Chuki na UDSM hakuna aliyekutuma Ufeli

Chuki na UDSM hakuna aliyekutuma Ufeli

UDSM chenyewe wanafunzi wanasoma wanahitimu hata kuandika insha hawajui.

Hicho ndicho chuo kinagombaniwa.

Kweli ukiwa jangwani hata matope utaita maji safi.

Nilivyokuwa nasoma A Levels enzi zangu, nilikuwa napenda sana Particle/ theoretical Physics.

Nikawa naenda UDSM kuangalia library yao, imechooka, vitabu vya tangu ukoloni.

Nikaenda American Library Peugeot House nikakuta vitabu vya mwaka mmoja uliopita vyenye latest updates vipo.

Nikaona tunacheza.
Mtu anasoma Engineering unataka aandike Insha kama Mwandishi wa habari.

umeongea uongo mkubwa sana. Udsm mtu asijue kuandika insha. Looh!
Unachanganya Vyuo mkuu
 
Ehheheh yaan wanavyojisifu sasa duu,,ni kupoteza tu pesa
Mnajifariji sana.

Mtu form six apate "A" Kwenye somo la history na Kiswahili alafu mtu aje aseme eti Udsm hawajui kuandika Insha. Looh! Kazi kweli kweli
 
Acheni kukikweza, UDSM si chuo cha kujisifia kiiovo ni sawa tu sawa na vyengine, tena hizi sifa zake Hazina tofauti na chama tawala ni mjina mkubwa tu hakunaga chochote zaidi ya kukopiana tuu
 
Mtu anasoma Engineering unataka aandike Insha kama Mwandishi wa habari.

umeongea uongo mkubwa sana. Udsm mtu asijue kuandika insha. Looh!
Unachanganya Vyuo mkuu
Mtu yeyote aliyehitimu Shule ya Sekondari tu, aliyesoma mchepuko wowote, inabidi ajue kuandika insha.

Hizi habari za kwamba umesoma Engineering eti ndiyo hutakiwi kujua kuandika insha ndiyo ujinga ninaousema mnahitimu lakini hamjamaliza ujinga wa msingi kabisa.
 
Kitu cha kujifunza ndugu yangu:
Elimu na Akili siyo kusoma Chuo kama UDSM au MZUMBE..Unaweza kusoma hapo na kupata PhD lakini kwenye soko la kimataifa hata usionekane na wala usichangie lolote kwenye ulimwengu wa taaluma au kwenye jamii. Au hata kusoma Ulaya au Marekani lakini bado ukaishia kuwa zwazwa tu.

Leo hii hao wasomi unaotaka kuwasifia wameshindwa kabisa kutatua matatizo ya nchi hii na wengine hata kujikwamua kimaisha wameshindwa, lakini unakuta mfanyabishara wa kikinga pale Kariakoo aliyeishia form four au darasa la saba anasaidia jamii kwenye kodi na kutoa ajira.

Vyeti vinakudanganya sana wewe.
Badilika, UDSM ni chuo cha kawaida sana kwa sasa.
Ahsante sana Mkuu Malcom Lumumba. Kwanza nipende kukupongeza kwa kuona Uzi wangu. Ni jambo la Sifa Uzi Wangu kupitiwa na mtu kama wewe.

Huwa nafuatilia nyuzi zako zenye jumbe kadha wa kadha zenye kujenga sana kiakili. Nikupongeze na kuzidi kukutia shime kwa kazi bora.

Nikirudi kwenye mada;. Madai uyasemayo yana chembe ya Ukweli kwa kiasi Fulani.

Naelewa ulicholenga na ulichokusudia watu wakibebe katika andiko lako.

Nikichokisema hapo si zaidi ya kuwasihi wale walioachwa kuchaguliwa na Udsm kisa wamekosa kigezo cha ufaulu yakuwa waache chuki kwani hakuna aliyewatuma wafeli.

Suala la michango kwenye jamii ni suala lingine kabisa.
 
We Kikwete na JPM unawachukuliaje?
Kikwete kasoma Uchumi kahitimu UDSM, akulizwa na Bob Gledof, kwa nini nchi yako ni masikini?
Huyu rais, ana state organs zote za kumpa blue books zote.
Kajibu hajui kwa nini nchi yake masikini.
Magufuli ndiyo kabisaaa.

Mtu kateua mawaziri, kawapa kazi nyeti, halafu anatuambia mawaziri wake wapumbavu.

Hao ni kati ya wahitimu wanaoheshimika kabisa wa UDSM.
 
