Chongolo: Tunapigana vita vya kiuchumi, wana pa kukimbilia

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Tunapigana vita vya kiuchumi…wana pakukimbilia: Chongolo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo amesema Tanzania ikiwa sehemu ya dunia, iko katika mapambano ya vita vya kiuchumi asubuhi, mchana na jioni, akiwataka Watanzania kuwa makini na watu wachache, katikati ya mapambano hayo, wenye dhamira ovu kwa nchi yetu, wanaotaka kutumia mjadala wa uwekezaji bandarini kuvuruga amani iliyopo, kwa sababu wanapo mahali pa kukimbilia nje ya nchi, kama baadhi yao walivyofanya miaka michache iliyopita.

Ndugu Chongolo amesema kuwa ingawa uhuru wa nchi ulipatikana baada ya kuwaondoa wakoloni, mapambano ya kujikomboa kiuchumi yako katika changamoto ya vita vya kiuchumi ambavyo havionekani kwa macho waziwazi, lakini vinahitaji akili, busara na mikakati zaidi kuvipigana na kwamba nchi inatakiwa kuwa imara ili isiyumbiwe wala kutolewa kwenye mstari sahihi na wapinzani au maadui wasioitakia mema.

Katibu Mkuu Chongolo amesema hayo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo Jumatano, Julai 19, 2023, katika Uwanja wa Shule ya Mazoezi, mjini Korogwe, mkoani Tanga, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake, kufafanua na kuwaelimisha wananchi masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, ikiwemo suala la makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai yanayolenga kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uboreshaji wa uendeshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam.

“Niwaambie miaka ya 50 kwenda ya 60 tulipigania uhuru wa nchi yetu. Uhuru ulipatikana na sasa Tanzania iko huru. Lakini vita haijaisha. Vita inaendelea. Sasa hivi hatupiganii uhuru tena. Kwa sababu upo. Vita ya sasa ni vita ya uchumi. Na hii ni vita ya dunia. Na sisi Tanzania ni sehemu yake. Na sisi tunapigana vita hiyo, asubuhi mchana na jioni. Ndugu zangu wana-Tanga, vita ya uchumi ni vita ya kutumia akili, busara na ya kimkakati zaidi.”

“Huwezi kuiona kwa macho, hauwezi kuishika kwa mkono. Lakini ni vita tena ni vita kubwa, kuliko ile ukombozi wa wakati huo. Ni vita ambayo ukikaa kienyeji umeenda na maji. CCM hoyee…CCM hoyee…Vita hii ukikaa kienyeji umeenda na maji. Kwanini nasema ukikaa kienyeji umeenda na maji? Kwa sababu fursa tunazopigania wote, kuzipata na kuzitumia ili kujiendeleza ni fursa za aina moja na zinapatikana kwenye maeneo yale yale. Kwa hiyo kila mmoja anaiangalia fursa kwa jina lake, kwa jicho lake, kwa namna yake na kwa mazingira,” amesema Ndugu Chongolo.

Ndugu Chongolo ambaye katika mkutano huo aliongozana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Steven Wassira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Ndugu Atupele Mwakibete (Mb) na Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM), Ndugu Jerry Silaa wakitoa ufafanuzi wa kina kuhusu ukweli na uhalisia wa mkataba wa uboreshaji utendaji wa bandari na manufaa yake,

Amesisitiza kuhusu umuhimu wa Watanzania kuilinda amani, amesema kuwa hiyo ni mojawapo ya tunu ambazo waasisi wa Tanzania walihakikisha inakuwa ni utambulisho wa taifa na inatakiwa kulindwa na kutetewa kwa nguvu zote bila kuwaonea aibu wala kuwaogopa wote wanaotishia kuivuruga kwa maslahi ya kisiasa.

“Mwalimu (Nyerere, Baba wa Taifa) alisema ukiulizwa Tanzania una nini, sema una amani huku ukijidai. Amani hii si amani rahisi, si amani ya lelemama, kuna watu wametoka jasho na wanatoa jasho ili hii amani iwepo. Tusiache amani hii ipotee kwa sababu ya wajanja wachache wenye dhamira ovu kwa nchi yetu, wenzetu wana mahali pa kukimbilia.”

