyu wa mahusiano kati ya serikali ya chuo na uongozi wa chuo.Nimejaribu kufatilia suala hili kwa ukaribu lakini sikufanikiwa kupata sababu za kutosha kuweza kulielezea hapa,ila kwa kifupi ni kuwa serikali ya chuo kupitia kwa baadhi ya viongozi wake wakekua wakilalamika kuwa uongozi wa chuo umekuwa ukiwaweka kando hasa pale wanapoamua kukaa na kufanya ama mabadiliko au sheria mpya zinazowahusu wanafunzi.Mfano suala la ulipai wa ada kutoka kwenye awamu tatu hadi kuwa awamu mbili na masuala mengine yanayogusa taaluma ya wanafunzi wako.

Pia serikali ya chuo inalalamika kukosa msaada wa kutaka kujadili na kuangalia uwezekano wa kutatua suala la wanafunzi ambao wamekumbwa na matokeo mabaya yanayowafanya washindwe kuingia mwaka wa tatu.Ukiachilia mbali mambo hayo tajwa hapo juu,serikali ya chuo pia imekuwa ikikosa msaada wa kifedha katika muda unaotakiwa pale wanapohitaji kuendesha masuala ya kishule yanayowalenga wanafunzi wake ambo ndio kiini kikubwa cha wao kuwa madarakani.

Hivyo ukiwa kama mkuu wa chuo unaombwa kuangalia masuala hayo kwa kina ili kuweza kudumisha mahusiano kati ya uongozi wako ma serikali ya wanafunzi.

7.RUFAA YA MATOKEO.

Mkuu wa chuo kwanza napenda kukupongeza kwakua chuo chako ni moja ya vyuo vinavyowapatia haki ya msingi ya mwanafunzi yoyote asieridhika na matokeo yake na hivyo kumpa nafasi ya kukata rufaa.Lakini hapa kuna changamoto nyingi sana zinazoambatana na ukataji rufaa huu.Mfano mzuri na ambao hata mimi nimeushuhudia kwa macho yangu ni kuwa hadi tarehe ya mwisho iliyokua imewekwa kwaajili ya watu wa kukata rufaa ya matokeo ya supplementary na special exams bado mamia ya wanfunzi walikuwa hawajabahatika kupata matokeo yao yote,matokeo ya watu wengi yalikua nusu nusu (Incomplete) kwa sababu mbalimbali ambazo nyingi haziusiani na mwanafunzi hivyo watu wengi walikuja kupata majibu ya masomo yaliokuwa hayaonekani baada ya muda wa appeal kuisha hivyo hawakua na fursa tena ya kuweza kukata rufaa kwa masomo ambayo hawakuridhishwa na matokeo yake.Naamini wakuu wa idara zote ni mashahidi wa hili jambo.

Hivyo tungeomba muda wa appeal uzingatie na upatikanaji madhubuti wa matokeo ya wanafuzi.Kwa maana pale majibu ya wanafunzi wote yanapokuwa yamepatikana ndipo utengwe muda wa mwisho wa kukata rufaa,au kama inawezekana wale ambao matokeo yao yanakua na shida wapewe kiapaombele wa kukata rufaa pale matokeo yao yanapokua yamepatikana.

Suala jingine linalowachanganya wanafunzi ni jinsi appeal ya matokeo inavyofanyika kwa maana ni utaratibu gani hasa unafanyika ili mitihani hiyo kusahishwa tena?Kwakifupi wanafunzi wanapendekeza kuwa wasahishaji wa mitiani ya appeal wangekua ni watu spesho kutoka nje ya chuo ili kuziba mianya ya uonevu au hata upendeleo wakati wa usahishaji.Mfano appeal inaposahishwa na waalimu wa chuo hicho hicho(cbe) ni rahisi wa ama uonevu au upendeleo kutokea kwakua walimu wote wanakaa mazingira hayo hayo,hivyo uwepo wa waalimu kutoka vyuo vingine kutasaidia kudumisha haki kwa pande zote mbili yaani kwa wanafunzi na waalimu.

8.ULIPAJI WA ADA.

