Chuki ya Watanzania dhidi ya watu hawa ilianzia wapi?

Ndio cha kushangaza. Hata sehemu ikifunguliwa ofisi watu wameajiriwa utaona wanachangamkia kwa kasi wanaenda kufungua migahawa, mabanda ya chips, uwakala, maduka ya rejareja na kila aina ya biashara
Halafu baadae utasikia waajiriwa ni watumwa, hawawezi kufikiria nje ya box blah blah blah, na ndio wateja wao wakubwa
Hata biashara zinapumua kwa mwisho wa mwezi 😁
 
Na sasa kuna Wimbi walio soma wana kimbilia kwenye kuji ajiri na wanafanya mambo kwa ukisasa zaidi hao viazi kazi wanayo
Mtu anaposema wasomi ni wajinga na ndio chanzo cha Africa kutoendelea alipaswa aeleze pia ni kundi gani wanaloona linachangia maendeleo ya Africa mpaka waone wasomi ndio wanarudisha nyuma juhudi zao za kuiendeleza Africa
 
Mtu anaposema wasomi ni wajinga na ndio chanzo cha Africa kutoendelea alipaswa aeleze pia ni kundi gani ndio linachangia maendeleo ya Africa mpaka waone wasomi ndio wanarudisha nyuma juhudi zao za kuiendeleza Africa
🤔
 
Wasomi sisi wachuuzi tusiosoma tunawaomba muendelee kuajiriwa ili tupate wateja. Sasa hivi mmeanza kuvamia biashara mtaani hadi mnaharibu soko. Tafadhalini bakini kwenye ajira huku mtaani kugumu tuachieni sisi wachuuzi tusiosoma.
 
Naona mpaka wahitimu wa vyuo wanafungua magenge siku hizi😁
 
Mtu anaposema wasomi ni wajinga na ndio chanzo cha Africa kutoendelea alipaswa aeleze pia ni kundi gani wanaloona linachangia maendeleo ya Africa mpaka waone wasomi ndio wanarudisha nyuma juhudi zao za kuiendeleza Africa
Tuchukulie mfano Tz. Serikalini kuna wasomi,wewe unaonaje serikali sio chanzo cha kudumaza uchumi wetu? Mashirika na taasisi za serikali kama ATCL etc zimejaa wasomi wanaofanya ubadhirifu na ndio walioua haya mashirika na wanaendelea kuyaua. Ufisadi unafanywa na nani kwa kiwango kikubwa? Sio wasomi waliopo serikalini na taasisi zake? Wasiosoma wapo wapo tu wanakamuliwa kodi na kupelekwapelekwa tu na ndio mtaji wa mafisadi. Hii nchi haitoi benefits kwa wananchi. Ingekuwa nxhi za EU ningekwambia wasiosoma jinsi walivyo mzigo maana wanakaa kusubiri benefits ili waishi ila Tz utajijuq mwenyewe.
 
Naona mpaka wahitimu wa vyuo wanafungua magenge siku hizi😁
Aisee ni shida. Mbaya zaidi wao hawategemei hizo biashara kwahio hata mkigawana wateja yeye haimuathiri. Watu wanashangaa fremu nyingi Maeneo ya kodi kubwa na biashara inasuasua zinasavaivu vipi? Hizi nyingi ni za waajiriwa na michepuko yao hazitegemei mauzo kusavaivu hela inatoka mifukoni mwa waajiriwa.
 
Wasomi sisi wachuuzi tusiosoma tunawaomba muendelee kuajiriwa ili tupate wateja. Sasa hivi mmeanza kuvamia biashara mtaani hadi mnaharibu soko. Tafadhalini bakini kwenye ajira huku mtaani kugumu tuachieni sisi wachuuzi tusiosoma.
Hakuna ajira za kutosheleza wasomi, kwa hiyo wanajiajiri
 
Tuchukulie mfano Tz. Serikalini kuna wasomi,wewe unaonaje serikali sio chanzo cha kudumaza uchumi wetu? Mashirika na taasisi za serikali kama ATCL etc zimejaa wasomi wanaofanya ubadhirifu na ndio walioua haya mashirika na wanaendelea kuyaua. Ufisadi unafanywa na nani kwa kiwango kikubwa? Sio wasomi waliopo serikalini na taasisi zake? Wasiosoma wapo wapo tu wanakamuliwa kodi na kupelekwapelekwa tu na ndio mtaji wa mafisadi. Hii nchi haitoi benefits kwa wananchi. Ingekuwa nxhi za EU ningekwambia wasiosoma jinsi walivyo mzigo maana wanakaa kusubiri benefits ili waishi ila Tz utajijuq mwenyewe.
Mambo za kiserikali hasa Afrika yana multiple factors sio usomi moja kwa moja hasa mtu akishaitwa mwanasiasa Afrika kichwa kinakuwa hakina kitu kabisa zaidi ya akili za kuvukia barabara
 
Huko serikalini kumejaa wasomi. Sisi wa 7B hatupo huko. Kwahio uozo wa serikali ni juu yao.
 