“Na ushahidi tumeuona miaka michache iliyopita. Walivyoona huku mambo yao yamekaa vibaya walitafuta pa kuishi. Sisi tuna wapi pa kukimbilia nje ya Tanzania? Kama hatuna tujue tuna wajibu wa kuilinda amani ya nchi hii, tuna wajibu wa kuiendeleza nchi hii. Na tuna wajibu wa kusimamia maslahi ya nchi hii bila aibu wala kumuogopa yeyote,” amesema Ndugu Chongolo akisisitiza pia kuwa CCM itahakikisha maoni ya wananchi yenye tija na chanya, yanafanyiwa kazi na Serikali katika hatua za kuingia mkataba wa utekelezaji.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo amesema Tanzania ikiwa sehemu ya dunia, iko katika mapambano ya vita vya kiuchumi asubuhi, mchana na jioni, akiwataka Watanzania kuwa makini na watu wachache, katikati ya mapambano hayo, wenye dhamira ovu kwa nchi yetu, wanaotaka kutumia mjadala wa uwekezaji
Chongolo aliokota embe chini ya Mbuyu ale kimya kimya Hana hadhi ya kuzodoa wanaoipenda nchi yao.
 
Kwanza, hiyo vita ya kiuchumi wanayopigana CCM watueleze wanapigana na nani au nchi ipi? Kwa miaka 60 na zaidi, CCM wameshikilia usimamizi wa rasilimali za nchi huku ikionekana kuwa na ufanisi usioridhisha.

Pili, watujibu, vita za kiuchumi hupiganwa kwa kuuza na kugawa bure rasilimali za taifa? Ni muda sasa tumeshuhudia uporaji na ugawaji wa rasilimali zote za kimkakati kama madini, gesi, vivutio vya utalii, wanyamapori, vitegauchumi na majengo yaliyokuwa chini ya serikali, mabenk, nk, . Wakati uporaji ukihamia kwenye bahari na maziwa yote, hawa CCM wanajidai wapo vitani.

Tatu, mkataba huu wa DP World tumebahatika kuusoma na kuridhika kuwa ni utapeli mtupu. Hii ndiyo vita ya uchumi anayopigana? Ni vita dhidi ya nani kama siyo dhidi ya Tanzania na rasilimali zake?

Watanzania tuamke tukamate silaha tupiganie rasilimali zetu. Kila mwenye silaha ya aina yoyote na akaiandae tusije tukajuta. Majuto mjukuu.
 
Unapigana vita vya kiuchumi huku maeneo nyeti na ya kimkakati unayafanyia mzaha! Unaingia mikataba ya hovyo na ya kitapeli kisha unategemea maajabu yatendeke katika kukuza uchumi wako!?
 
Chongolo nadhani siyo mzima. Hajielewi na haelewi hata anachoongea.

Uhuru ambao wazee wetu waliupigania kwa gharama kubwa, yeye na wenzake wanauuza kwa waarabu halafu anakuja kubwabwaja ujinga wa ajabu.

Hawa watu nadhani rushwa waliyoila imewaondolea hata akili ya kawaida.
 
Tunapigana vita vya kiuchumi…wana pakukimbilia: Chongolo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo amesema Tanzania ikiwa sehemu ya dunia, iko katika mapambano ya vita vya kiuchumi asubuhi, mchana na jioni, akiwataka Watanzania kuwa makini na watu wachache, katikati ya mapambano hayo, wenye dhamira ovu kwa nchi yetu, wanaotaka kutumia mjadala wa uwekezaji bandarini kuvuruga amani iliyopo, kwa sababu wanapo mahali pa kukimbilia nje ya nchi, kama baadhi yao walivyofanya miaka michache iliyopita.

Ndugu Chongolo amesema kuwa ingawa uhuru wa nchi ulipatikana baada ya kuwaondoa wakoloni, mapambano ya kujikomboa kiuchumi yako katika changamoto ya vita vya kiuchumi ambavyo havionekani kwa macho waziwazi, lakini vinahitaji akili, busara na mikakati zaidi kuvipigana na kwamba nchi inatakiwa kuwa imara ili isiyumbiwe wala kutolewa kwenye mstari sahihi na wapinzani au maadui wasioitakia mema.

Katibu Mkuu Chongolo amesema hayo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo Jumatano, Julai 19, 2023, katika Uwanja wa Shule ya Mazoezi, mjini Korogwe, mkoani Tanga, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake, kufafanua na kuwaelimisha wananchi masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, ikiwemo suala la makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai yanayolenga kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uboreshaji wa uendeshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam.

