Jinsi upandikizaji wa Uume unavyofanyika kwa wenye tatizo la Nguvu za Kiume

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1690799787888.png

Huduma ya upandikizaji uume iliyotangazwa hivi karibuni na Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma ilizua mjadala, huku wengi wakipiga simu kuulizia huduma hiyo.

Hospitali hiyo ilifanya upasuaji huo wa kwanza kwa kushirikiana na chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo nchini (TAUS) pamoja na daktari bingwa kutoka nchini na walipandikiza uume kwa watu wawili waliokuwa na matatizo ya nguvu za kiume.

Huduma hiyo hutolewa kwa mgonjwa kuwekewa vipandikizi vya plastiki vinavyoitwa silicone kwenye uume, hivyo kuwa na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kama kawaida.

Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo na uzazi wa Hospitali ya MDM Specialized, Deogratius Mahenda anasema vipandikizi hivyo vinasaidia misuli ya uume kuwa imara.

Vipandikizi hivyo ambavyo ni plastiki vinaingizwa kwenye misuli ya uume na vitaendelea kuwapo kwa maisha yote ya mhusika. Upasuaji hufanyika kwa muda wa saa moja na nusu.

Anaeleza baada ya upasuaji huo, siku saba za awali zinakuwa za uponyaji na mhusika anatakiwa asubiri kwa mwezi mmoja ndipo aanze kushiriki tendo la ndoa.

“Mwanamume aliyewekwa vipandikizi, hisia zake zitabaki palepale…kama atahitaji kupata watoto ataweza kwa kuwa utoaji wa mbegu hauathiriwi.”

Anaeleza kuwa mwanamume aliyewekewa vipandikizi hategemei mtu amvutie hisia au kuguswaguswa ndipo uume usimame.

"Mwanamume aliyewekwa vipandikizi akitaka kufanya tendo la ndoa anainyoosha, akikubaliana na mwenza wake inatosha, uume anaupindisha.

“Vipandikizi havisababishi maumivu, mhusika anaweza kushiriki tendo hilo kadiri anavyotaka kwa sababu vinauwezesha uume usimame wakati wote,” anasema na kuongeza kuwa akimaliza tendo kuna namna ya kuuweka uume usionekane kama umesimama.



Upatikanaji vipandikizi

Anasema vipandikizi vinaagizwa nje ya nchi na gharama yake inategemea na bei ya soko kwa wakati husika.

“Kulingana na uhitaji wa wagonjwa wanaopata matatizo ya nguvu za kiume, Serikali iondoe kodi kwa vipandikizi hivyo.

“Vipandikizi hivi jozi moja inauzwa kwa Euro 2,500, sasa ikiletwa hapa kwetu ikawekewa VAT asilimia 18, bado maandalizi ya upasuaji mgonjwa anaweza akajikuta akigharamia hadi kufikia Euro 5,000,” anasema Dk Mahenda. Mkurugenzi wa Kampuni ya Zephyr Surginal Implants inayosambaza vipandikizi kutoka nchini Swizerland, Raphael Llorens anasema kaka yake ambaye ni daktari amejenga kiwanda hicho baada ya kukutana na wagonjwa wenye tatizo la kukosa nguvu za kiume.

Llorena anasema vipandikizi hivyo vipo vya aina tatu; Inflatable Penile Implant, Malleable Penile Implant na Soft Penile Implant.

Anasema mwanamume anayewekewa vipandikizi hivyo anakaa navyo maisha yake yote, hufanyika baada ya sindano na dawa kushindwa kufanya kazi.

Anasema wanatarajia kuwa na maabara Tanzania ambayo itatengeneza dawa na sindano zitakazokuwa zinachomwa kwenye uume wa mwanamume, ili imsaidie kusimamisha.

Llorens alitolea mfano kwa Serikali za Ulaya huwa wananunua vipandikizi kwa ajili ya hospitali za Serikali, ili upasuaji ufanyike kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.

Anasema kama Serikali ya Tanzania itanunua vipandikizi hivyo kwa wingi, kampuni hiyo itapunguza gharama ili wananchi wenye matatizo hayo waweze kuwekewa.



Chanzo kukosa nguvu za kiume

Dk Mahenda anasema wengi wameathirika na msongo wa mawazo na matatizo ya kisaikolojia kutokana na kazi za kila siku, ugumu wa maisha na kutokuwa na maelewano mazuri na wenza wao.

Sababu nyingine ni magonjwa, mfano kisukari ambacho kinaathiri mishipa ya damu na mifumo ya fahamu pamoja na baadhi ya dawa na daktari hakuwa tayari kutaja aina hizo za dawa.

“Shinikizo la damu nayo inaharibu mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume, hivyo kuchangia changamoto hiyo,” anasema.

Pia waliopata ajali na kuvunjika uti wa mgongo na wenye matatizo ya mfumo wa fahamu kwa waliopata kiharusi, wanaweza kupata shida ya nguvu za kiume.

Wenye matatizo ya kisaikolojia, daktari anasema wanatakiwa kupatiwa ushauri nasaha pamoja na dawa, ili waondokane na tatizo hilo.

Anasema wenye matatizo ya ufahamu, magonjwa ya shinikizo la damu na sukari zipo dawa za vidonge ambazo wakitumia zitasaidia kurudisha usimamishaji wa uume katika hali ya kawaida, sindano pamoja na dawa za kupaka.

“Kwa wale ambao tiba hizo zimeshindikana wana nafasi ya kuwekewa vipandikizi kwenye uume visaidie katika usimamishaji wa kawaida wa uume,” anasema.
 
Tubadilishe tu mfumo wa maisha. Tule vizuri tulale mapema, tufanye zoezi na kuounguza mawazo.

Just imagine una 30yrs unafanya UWEKEZAJI wa kusimamisha mbo.o wa EURO 5000= 13,559,998.51.

Bado uhonge Bado ukutane na kisima bahari maziwa mto
 
Mi ntakua na shida gani nikipizi dushe inauma kinoma mpka naona uvivu kuendelea
 
Habari wakuu, kwa wasiofahamu ni kuwa kuna kuna huduma mpya ya Kupandikiza uume ambayo inatolewa na baadhi ya hospitali zetu hapa nchini, Imeelezwa kuwa gharama zake ni kati ya Milioni 6 mpaka 10.

Operesheni hiyo ya kupandikiza uume ni maalum kwa watu wenye changamoto za uume mdogo au mkubwa kupita kiasi, na nguvu za kiume kutokana na matatizo mbalimbali.

KWA MNAOFAHAMU,
Nini huwa kinafanyika katika upandikizaji huo yaani kuna kifaa huwa unafungwa au inakuwaje kuwaje?

Au unawekewa naniliu nyingine? Na huwa inatoka wapi?

Je, madhara gani yanaweza kupatikana?

(Isomeke NAULIZA hapo juu)
 
Hilo ni swali la kitaalam ameuliza Kama unajua kinachofanyika ujibu na sio kutumia lugha ngumu na majina mabaya Kwa muuliza swali. Jiheshimu nawe utaheshimika na sio Kila wakati ni masihara.
Mbona na viongozi wetu wanawaza misaada toka ulaya wakipata tunawasifu eti wamefungua nchi! Yote ni sawa tu.
 
Kwani ungekaa kimya wajibu wataalamu ungepungukiwa Nini? Kuhusu misaada hakuna nchi duniani inayojitegemea Kwa Kila kitu.
Hivi bandari na ardhi yetu, misitu yetu, SGR na epz vimeuzwa, vimekodishwa, vimebinafsishwa au vimehongwa kwa mwarabu wa Dubei?
 
Back
Top Bottom