Changamoto ya mfumo wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kushindwa kutatuliwa takriban wiki 3 sasa

DigitalPointtz

New Member
Sep 6, 2023
4
2
Ujumbe kutoka kwa kati ya mwanafunzi aliyehitimu na kuomba kupaziwa sauti.

"Mimi ni muhitimu wa stashahada ya computer science chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeyaa

Kumekuwa na tatizo la mfumo yaani SIMS (student information management system) kwa muda wa takribani wiki 3 mpaka sasa lakini hakuna jitihada zozote wanafnya kushughulikia mfumo na hii inatuumiza sisi wanafunzi.

Mpaka sasa wengine tumeshindwa kuomba hata nafasi za JKT au kujitolea katika kampuni na internships mbalimbali kwa kushindwa kupatikana kwa transcripts kama kithibitisho cha kuonesha umehitimu ngazi flani ya elimu

Wahusika wanapopigiwa simu na kutumiwa sms ili watupe alternative ya uthibitisho wa kuhitumu pale chuoni ili tuoneshe katika taasisi hawapokei simu na muda mwingine wanazima. Nimeenda ofsini kwa Head of exaamination officer 3hrs naambiwa hajafika ukipiga simu hapokei maana yake nini?.

Na baadhi ya wafanyakazi ambao wameajiriwa kama wataalamu wa IT tunawasikia wakisema kuwa wao ni IT kwa majina tu, hii inaleta picha kuwa wapo watu wamejiriwa katika taasisi flani kwa utaalamu flani lakini inapotokea tatizo hawawezi kulitatua kabisa wakati huo kuna watu wenye utaalamu huo huo na wanaweza kufanya hiyo kazi wako mitaani.

Hii inatupa changamoto kwa kweli, inaonekana bila shaka kuna hujuma inafanyika hapo.

Mpaka sasa hakuna mwanafunzi yeyote anayeweza kuingia katika mfumo, na hata wafanyakazi nao wanatoa majibu hayo hayo pale unapowafata kuomba usaidizi labda kama ni kuthibitisha malipo ya invoces na wao hawawez kuingia kwenye mfumo.

Tunaomba mtusaidie kupaza sauti tunahangaika mitaani huku na wengine wameshatumia gharama zaidi kuendlea kuishi mbeya ili wasubiri transcript hiyo bila mafanikio."



1.Tunaomba maoni yenu hii imekaaje chuo kikuu cha sayansi na teknolojia ambacho ndicho wanasema ni chuo pekee ya cha sayansi na teknolojia Tanzania kinashindwa kutatua tatizo hilo la mfumo wao wenyewe?.

2.Na inakuwaje kunakuwa na tatizo ila wahusika mnapotafutwa kutoa majibu au maelekezo ni namna gani na ni lini mtatatua tatizo hamjibu sms wala kupokea simu, huku vijana wenu wenyewe mliowazalisha hapo chuoni wanakosa fursa mbalimbali huku mitaani kisa tu hana transcript ambayo nyie kama chuo/taasisi mlitakiwa mpatie kwa wakati sahihi.

3.Lakini pia kuna wanafunzi wanaingi gharama wakiendele kusubiri hizo transcript mpaka wazazi wengine waona kama watoto wao wanawapiga pesa.
 
Back
Top Bottom