Christine Shusho ulipofikia ni pabaya......

sijaona mauno hapo aisee. kusema ni kama twanga pepeta ni uongo. sasa nyie mkienda praise and worship mnaimba mmekaa? mweh! acha kila mtu amuabudu muumba wake sawa na alivyotendewa. mie saa ya kusifu mungu najiskiaga kupaa maana amenitendea maajabu hayasimuliki!:A S-fire1::A S-fire1:
 
Usiandikie mate na wino upo, tuwekee tuone.

Hehehehee bwana wewe, hujawahi kumwona?

Mie nilimwona live jumapili iliyopita akitumbuiza kwenye tamasha la pasaka!! alikuwa anajitikisa kwa sana tuuu, na mauno juu!!

Uwe unaenda mkuu.....ungeshuhudia hata Membe alivyozomewa lkn watu bila aibu wanakanusha!
 
na wewe sasa jamaa yalikuwa maoni yake yametoka wapi hayo yakutumiwa na muovu,
ndo ninyi mkiona nyoka mnasema mnalogwa, sijaona ubaya wa video hii but wewe ndo umenikwaza na maneno yako!

1.Inawezekana kweli nimekukwaza.....ila ni vema ukaelewa kuwa jamaa nae alinikwaza.....si unajua ukikwazika!?
2.Kesi hii siyo yako mwenye kesi hii katulia tulii kama Batilda balozi wetu Kenya, wewe ukawa kama jaji Rwakibarira kunihukumu mimi kama Lema!! Huna haki hiyo.......!
 
frankly speakin on this issue i only see a sort of personal issues vendetta like character assassination defamation plus a lot of ..i dont know exactly what is about...kimsingi sijaona hatia ya mtu huyu kutuhumiwa na kufuatiliwa kuanzia nguo kuwa na pictures za mafuvu na mengineyo.... JUDGE NOT AS U WILL BE JUDGED FIRST.
 
Ninachokiona hapo ni kupoteza mwelekeo wa uchaji wa Mungu: Kitakachofuata ni kuomba kurabo na marapa wa Bongo fleva; Sihukumu ila naqpenda sana huduma ya dada huyu ninachoogopa ni jinsi safari yake inavyoanza kutia mashaka. Alianza vizuri. naomba amalize huduma yake vizuri !
 
Mkiona kwaya ya Nakonde Zambia wanakata mauno kama akina Aisha madinda sijui mtasemaje?

MATARAJIO YA WENGI NI KWAMBA WASANII WA NYIMBO ZA INJILI WANAMAANISHA AU KUYAISHI YALE WANAYOYAIMBA,(WAMEOKOKA ) KUMBE ALAS! WAO NI SANAA NA WALA KWA YESU HAWAPO, WANATAFUTA MAISHA TU SABABU NDIO SOKO LINAHITAJI BIDHAA HIZO,NI WAFANYA BIASHARA TU WALA SI WAHUBIRI WA INJILI,WANATUMIKISHWA NA UPANDE MWINGINE KABISA, NDIO MAAMA YA "sio kila aitaye Bwana Bwana anajulikana na Mungu au na Yesu" ndio maana siku ya hukumu imeweka wazi kabisa "wataambiwa ondokeni sikuwajua na wala siwajui ninyi" SASA WEWE UKIONA HAO NAKONDE WAKIKATA MAUNO WEWE UNAFANYA NI KIGEZO??????????????! YESU ALIAACHA KIELELEZO KWA KILA JAMBO TATIZO HAMTAKI KUJIFUNZA KUTAMBUA maroho ya uongo,nyenzo zao, janja ( tricks ) zao. HIVYO UNASOMBWA TU NA KILA UPEPO UKIDHANI HAO NI WATUMISHI WA BWANA. na ukiambiwa unasema usihukumu.WANAMCHEZEA BWANA.
 
HUo ndio uinjilisti ndugu yangu Father Chrismas. Unajuaje kati ya hao aliokuwa anashiriki nao katika huo uimbaji hataguswa mmoja akaokaoka hata siku zijazo? Je angekaa na kuimba kanisani tu huyo angepatikanaje? Unajua kazi yetu tunapanda mbegu akuzaye ni Bwana. Tusimhukumu bali tumpongeze kwa ujasiri hata wa kufanya huduma katika mazingira hayo. Kuhusu mavazi sijaona na sijawahi kumwona huyu dada akiwa amevaa mavazi ambayo si ya heshima kama baadhi ya wengine. Tumtie moyo na kama tukiona kuna kitu chenye shida tumtafute yeye mwenyewe tumwambie lakini kwa kumweka huku harumsaidii.
 
Ha ha haaa mnataka achezeshe meno tu na si sehemu nyingine kama dhehebu fulani...
 
wakubwa naheshimu kuwa ninyi mnaona kinachofanyika katika video ni sahihi.............Haya ni mambo ya kiimani......mfano sabato hawaruhusu uchezaji wa kujitikisa kwa aina yeyote ile.........mim binafsi wimbo huu naupenda sana lakini hii clip sijaipenda........ni vyema wanaomtumikia Mungu wakawa humble na kujitofautisha na twana pepeta na Fm academia.........kinachofanyika katika hii video hakijanifanya nihisi uwepo wa roho mtakatifu katika eneo hilo..........mim sikubaliani na mauno na kutoonyesha unyenyekevu wakati wa kuimba nyimbo zinazomhusu Mungu.....kama kwaya ya zambia na Rebeca malope wanakata mauno hiyo hainifanyi nione vitendo hivyo ni sawa..........siku wakitangaza kuwa kwenye hizo kwaya kuna mashoga na wasagaji na wao wanaona sawa mtataka na sisi pia tuone ni sawa...........mim sio mlokole wala na ni miongoni wanaompenda Shusho lakini ninamuogopa Mungu,najua anastahili kuheshimiwa na kamwe sio kuimbiwa na watu wanaobehave kama kundi la wavuta bangi wasio onyesha chembe ya kumuheshimu............huu ni mtizamo wangu..................na pia nina heshimu mitazamo yenu wakuu mnaoona siko sahihi kuona anachofanya sio sahihi........................!
Mkuu mbona haya mambo ni ya kawaida sana siku hizi!
 
Mwisho wa Siku Mungu ndiye atakayekuja kusema What you did was right or wrong.
 
mmmh huu ni utata.

hiyo siyo video ya christina Shusho ni Gospel live band inapiga kila ijumaa jioni pale hoter atriums sinza, Kwa hiyo kama kuna mwanamziki wa injili amehudhuria shoo wanamwalika aimbe wimbo mmoja, inapiga nyimbo za muziki wa injili za kisasa na za zamani na pia wanacopy za kizazi kipya,
 
Yeah Preta...ni Wimbo wa Beenie Man - song linakwenda kwa jina la GOSPEL TIME...Kwema lakini!
kuna nyimbo nimewahi kusikia ya kumsifu Mungu inasema......can you shake that bu** Jesus gave you....
sasa hapa sijui tunasemaje......hii kidogo hata mimi ilinistua.....

 
Back
Top Bottom