Chuo cha Madini Dodoma siwaelewi

Billion Dolar

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
1,440
Reaction score
3,249
Nina mtoto wangu amemaliza form four, amechaguliwa kwenda kusoma mining engineering chuo cha madini dodoma (MRI) nimejaribu kufuatilia website ya chuo hawana, nimepiga simu zao +255 26 230 0472 za ofisi zimefungiwa hawajalipa bill muda mrefu, nimetuma email zimekuwa rejected kwa maana email hizo hazipo.
info@mri.ac.tz
principal@mri.ac.tz

Kama kuna mtu anawajua vizuri hiki chuo msaada tafadhali namna ya kuwafikia kwa njia za kisasa sio kusafiri kwenda Dodoma. namna ya kufanya application ama kuconfirm selection maana hawajitangazi, hawafanyi kila kitu nimesearch tu hata taarifa zao zipo kwa uchache sana mpaka nawaza kama hamna kitu pale
 
Mtume mtu wako wa karibu aliye dodoma usilie lie jamiiforum.com huku hatukusaidii tuko busy na biashara zetu kama mimi hapa nina takiwa nikate ticket ya ndege kwenda Malaysia mambo ya chuo cha madini nitajuaje
 
Pale ni bonge la Chuo mzee.
Kuna shule nzito na ngumu kweli kweli.
Kama kijana wako amechaguliwa pale ni kichwa haswa.

Kipo karibu na Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP)
Kunaitwa Mipango - Anashuka Mipango (Miyuji ) kwenda madini ni Dakika 5 tu....

Nenda Dodoma
Usichezee hiyo Fursa adhimu Dogo akitoka hapo uhakika ni mkubwa kwenda GGM.
 
Hivi ndivyo inavyotakiwa Sasa. Unampa mtu info. Siyo tiketi za ndege sijui ujinga gani
 
Chuo kipo jirani na chuo cha mipango, kipo barabarani karibu na huduma zote za kijamii
 
Kipo mkuu ni njia ya kwenda Arusha kutoka Dodoma,kipo karibu na chuo cha mipango.
 
GGM hatupokei hao..chuo kilisha shuka kiwango..ilikuwa zamani..Chuo chenye Madeni mpaka kinakatiwa huduma muhimu za simu na Intaneti hakiwezi kutoa Injinia mahiri wa Mining...
 
Hawezi kuwa Engineer kutoka kwenye Chuo chenye Madeni ya huduma za simu na Intaneti bwana.
 
Kama hata hii email haipo hewani registrar@mri.ac.tz,
Jaribu kuwapigia NACTVET 0800110388, 0736 310 311.

Waeleze shida yako, itakuwa rahisi wao kukusaidia sababu wanafanya nao kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…