Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Sio chama tu shekhe, ni serikali nzima, angalia wakuu wa mikoa mwantum mahiZa katolewa wamemuweka paul christian makonda, na dr dau katolewa kawekwa wa kwao.. Nenda hata necta kule .. Dah!!
hata kama mnaonewa,hv ni lini mtaamua kuandamana kwa kuwapeleka watoto mashuleni ili wasome waelimike,badala ya kuandamana katika keypads ya simu!mabadiliko huja kwa matendo sio maneno!ebu waigeni wanyambo wa karagwe,wanavyo wafanya wahaya wa bukoba!
 
This is too low kwa JF Senior Expert Member kama wewe?...

Of all the people wewe ndiyo mtu wa kuja na post ya namna hii!!!....Smh

Sio poa kabisa Kamanda...

Apate 0 form Six kuna shida gani?, Mbona kuna viongozi wengi tu wa CCM na upinzani hawakufanya vizuri kwenye elimu yet wamefanya vizuri kwenye siasa..Mifano ipo...

Si vizuri kuitumia JF kuwadhalisha watu kwa sababu tu ya milengo ya kisiasa...

JF ni zaidi ya haya uliyoyaandika Mkuu wangu...
Alipata ZIRO? Achana na U-expert wangu
 
Kubenea ana elimu gani?? Mbowe ana elimu gani?? Hiyo elimu kubwa ya viongozi waliopita imesaidia nini Tanzania?? Mimi ni CDM ila kushambulia mtu sababu ya elimu yake ni upuuzi

Umenena mkuu kwa nn umshambulie mtu kwa kigezo cha elimu?

Elimu hizi zimeletwa tu ndo maana hatuna mawazo yakinifu tutabaki kutawaliwa, angalia hata wenye PhD wanavyoharibu Taifa hili leo mtu anakumbatia elimu, ni bure kabisa tutabaki kutawaliwa ngoja Trump akamate madaraka tuisome.
 
Kuna taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ikiwemo hapa jamiiforums, ikieleza kuwa Ndugu Christopher Ole Sendeka ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) aemteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, taarifa hiyo ina makosa na imepotoshwa.

USAHIHI ni kuwa Ndugu Christopher Ole Sendeka, amepewa jukumu la kuwa "MSEMAJI" wa Chama Cha Mapinduzi akiwa ni msaidizi wa Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Mhe Nape Moses Nnauye.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.

Historia ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya Tano inaendesha shughuli zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo kila mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.


Utekelezaji wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirishakatika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na ukwepaji kodi, mambo ambayo matokeo yake yameshaanza kuonekana.

Matokeo hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na umaskini kwa ustawi wa jamii kwa ujumla.

Aidha CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na serikali yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa umma.

Kumbukumbu zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali kwenye utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria, wamefanyiwa hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.

Hata hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa Rais na serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta na uonevu.

Naomba ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya uchaguzi ya 2015/2020 kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa hiyo kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na ndiyo mahitaji na matakwa ya watanzania walio wengi.

Watanzania walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na uwajibikaji hivyo tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri hatua hizi kuwa ni udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo yao na maneno yao wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo ambalo CCM haikubaliani nalo.

CCM inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania wote kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais Magufuli kwa dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye Tanzania yenye maendeleo ifanikiwe.




Ndugu Christopher Ole Sendeka

MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,


20/03/2016
haya watani zetu,naona kusoma upepo fasta mmempa cheo kingine!kama ilikuwa ni nia yenu,basi fanyeni hima mlete mtu kijana na mwenye elimu kuanzia masters au udokta na pia awe na ujuzi na uzofu!nashukuru mmeusoma upepo na haraka kubadilisha gia angani!
 
Mzee Christopher Ole ana tuhuma mbili ambazo hazijakanushwa. Alipata Pumbu form six na eti ni Bwabwa. Umezisikia hizi tuhuma?
Kamanda kulikoni tena hizi siasa tu unapanic bure Mbowe na Ole ni washikaji nashangaa wewe unawaka bure tulizana kidogo na ili joto kunywa class mbili za maji ya vuguvugu kisha tulia kama dakika 10 munkari utaisha then njoo tujadili CV za hawa vioingozi.
 
Huyu bwana kila siku namuona pale Kariakoo anazugazuga nadhani a nasubiria post za Magufuli au CCM yake
 
Kamanda kulikoni tena hizi siasa tu unapanic bure Mbowe na Ole ni washikaji nashangaa wewe unawaka bure tulizana kidogo na ili joto kunywa class mbili za maji ya vuguvugu kisha tulia kama dakika 10 munkari utaisha then njoo tujadili CV za hawa vioingozi.
Anza na Ole Sendeka kwanza
 
Tunaomba mwenye cv Za Mbowe, Kubenea Na huyo Sendeka aziweke hapa tumalize ubishi!!!
 
Acha kuwa mna andika vitu vya kijinga kijinga hapa!!

Ana Div Four 29. Hana Diploma wala Bachelor yoyote eti Masterz mbili!!!!.
Mzumbe Univ pia ni JIPU wanauza sn marksi na vyeti kwa wanasiasa. Mtu amefanya MBA-UNAFAHAMU TITLE ya Research ya NAPE NNAUYE MZUMBE? Sababu zinazo athiri wapiga kura wakati wa uchaguzi washindwe kujitokeza!!! MBA???? STUPIDITY INDEED!!!
Sasa hapa ww ndio unaonekana stupid kwa kupinga kitu ambacho haukijui na hauna uhakika nacho...

Nape Moses Nnauye :

Amesoma O level Nsumba secondary...

Kisha kajiunga Butimba TTC..

Baadae akasoma Diploma ya Sayansi ya Jamii chuo cha Kivukoni...

Kisha akaenda Chuo cha Diplomasia kwa ajili ya Diploma ya International Relations...

Mwaka 2005 alijiunga na Bangalore University India kwa ajili ya Shahada ya kwanza ya Saikolojia, Lugha na Habari ambayo aliimaliza mwaka 2008

Kisha akajiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kwa ajili ya Shahada ya Uzamili ya Utawala (MPA) ambayo aliimaliza mwaka 2011...Andiki lake lilihusu SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGA KURA (Sababu za kutojitokeza wapiga kura siku ya kupiga kura)...
 
Mkuu kwani ww ni boko haram?
Ha ha ha, umenifurahisha eti kwani ww boko harm, hapana mkuu palipo na ukweli lazima tuseme siku hizi tz mtu anapoteuliwa tu wanaanza kuhoji elimu, itatusaidia nn cha mhimu ni utendaji wake kama unafaa, so sendeka ni mtu mhimu Sana kwa kipindi hiki awe na zero au one anafaa kuongoza Chama
 
Back
Top Bottom