Uwikariri mpendwa, ukitaka kilimo huwezi kusoma udsm z
Accounts huwezi kusoma udsm sasa chuo gani kinatoa course nyingi kinaacha kozi muhimu ya fedha. Siku hizi Nasikia B.com wameboresha walau unaweza kukuta course inayofanana na uhasibu.
Mada inasemaje Mkuu?

Soma kichwa cha habari hapo alafu usome ulichopost.

Nimesema wale wenye chuki na Udsm kisa tuu hawajachaguliwa sababu ya ufaulu wao mdogo. Sijasema kuwa lazima mtu asome Udsm.
 
Acheni kukikweza, UDSM si chuo cha kujisifia kiiovo ni sawa tu sawa na vyengine, tena hizi sifa zake Hazina tofauti na chama tawala ni mjina mkubwa tu hakunaga chochote zaidi ya kukopiana tuu

Pole sana
 
Mtu yeyote aliyehitimu Shule ya Sekondari tu, aliyesoma mchepuko wowote, inabidi ajue kuandika insha.

Hizi habari za kwamba umesoma Engineering eti ndiyo hutakiwi kujua kuandika insha ndiyo ujinga ninaousema mnahitimu lakini hamjamaliza ujinga wa msingi kabisa.
Insha zinatofautiana sana Mkuu.
Kidato cha pili kama sikosei kuna Insha za Wasifu na zile za hoja.

Uandishi wa Insha unategemea mambo mengi. Moja wapo ni Ujuzi na uelewa na mwandishi. Mtu aliyesomea Uhandisi atakuwa na ujuzi wa kawaida wa kuandika insha tofauti na mtu wa fasihi na mwandishi wa habari.

Wewe mwenyewe unaweza jiona unajua kuandika insha lakini ukawa hujui
 
Divisheni one zipo lakini ni chache sana.

Mtu aliepata one huchagua vyuo vingine ikiwa Udsm hakuna Kozi anayoitaka kusomea.

Pia bandiko langu limebeba ujumbe wa kuwa kama umefeli usihangaike kulaumu kwa nini hukuchaguliwa Udsm.

Mbona hata Rais wako hilo analijua na kuliheshimu
Ushamba tu hakuna lolote wengi wa mikoani wanataman kuja kuosha macho dar watu wana div 1 pt 3 wamesoma vyuo vingine na wapo vzr tu
 
Insha zinatofautiana sana Mkuu.
Kidato cha pili kama sikosei kuna Insha za Wasifu na zile za hoja.

Uandishi wa Insha unategemea mambo mengi. Moja wapo ni Ujuzi na uelewa na mwandishi. Mtu aliyesomea Uhandisi atakuwa na ujuzi wa kawaida wa kuandika insha tofauti na mtu wa fasihi na mwandishi wa habari.

Wewe mwenyewe unaweza jiona unajua kuandika insha lakini ukawa hujui
Kwani wapi nimesema hawawezi kuandika insha ya muandishi wa habari?
 
Kikwete ni mtu bogus kabisa, kasoma Uchumi kahitimu UDSM, akulizwa na Bob Gledof, kwa nini nchi yako ni masikini?

Huyu rais, ana state organs zote za kumpa blue books zote.

Kajibu hajui kwa nini nchi yake masikini.

Magufuli ndiyo kabisaaa.

Mtu kateua mawaziri, kawapa kazi nyeti, halafu anatuambia mawaziri wake wapumbavu.

Maana yake yeye aliyewateua na kuwapa kazi nyeti za uwaziri ni mpumbavu zaidi yao.

Hao ni kati ya wahitimu wanaoheshimika kabisa wa UDSM.
Unajua nini maana ya Siasa Mkuu?

Watu uliowataja hamulingani kwa lolote labda tu kwa kuvuta pumzi na kwenda chooni.

Kikwete na JPM si kama unavyowachukulia. Ni watu Smart kuliko unavyoona. Ni kwa vile unaleta hisia katika suala la siasa.

Siasa ni mchezo wa kupanga matukio ili yalete maana kwa wananchi.
 
Ushamba tu hakuna lolote wengi wa mikoani wanataman kuja kuosha macho dar watu wana div 1 pt 3 wamesoma vyuo vingine na wapo vzr tu
Kuosha macho ni sehemu ya kuongeza maarifa. Kitu kama ni kizuri hufuatwa hata kama kipo kuzimu Mkuu.

Endelea kusema ni ushamba wenzako wanafuata kilicho bora
 
Back
Top Bottom