Katika moja ya vitu ambavyo wanafunzi huangalia wakati wa kutafuta chuo cha kujiunga nacho,aina ya ulipaji wa ada hua kivutio kikubwa sana hasa ukizingatia hali halisi ya maisha ya sasa.Hivyo basi ningependa kukukumbusha kuwa ulipaji wa ada wa awali amabo uliruhusu mwanafunzi kulipa kwa awamu tatu ndio uliowavutia wanafunzi wengi ulionao sasa katika chuo chako,pamoja na kuwa kuna sababu nyingine nyingi pia zilizowashawishi wanafunzi kukichagua chuo chako

Ila kitendo cha kubadilisha ghafla jinsi ya ulipaji wa ada kutoka kwenye awamu tatu hadi mbili pasipo hata kuhitaji majadiliano na walengwa ambao ni wanafunzi kwakweli ni kuwatendea ukatili wa hali ya juu sana.Angalia mustakabali wa maisha ya mtanzania wa leo,kama hadi leo takwimu zinaonyesha mtanzania anaishi chini ya dola tatu kwa siku ni dhahiri unaona ni kwa jinsi gani watanzania wanahitaji msaada,japo sio msaada wa kusoma bure bali kuwekewa mifumo rafiki ya kuweza kulipa ada.Hakika nakueleza watu inawalazimu kufanya uhalifu(kuiba),makazini kwao ili kuweza kumudu kulipa hizo awamu mbili ambayo ni laki 8 kwa awamu ya kwanza na vile vile kuweza kuikimu familia yake kwa wakati huo huo.

Hivyo basi wanafunzi wanakuomba hata kwa kukuvunjia goti kuwa utaratibu wa zamani wa kulipa ada kwa awamu tatu urudishwe au kama hilo ni gumu basi utaratibu huu mpya wa kulipa awamu tatu uanze na watu wapya wanaojiunga na chuo kwani wao tayari watakua wamejiandaa kisaikolojia kulipa ada hiyo kwa awamu mbili.


HITIMISHO.

Kutokana na wingi wa mambo yaliyojadiliwa hapa ningependa kuhitimisha kuchagua yale mambo machache muhimu kulingana na hitaji la wanafunzi walio wengi.Mkuu wa chuo,wanafunzi wako wanaomba kufanyike utaratibu utakaosaidia kuokoa nafasi ya elimu waliyopoteza baada ya kushindwa kuendelea mwaka wa tatu,japo wana nafasi nzuri ya kuyarudia masomo hayo ila wanakuomba wewe na uongozi wako kuwafikiria tena na kuweza kuwasaidia kama ambavyo wewe na uongozi wako ulivyowasaidia wanafunzi waliokuja kwako kwa kesi iliyobatizwa jina la OLD SYLLABUS ambao walikuja kulalamika kwako huku wakikosa vigezo vyote vya kuweza kusaidiwa lakini bado huruma yako iliweza kuwasaidia na kurudia mtihani kwa wale ambao hawakufanya vizuri.Kwanini nasema hawakua na vigezo vya kusaidika?Ni kwasababu moja kuu ambayo ni:

Kwa utaratibu wa kawaida ya chuo chako ni kuwa mtu yoyote anaetakiwa kurudia somo / masomo ambalo hakufanya vizuri hapo awali(alifeli) anapaswa kuhudhuria tena vipindi kama wafanyavyo wanafunzi wengine na kuhakikisha wamehudhuria semina au vipindi kwa asilimia isiyopungua themanini(80%) lakini wanafunzi hawa waliobatizwa jina la OLD SYLLABUS hawakuwa wakiudhuria darasani hata kidogo wala kutaka kujua ni aina gani ya masomo au topic zinazofundishwa katika masomo hayo,badala yake walifanya utaratibu wa kujiandikisha masomo hayo kasha kupotelea kusikojulikana hadi pale walipoonekana siku ya mtihani,hivyo kwa hali ya kawaida ilikuwa ni miujiza kwao kuweza kufaulu hasa ukizingatia aina ya ufundishaji wa masomo hayo ulibadilika kutoka kwenye mfumo wa zamani kuja mfumo mpya.

Lakini tunashukuru Mungu kuwa maombi yao ya kurudia mitihani yalikubaliwa baada ya wewe na kukaa chini na uongozi wako na kutafuta njia mbadala ya kuweza kusikiliza na kutatua shida yao kama ambavyo walipendekeza wao wenyewe japokua idadi ya watu wa OLD SYLLABUS haifiki hata robo ya idadi ya wanafunzi wa digree wa intake ya 2014/15.

Hivyo basi naomba nichukue wasaa huu kujaribu kukuomba kuangalia tena maamuzi yako dhidi ya watoto wako,wadogo zako,dada zako ambao wamekumbwa na balaa hili la kufanya vibaya kwenye masomo yao ya core ambao idadi yao ni zaidi ya wanafunzi 500 hadi 1,200 kama sio 1,700.Ninaamini uwezo wa kuwasaidia unao wewe na jopo lako la viongozi pia kwa kushirikiana na serikali ya chuo ambacho ni chombo muhimu sana katika kuunganisha mahusiano mazuri kati ya uongozi wako na wanafuzi wa chuo chako.

