Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Nakumbuka Profesa Sospeter Muhongo alisema matokeo yake ya form six ni disaster

Sijui kama alishare-seat na kujiondoleaNa hayo majanga ya Kitaaluma

Ni kweli hatua ambayo CCM imefikia ni lazima iwe na Msemaji asiyekuwa na upeo mpana wa kuchanganua mambo maana itabidi afanye kazi ya kutetea visivyotetewa.

Lazima itafute Mweledi wa kujitoa ufahamu bila soni.
Naona unamnanga Mwenyekiti wako Mbowe.
 
Kabla haujahoji matokeo ya Ole Sendeka,anza kwanza na matokeo ya Mwenyekiti wako Mbowe hapo upo?hahahahaha Nyani haoni kundule ni kama unamwambia Mbowe vile

Kwa siasa za Tanzania bila elimu siasa inakwenda maana wakati mwingine bora hata hao kina Mbowe na Sendeka kuliko hata hao wanaojifanya wasomi alafu wanapitisha vitu ambavyo moyoni hawapendi lakini wanapitisha tu wasionekane wasaliti, kwa mtaji wakati mwingine bora wanasiasa hawa ambao tunaona walichemka shule kwani wamethubutu bila kujali wana majanga kwenye taaluma
 
Ha ha ha ha ha!! Vijana wa Ufipa badala ya kutoa boriti kwenye macho yao kwanza ili waweze kuona... wao wanakimbilia kuwasimanga Majirani
 
uteuzi sahihi kwa chama. Elimu sio kigezo pekee cha kufanya kazi.
 
Kamanda naona unamsema Mwenyekiti wetu Mbowe kijanja angalia usije kufukuzwa Chadema.
Mkuu hapa angejadiliwa Ole Sendeka ingependeza zaidi, Haya ya Mbowe yangeanzishiwa mada yake binafsi.

Ila mngetujuza huyu msemaji mkuu wa CCM alifikia wapi kitaaluma mgetusaidia sana kumfahamu kiundani!
 
Kuweka records sawa..Nape ana Shahada mbili..Ya kwanza aliipata Bangalore university India na ya Pili ya Uzamili aliipata Mzumbe University...

Mbowe elimu yake ikoje?, mbona pamoja na elimu duni aliyonayo ni kiongozi mzuri wa upinzani kuwahi kutokea Tanzania??....

Kubenea...Lema..Sugu n.k mbona elimu zao ni za sekondari na bado ni viongozi wazuri na wawakilishi wazuri wa wananchi waliowachagua?...
Acha kuwa mna andika vitu vya kijinga kijinga hapa!!

Ana Div Four 29. Hana Diploma wala Bachelor yoyote eti Masterz mbili!

Mzumbe Univ pia ni JIPU wanauza sn marksi na vyeti kwa wanasiasa. Mtu amefanya MBA-UNAFAHAMU TITLE ya Research ya NAPE NNAUYE MZUMBE? Sababu zinazo athiri wapiga kura wakati wa uchaguzi washindwe kujitokeza!!! MBA???? STUPIDITY INDEED!!!
 
Kuweka records sawa..Nape ana Shahada mbili..Ya kwanza aliipata Bangalore university India na ya Pili ya Uzamili aliipata Mzumbe University...

Mbowe elimu yake ikoje?, mbona pamoja na elimu duni aliyonayo ni kiongozi mzuri wa upinzani kuwahi kutokea Tanzania??....

Kubenea...Lema..Sugu n.k mbona elimu zao ni za sekondari na bado ni viongozi wazuri na wawakilishi wazuri wa wananchi waliowachagua?...
Yaani mkuu huu upuuzi wa kuulizana elimu ni ujinga uliokithiri... Kama huyo Ben Saanane na elimu yake mpaka sasa imemsaidia nini?? Ubunge kura alipata 27 tu, kazi yake kupiga kelele huku mitandaoni tu
 
kinana wa kaskazini kachagua mkaskazin mwenzie, jamani!
 
Hatimaye ole sendeka kakumbukwa bado babu wasira ,Prof.kapuya,Mzee wa standard and speed,Mustafa mkulo hayaaa endeleeni kutaja wengine
 
Mzee Christopher Ole ana tuhuma mbili ambazo hazijakanushwa. Alipata Pumbu form six na eti ni Bwabwa. Umezisikia hizi tuhuma?
This is too low kwa JF Senior Expert Member kama wewe?...

Of all the people wewe ndiyo mtu wa kuja na post ya namna hii!!!....Smh

Sio poa kabisa Kamanda...

Apate 0 form Six kuna shida gani?, Mbona kuna viongozi wengi tu wa CCM na upinzani hawakufanya vizuri kwenye elimu yet wamefanya vizuri kwenye siasa..Mifano ipo...

Si vizuri kuitumia JF kuwadhalisha watu kwa sababu tu ya milengo ya kisiasa...

JF ni zaidi ya haya uliyoyaandika Mkuu wangu...
 
Kuna taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ikiwemo hapa jamiiforums, ikieleza kuwa Ndugu Christopher Ole Sendeka ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) aemteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, taarifa hiyo ina makosa na imepotoshwa.

USAHIHI ni kuwa Ndugu Christopher Ole Sendeka, amepewa jukumu la kuwa "MSEMAJI" wa Chama Cha Mapinduzi akiwa ni msaidizi wa Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Mhe Nape Moses Nnauye.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.

Historia ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya Tano inaendesha shughuli zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo kila mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.


Utekelezaji wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirishakatika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na ukwepaji kodi, mambo ambayo matokeo yake yameshaanza kuonekana.

Matokeo hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na umaskini kwa ustawi wa jamii kwa ujumla.

Aidha CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na serikali yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa umma.

Kumbukumbu zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali kwenye utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria, wamefanyiwa hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.

Hata hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa Rais na serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta na uonevu.

Naomba ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya uchaguzi ya 2015/2020 kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa hiyo kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na ndiyo mahitaji na matakwa ya watanzania walio wengi.

Watanzania walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na uwajibikaji hivyo tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri hatua hizi kuwa ni udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo yao na maneno yao wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo ambalo CCM haikubaliani nalo.

CCM inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania wote kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais Magufuli kwa dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye Tanzania yenye maendeleo ifanikiwe.




Ndugu Christopher Ole Sendeka

MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,


20/03/2016
 
Kupitia radio Uhuru FM wametangaza kuwa Bw. Kinana amemtangaza Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.

* Nafasi hii ni tofauti na ile ya Nape. Nape anaendelea kuwa Katibu Mwenezi wa chama

Taarifa zaidi zitatolewa baadae.
kumbe ni msemaji mkuu,basi fine,hyo hata kujua kusoma na kuandika inatosha!
 
Back
Top Bottom