Citizen: Shisha na 'e-ciggarates' zinasababisha upungufu nguvu za kiume & changammoto ya uzazi kwa wanawake

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,830
shisha e cigarettes.jpg

Uvutaji wa shisha umekuwa kawaida nchini siku za karibuni na kukua kiasi kwamba wengine wameamua kuwa na shisha majumbani mwao. Pia siku hizi kuna sigara za kielektroniki, inatumia battery na inaunguza kimiminika kinachojumuisha nikotin, flavours na uraibu mwingine kuwa moshi ili mtu kuweza kuvuta.

Pamoja na madhara ya mapafu na kansa, ambacho hakisemwi sana ni kusababisha kupunguza ufanisi wa mfumo wa uzazi wa mwanaume na uzazi wa watoto kwa mama watarajiwa.

Gazeti la citizen liliongea na mtumiaji wa shisha na sigara za kielektroniki, alisema "Nilikuwa mtumiaji wa shisha na sigara za kielektroniki kila siku nikipumzika wakati wa chakula au majukumu yakinizonga. Nimefanya hivyo mpaka siku nilipogundua ni chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume" Alisema Brighton Makwaya, mtunzi na muimbaji mwenye miaka 31.

Makwaya anasema alitembelewa na rafiki yake wa kike na walipojaribu hakuweza kusimamisha na tatizo hilo liliendelea kujirudia na akifanikiwa hamalizi dakika mbili.

Dkt. Katanta Simwanza amesema Shisha na tumbaku vinajumuisha nikotin vinavyosababisha uzalishaji mdogo wa mbegu za kiume za zenye ubora hafifu na kufanya ziwe dhaifu.
 
Back
Top Bottom