Pia ningependa kukushauri tena juu ya mfumo huu wa COMPETITIVE BASED ambao ndio mfumo wenu mnaoutumia kuangalia faida na athari zake,na pia kama mfumo huo ni rafiki kwa aina ya wanafunzi ulionao na pia kwa aina ya mfumo wa elimu unaohitajika na dunia ya leo.

Napenda pia kukuomba kama itawezekana uanzishe utaratibu wa angalau kuonana na wanafunzi mara moja au mbili kwa mwezi ili uweze kujua mambo baadhi ya mambo yanayofanyika hapo ambayo wewe huyafamu napengine ni vigumu kabsa kuyajua kwakua umejiwekeanukuta mkubwa kati yako na wanafunzi.

Nigependa kutanguliza shukrani zangu kwa kuweza kuusoma waraka huu na ninaomba pale nitakapokua nimekukwaza basi naomba radhi kwakua haikua dhumuni langu mimi kama mwandishi kukuudhi wewe,bali nilipenda kufikisha ujumbe wangu kwako dhidi ya mambo mbalimbali yaliyotokea na yanayoendelea kutokea katika seheme yako ya kazi.

Nasema asante sana na nakutakia kazi njema katika kufanikisha majukumu yako ya kila siku.
 

Attachments

  • Barua Ya Wazi Kwa Mkuu Wa Chuo Cha Biashara CBE.docx
    29.3 KB · Views: 163
Kwa sababu Chuo kina Campus nyingi,basi ikifika kipindi cha Usahihishaji wajumuike wote specifically kwa ajili ya kusahihisha mitihani. Kila Lecture apangiwe maswali ya kusahisha na kutoa matokeo.

Au mitihani ya Campus moja ipelekwe kwenye Campus nyingine ile kutupilia mbali mambo ya Upendeleo Rushwa.

Pili,Viongozi wa Wanafunzi wasikubali kutia sahihi matokeo pale ambapo wataona matokeo hayaridhishi bila sababu za msingi.

Mengine nitayajazia nikikaa vizuri.
 
Ndefu mno kama kitabu!anyway kuhusu pass mark hiyo ni sera ya CBE kuwa na pass mark ya juu kuliko vyuo vyote nchini.Hapo walikuwepo Kashaija, Irungu na Warioba na watu walifaulu hao unawataja sijui Maige au Assey watakuwa chamtoto tu
 
Ndefu mno kama kitabu!anyway kuhusu pass mark hiyo ni sera ya CBE kuwa na pass mark ya juu kuliko vyuo vyote nchini.Hapo walikuwepo Kashaija, Irungu na Warioba na watu walifaulu hao unawataja sijui Maige au Assey watakuwa chamtoto tu

alama 18 -25 ndiyo iko juu kuliko vyuo vyote Nchini Tanzania?
 
Prof Mjema...Mwalimu wa maintenance au sijui management au safety akiwa kule engineering...I hope he has what it takes to lead, in the age where people dare to challenge.
Katika walimu wa rika yake, ninawiwa na deni kubwa la shukrani kwa walimu kama Prof Mshana, Prof Mshoro, the Late Prof Mkilaha na Prof John mzee wa energy...kwake sina mengi zaidi ya kushangaa shangaa...Tusitegemee muujiza maana hakuna mtu atakayekupa kitu amabcho hana. Maisha yanatufundisha mengi sana kadri kila siku zinavyosonga mbele. Ngoja tuone CBE itafananaje baada ya yeye kuwepo na hata kukaa pembeni muda ukifika
 
Ndefu mno kama kitabu!anyway kuhusu pass mark hiyo ni sera ya CBE kuwa na pass mark ya juu kuliko vyuo vyote nchini.Hapo walikuwepo Kashaija, Irungu na Warioba na watu walifaulu hao unawataja sijui Maige au Assey watakuwa chamtoto tu
Hata mpumbav akikaa kimya huonekana mwelevu, ole wake mpumbav yule(wewe) aendaye mbele za watu na kufunua upumbavu wake.

TANGU LINI CBE IKAWA NA UFAULU WA JUU KULIKO VYUO VYOTE?
 
CBE now is excelling. Mwandishi anaonekana mzembe hivyo hapendi watu serious kama MAIGE NA ASSEY. Hebu vijana someni acheni 'siasa kwenye taaluma'.
 
Back
Top Bottom