Hii ina maana JF inakua (growing), ila naona baadhi ya watu hapo juu wamekuwa wakali baada ya kukosolewa...Ni budi mkumbuke kuwa ni kweli baadhi ya thread humu zimeacha kujadili hoja na kukazania personality za watu. Kwa hiyo ni muhimu kama watu wazima tukubali kuwa hapo kuna kaukweli ndani yake, ingawa kwa kiasi kikubwa mijadala mingi ni kuhusu maswala muhimu.
Nakumbuka miaka ya chama kimoja Tz, CCM walikuwa wanadai kuwa kukosoa na kukosoana ruksa, ilhali hakuna aliethubutu kufanya hivo kwa viongozi wao. Hivyo mi naona sawa tu ingawa sikusikiliza hicho kipindi ila nakubali na niko muazi kwa maoni ya watu wote hasi au chanya, bring them on!! Tukumbuke kuwa kukosolewa ni mojawapo ya kusonga mbele kwa uhakika..
Hey! wakuu sioni sababu ya kujadili suala la Kibonde na mwenzake. Let us concentrate on serious issues.
Nimesikiliza na nimesoma. Kwa muda mrefu kumekuwa na dalili za wazi kuwa hiki kipindi chao kina mlengo fulani.
Katika hoja yao leo wamesema kuwa " CCM wametangaza kampeni yao na kama wewe una kampeni yako peleka pale watatangaza" ninalotaka kujua ni kwamba jana jioni Kibonde alikuwa anaongea na nani aliyemharibia jioni yake ambaye ni mwana JF? Jitokeze na utueleze hoja yenu ilikuwa kitu gani mpaka leo tutukanwe kiasi hiki na hiki kibwana mdogo ambacho tukiamua leo kinarudi kijijini Tukuyu kwa miguu.
Angalia sana kijana hapa kuna watu wanaokupa mkate wako wa kila siku acha kutukana jamii yote. Nimechukizwa sana na maneneo yake na ni vyema atumie njia ileile kutuomba radhi sisi.
Najua pale Clouds halipwi zaidi ya posho kazi tunazompa sisi ndizo zinampa kiburi, tukifunga bomba umekufa njaa kaka. OMBA RADHI HARAKA.
KWELI kabisa,
tena nilikuwa nimpe kazi ya uMC katika harusi ya dogo mmoja hivi,itabidi nibadilishe mc,amenichefua
maybe its time all jf members tumudibishe kwa kutompa kazi.
MH lakini huruma inanijia considering his situation and majukumu mazito ya kifamilia aliyonayo