“Niwaambie miaka ya 50 kwenda ya 60 tulipigania uhuru wa nchi yetu. Uhuru ulipatikana na sasa Tanzania iko huru. Lakini vita haijaisha. Vita inaendelea. Sasa hivi hatupiganii uhuru tena. Kwa sababu upo. Vita ya sasa ni vita ya uchumi. Na hii ni vita ya dunia. Na sisi Tanzania ni sehemu yake. Na sisi tunapigana vita hiyo, asubuhi mchana na jioni. Ndugu zangu wana-Tanga, vita ya uchumi ni vita ya kutumia akili, busara na ya kimkakati zaidi.”

“Huwezi kuiona kwa macho, hauwezi kuishika kwa mkono. Lakini ni vita tena ni vita kubwa, kuliko ile ukombozi wa wakati huo. Ni vita ambayo ukikaa kienyeji umeenda na maji. CCM hoyee…CCM hoyee…Vita hii ukikaa kienyeji umeenda na maji. Kwanini nasema ukikaa kienyeji umeenda na maji? Kwa sababu fursa tunazopigania wote, kuzipata na kuzitumia ili kujiendeleza ni fursa za aina moja na zinapatikana kwenye maeneo yale yale. Kwa hiyo kila mmoja anaiangalia fursa kwa jina lake, kwa jicho lake, kwa namna yake na kwa mazingira,” amesema Ndugu Chongolo.

Ndugu Chongolo ambaye katika mkutano huo aliongozana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Steven Wassira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Ndugu Atupele Mwakibete (Mb) na Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM), Ndugu Jerry Silaa wakitoa ufafanuzi wa kina kuhusu ukweli na uhalisia wa mkataba wa uboreshaji utendaji wa bandari na manufaa yake,

Amesisitiza kuhusu umuhimu wa Watanzania kuilinda amani, amesema kuwa hiyo ni mojawapo ya tunu ambazo waasisi wa Tanzania walihakikisha inakuwa ni utambulisho wa taifa na inatakiwa kulindwa na kutetewa kwa nguvu zote bila kuwaonea aibu wala kuwaogopa wote wanaotishia kuivuruga kwa maslahi ya kisiasa.

“Mwalimu (Nyerere, Baba wa Taifa) alisema ukiulizwa Tanzania una nini, sema una amani huku ukijidai. Amani hii si amani rahisi, si amani ya lelemama, kuna watu wametoka jasho na wanatoa jasho ili hii amani iwepo. Tusiache amani hii ipotee kwa sababu ya wajanja wachache wenye dhamira ovu kwa nchi yetu, wenzetu wana mahali pa kukimbilia.”

“Na ushahidi tumeuona miaka michache iliyopita. Walivyoona huku mambo yao yamekaa vibaya walitafuta pa kuishi. Sisi tuna wapi pa kukimbilia nje ya Tanzania? Kama hatuna tujue tuna wajibu wa kuilinda amani ya nchi hii, tuna wajibu wa kuiendeleza nchi hii. Na tuna wajibu wa kusimamia maslahi ya nchi hii bila aibu wala kumuogopa yeyote,” amesema Ndugu Chongolo akisisitiza pia kuwa CCM itahakikisha maoni ya wananchi yenye tija na chanya, yanafanyiwa kazi na Serikali katika hatua za kuingia mkataba wa utekelezaji.

View attachment 2693599
Wapewe kichapo Ili warudi Kwa bwana zao wa Ulaya Waliowatuma
 
  • Hahaha! Unapigana vita kwa kutetea 'uuzwaji' wa uhai.
  • Watu wa propaganda walivyo, yawezekana hata huo mkataba hajausoma. Kuna jamaa alisafirishwa kuhudhuria mkutano wao huko Mbeya, amerudi anabwabwaja aliyokaririshwa. Nilipomsomea vifungu vya mkataba, naye akawa mpole
 
Mapungufu yaliyoanishwa kweny mkataba wa DP world yafanyiwe kaz!! Haya mengine ni ngonjera kama ngonjera nyingine!!
 
Chongolo ,umepita kwenye mstari sahihi.
Kwa ukweli mimi si CCM mwenzako ,tena ni mpinzani kweli na naiombea CCM ianguke leo ili niingie madarakani mimi na chama changu , lakini kwa hili hata mimi naunga mkono hoja.

Kenya wanainyemelea Tanzania ianguke kwenye Mkataba huu ili ivune manufaa.

Msumbiji wanaomba dua ya Kuku dhidi ya TZ.

South Afrika inatamani Tanzania Ibaki hivi ilivyo il waendele kutupiga mabao.