Hapana mkuu wabunge wengi ni std7, wakuu wa mikoa, wilaya, madiwani, na wakati mwingine hata raisi (kulingana na vigezo vya kielimu).

Ninachojaribu kusema ni kuwa siasa za Afrika hazithamini elimu zinathimini uchawa na kujipendekeza kutokana na katiba zetu ukileta ujuaji wako huendi popote
 
Hapo hakuna chuki ukitafakari yote yaliyoandikwa hapo ni ukweli mtupu.
Tumia muda wako vizuri ufanye research wasomi wa nchi zingine kama Dubai,Tukey,Iran,Singapore,India,Europe,USA mambo wanayofanya kisha ulinganishe na wasomi wa Africa hasa Tanzania kisha utapata majibu.
Nakumbuka miaka ya nyuma nilifanya kazi sehemu fulani hivi na mmiliki wa Kampuni(Bilionea) elimu yake ni Darasa la 7 ila alikuwa anapenda sana kuwachallenge wafanya kazi wake ambao ni degree holders.
Yaani kwenye utendaji wako wa kazi kuna maswali fulani ya Logic/Kimantiki anakuwa anakuuliza ni maswali deep ambayo kama elimu yako ni ya kukariri huwezi kujibu basi baadae wale wasomi wanababaika na kuonekana hawajui wanachokifanya mwishoni anawaponda"sasa mmesoma nini kama vitu vidogo tu hivi hamvielewi".
Mimi muda huo nakuwa nimekaa kwa pembeni nawazoom na kulinganisha hoja halafu nagundua kuwa mzee yuko sahihi ila wenyewe wasomi wanaokosolewa hawaelewi mzee anamaanisha nini.
 
Hapana sio kweli, wanachofanya wasomi wa Marekani hakina tofauti kubwa na Tanzania
Hivi unajua kuwa asilimia 90 ya graduates Marekani wanapata ajira? Wamarekani wanaoajiriwa wanafanyia kazi makampuni, sekta mbalimbali na kadhalika, hakuna tofauti na wasomi wa Tanzania wanaomaliza kusoma na kuajiriwa
Nashangaa mnaposema wasomi wa Bongo hawana ujuzi wa kutatua matatizo ya Tanzania. USA ni 1% hadi 5% tu ya wasomi ndio wanafanya hizo gunduzi za kubadili maisha ya Wamarekani. Wengine ni just regular people
Tena hii 1 to 5 percent imepatikana kwa sababu wenzetu wana R&D companies za kutosha ambazo zinawapa uzito watu wenye idea mpya
Sio kweli kwamba wasomi wa nchi zilizoendelea wana akili magical ambazo mnazitaka kutoka kwa wasomi wa Bongo

Unataka kujua kwa nini wasomi wa Marekani wana maisha mazuri? Kwa sababu wana makampuni mengi, viwanda vingi, sekta nyingi kwa hiyo hawakosi ajira, sio kwamba ni magical genius people ambao wametumia skills zao kufanya ubunifu wa kubadilisha maisha yao
Guess Marekani mtu akikosa ajira anakuwaje. Wengi hata wakifukuzwa tu kazi wanakuwa homeless ghafla, na madeni chungu nzima licha ya elimu yao kuwa bora

Nyinyi mnataka wasomi wa Tz wawe supermen kwenye nchi ambayo maisha yake ni magumu kwa most families, na mambo yamekaza kila kona
 
Unataka kujua kwa nini wasomi wa Marekani wana maisha mazuri. Kwa sababu wana makampuni mengi, viwanda vingi, sekta nyingi kwa hiyo hawakosi ajira, sio kwamba ni magical genius people ambao wametumia skills zao kufanya ubunifu wa kubadilisha maisha yao
Guess Marekani mtu akikosa ajira anakuwaje. Wengi hata walifukuzwa tu kazi wanakuwa homeless ghafla, na madeni chungu nzima licha ya elimu yao kuwa bora
👏👏👏
 
Hapana sio kweli, wanachofanya wasomi wa Marekani hakina tofauti kubwa na Tanzania
Hivi unajua kuwa asilimia 90 ya graduates Marekani wanapata ajira? Wamarekani wanaoajiriwa wanafanyia kazi makampuni, sekta mbalimbali na kadhalika, hakuna tofauti na wasomi wa Tanzania wanaomaliza kusoma na kuajiriwa
Nashangaa mnaposema wasomi wa Bongo hawana ujuzi wa kutatua matatizo ya Tanzania. USA ni 1% hadi 5% tu ya wasomi ndio wanafanya hizo gunduzi za kubadili maisha ya Wamarekani. Wengine ni just regular people
Tena hii 1 to 5 percent imepatikana kwa sababu wenzetu wana R&D companies za kutosha ambazo zinawapa uzito watu wenye idea mpya
Sio kweli kwamba wasomi wa nchi zilizoendelea wana akili magical ambazo mnazitaka kutoka kwa wasomi wa Bongo