Akin Tundu na Maria Sarungi na wengine wanao wafuata, huenda ikawa wanatumiwa, au wanamaslahi binafsi kwenye hali ya sasa au Hawana uelewa wa kutosha juu ya HII VITA VYA KIUCHUMI vya kimataifa.
SOMA HAPA

BANDARI YA DARESALAM IMEMUINGIZA RAIS SAMIA KWENYE VITA VYA KIUCHUMI.

Na Thadei Ole Mushi.

Chukua kalamu na karatasi kwenye andiko hili unaweza kuandika chochote…. Ipo hivi….

Bandari ya Daresalam inahusika kwa asilimia 95% kwenye biashara za Kimataifa Tanzania. Ni eneo Muhimu mno na fursa kubwa sana kwa nchi yetu. Ukiigusa Bandari yetu kwa jema au baya basi umegusa asilimia 95 za biashara kati ya Tanzania na maeneo Mengine.

Kupitia rank za World Bank’s Conteiner Port Performance index (CPPI) inaonyesha mwaka 2022 Bandari ya Daresalam ilishika nafasi ya 361 kati ya Bandari 386 kwenye utoaji wa huduma za kibandari Duniani. Mwaka wa 2023 tukashika nafasi ya 312 kati ya bandari 348. Tafsiri yake ni kwamba bado Bandari yetu haifanyi vizuri hata kidogo pamoja na kwamba inatajwa kuwa ipo eneo zuri kuliko bandari Nyingi Duniani.

Kwa mfano mwaka 2021 World bank walitoa ripoti ya CPPI (Global ranking of container Ports) ambapo Bandari ya Daresalam ilishika nafasi ya 361 kwa ubora kati ya bandari 379 zilizoorodheshwa, yaani tulikuwa ni wa 9 kutoka Chini. Kwenye kipengele cha administrative approach bandari yetu ilikuwa na points negative -248 na katika kipengele cha Statistical approach tulikuwa na points negative -105. Tafsiri ya hizi negative ni kwamba Bandari yetu uongozi ni Mbovu, kupita kiasi na utendaji wake kwa ujumla ni mbovu kupita kiasi hivyo Bandari yetu inafanya kazi Chini ya kiwango na katika udhaifu mkubwa. Nakuwekea link kabisa uweze kupitia ripoti hiyo ya worl Bank:- https://thedocs.worldbank.org/en/do...nal/Container-Port-Performance-Index-2021.pdf

Kutokana na Kufanya huko vibaya nchi ambazo tulikuwa tukizihudumia zimeshaanza kutuhama hivyo kunahitajika juhudi za makusudi na za haraka kabisa kuponyesha bandari yetu kutokana na umuhimu wake kwenye uchumi wetu.

Wataalamu wanasema kutokana na hali ya Utulivu ya Tanzania kisiasa,na kijamii Bandari ya Daresalam imeendelea kuwa Chaguo la kwanza kwa nchi zote ambazo hazina bandari na tumepakana nazo. Bandari ya Daresalam imeendelea kuwa chaguo la Kwanza kwa nchi za Zambia, DRC, Malawi, Burundi, Rwanda na Uganda. Kwa sasa nchi hizi zimeanza kufikiria kuchukua Risk za kibiashara kupitisha mizigo yao kwenye Bandari za Mombasa, na Durban Africa Kusini kutokana na Huduma mbovu kwenye Bandari yetu. Tukicheza washindani wetu wataua kabisa Uchumi wetu hivyo hili jambo lazima tulijadili tukiwa tumetanguliza Uzalendo mbele bila kuwa na interest zozote zile.

Kwenye Bandari kumi bora Dunian taifa la China linaingiza Bandari zake saba kwenye top ten. Lakini ukifuatilia kwa nini China wanafanya Vizuri sana kwenye mambo ya Bandari utagundua kwamba katika Bandari zake tano ambazo zipo kwenye top ten ya Dunia anayeziongoza ni Mwekezaji toka nje. Sio kwamba China imeshindwa kuongoza ila kampa mwenye uzoefu zaidi hizi rasilimali za Dunia huwezi kuzifaidi zote kwa kuzikalia mwenyewe…. Wewe una dhahabu lakini huna Technolojia lazima ukubali kubadilishana ili nyote mnufaike.