Unataka kujua kwa nini wasomi wa Marekani wana maisha mazuri? Kwa sababu wana makampuni mengi, viwanda vingi, sekta nyingi kwa hiyo hawakosi ajira, sio kwamba ni magical genius people ambao wametumia skills zao kufanya ubunifu wa kubadilisha maisha yao
Guess Marekani mtu akikosa ajira anakuwaje. Wengi hata wakifukuzwa tu kazi wanakuwa homeless ghafla, na madeni chungu nzima licha ya elimu yao kuwa bora

Nyinyi mnataka wasomi wa Tz wawe supermen kwenye nchi ambayo maisha yake ni magumu kwa most families, na mambo yamekaza kila kona
Hoja yako umejitahidi kudefend ila umetoka nje ya mada kidogo.
Mimi kwenye hoja yangu siongelei mambo ya kuwa na pesa au kuwa maskini.
Mimi naongelea wasomi kuwa na uwezo mpana,kureason according to the situation/analysing things in normal life,kufanya vitu vyenye tija na kuleta impact kwa jamii.
Pia siongelei kuhusu kupata au kukosa ajira ila jambo la msingi hapa ni je ukishapewa hiyo ajira unaitumia vipi hiyo nafasi ya ajira?ufanisi wako na utendaji wako je unaleta tija?
Pia Siongelei habari ya msomi kuwa na hela au kutembelea Benz hizi ni showoff ambazo hata wakina Mwijaku na Doto Magari au Chief Godlove wanazifanya.
Labda ngoja nikupe mfano mmoja halisi ili unielewe vizuri;tutolee mfano wasomi walioajiriwa kwenye kampuni/shirika la UDART/BRT(Mwendokasi) kampuni inakufa kwa kupata abiria wengi lakini huduma mbovu,wakati wa mvua mabasi yanaingia matope wanayadump na hawajui wafanye nini wanangojea hadi Rais aje awafundishe jinsi ya kufanya.
Wewe unadhani hao wafanyakazi kuanzia Mkurugenzi wanajua hata wanachokifanya hapo maofisini kwao?
 
Kitu ambacho hujui ni kwamba kokote dunia hii, wafanyakazi incompetent wamejaa sana
Ni vile huku hakuna sheria kali za kuwawajibisha wafanyakazi wazembe ndio maana unaona mradi wa mwendokasi unasuasua
Ila uzembe upo dunia nzima, kila sehemu ina watu walio serios na wajinga wajinga. Ili organization iwe stable inabidi kuwe na mfumo unao discourage ujinga kazini
Wala sio kosa la wasomi wa Bongo kama unavyodai
 
Wivu mkuu
Nimesoma comments nyingi hapa zinakubaliana na maoni ya mleta mada. Mimi nadhani haya ni maoni yake kwa sababu nipo kwenye social media sana na kundi ambalo ni dhahiri kabisa linachukiwa sana na watanzania ni wanasiasa wa CCM. Hawa sasa hivi wanachukiwa kuliko shetani mwenyewe hasa baada ya 29/10
 
Mimi huwa naonaga kuna ile umefanya kitu kwa aina tofauti "utasikia uyu naye kujifanya msomi"

Ile mimi sihesabu kama chuki,ni aina tu ya mtu anakusifia ila kwa reverse maneno lakini anakuwa tayari kakubaliana na wewe.

Chuki ambayo naweza kuita chuki mfano,jinsi wananchi wanavyoonesha kwa viongozi wao wakifariki siku hizi,ile ni pure chuki.

Au ile ambayo jamii za mikoani wanavyokuwa treated wakifika maeneo ya pwani,ile ni chuki halisi...
Uko sahihi mno. Sijui mwanzisha mada anaishi wapi ambako waalim au wasomi wanachukiwa. Kazi ya ualimu wengi wanaidharau (siyo kuchukia waalim). Hata ''wasomi'' wanaochukiwa ni hawa ma ''Dr'' feki kama Samia na siyo wasomi wa kweli. Chuki ya watanzania iko kwa viongozi wa CCM.
 
Nipe mfano wa taasisi tatu ambazo wasomi wake wanafanya kazi kwa uweledi na wameleta impact?maana umesema kwenye kila nchi kuna wazembe na waweledi

Back
Top Bottom