APM terminals kampuni ambalo ni subsidiary ya kampuni Maersk toka Denmark ndio waliowekeza kwenye hizo bandari za China. Zaidi ya asilimia 50 ya uendeshaji wa bandari za China zinaendeshwa na makampuni ya nje (Wawekezaji). Kuna haja ya kutafakari sana wakati tukiendelea na mjadala huu wa Bandari kuwa issue si mkataba tu kukosewa ila ndani yake pia kuna Vita kubwa ya Kiuchumi.

Kwenye hili la Bandari Rais Samia ni Dhahiri ameingia kwenye Viunga vya Uwanja wa Vita ya Kiuchumi hili linaonekana wazi wazi kwa sasa. Tulizoea kumsikia Rais Magufuli akisema vita ya Kiuchumi ni Ngumu hatukuwa tunamwelewa. Ndio maana alivyoanza ujenzi wa Miradi Miwili Mikuwa wa Umeme na SGR ndio kipindi alichopigwa vita kuliko kipindi kingine nje na ndani ya Nchi. Na katika kipindi alichokaa madarakani SSH kama Rais wa Nchi wakati huu wa uwekezaji wa Bandari ndio wakati ambao kelele na kurushiwa mawe kumeongezeka.

Ukiachana na Bandari SGR nayo ilikuwa ni vita…..

Kenya ndio wa kwanza kabisa kujenga mradi wa SGR wakishirikiana na Ethiopia kwa kukopa China. Mkopo huo waliokopa China uliziingiza nchi hizi mbili Kenya na Ethiopia kushika number mbili na number tatu kwa nchi zilizokopa Sana China Kutoka Africa. Yaani tukipanga wanaodaiwa fedha nyingi na China Africa basi kenya na Ethiopia zinashika number mbili na number tatu. Ni Mkopo ambao ni mkubwa Sana na kuulipa si kazi ndogo.

Jarida la African Report liliwahi kunukuu mtafiti mmoja aliyeandika kwenye Gazeti la Kenya (Daily Nation) kuwa:-.

"Kenya’s and Ethiopia’s SGR projects impacted significantly the amount of their debt to China and generally their ratio of debt relative to GDP,” researchers wrote in the Daily Nation in December 2019, “As of 2017, Ethiopia and Kenya ranked the second and third highest Chinese debtors on the continent respectively. Their debt relative to GDP has also risen exponentially compared to Tanzania’s.”

Further complicating matters is the fact that, despite accumulating debt and government focus over the past decade, Kenya and Ethiopia’s SGR’s have not delivered what they promised.

Pamoja na kwamba Wana Mkopo mkubwa Sana lakini hawatarajii kuvuna matunda yoyote yale kwenye mradi huo. Hawatarajii kuvuna Kama walivyopanga hapo awali. Yaani mipango yao imevurugika....

Sababu za kutokupata faida

Kutokana na mradi huo kutumia fedha nyingi Sana za Mkopo na ugumu wa kulipa Mkopo wenyewe Bandari ya Mombasa imekuwa si rafiki tena kupitisha bidhaa kwa nchi za Africa mashariki kutokana na masharti na Kodi walizoweka ili wapate fedha za kulipa Mkopo.

Kutokana na hilo bandari Daresalam Tanzania imeendelea kuwa kivutio kwa nchi za Africa mashariki na Kati. Balaa kubwa zaidi kwa Kenya limekuja kujitokeza kwa Tanzania ilipoanza kujenga SGR yake.

Baada ya Mradi kuanza mataifa ya Burundi, Rwanda, na Congo waliingia mkataba wa Reli hii kufika kwenye nchi zao. Kwa maana hiyo Nchi hizi zitakuwa na access ya Moja kwa Moja kwa njia ya Reli na bandari ya Daresalam. Jiulize bandari ya Mombasa Kenya itabaki inahudumia nchi nchi gani? Bandari yao itamlisha Nani? Kwa hiyo SGR yetu imekuja kuwa ni maziko ya bandari ya Mombasa.

Justification

Baada ya Tanzania kutiliana saini na nchi za Burundi, Rwanda, na Congo kuhusu ujenzi wa SGR Gazeti la nchini Kenya linalojulikana Kama the East Africa liliandika kuwa Kenya imepata pigo kubwa kutokana na makubaliano hayo ya Tanzania na Rwanda, Burundi, na Congo. Fuata Link kusoma walichokiandika.

Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC - The East African - Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC

Habari hii ilichapishwa pia na jarida la The China Project in Africa. Unaweza pia kusoma kupitia link ifuatayo kujionea kinachoendelea.

Vita nyingine ya kiuchumi ilikuwa Stiglers…

Mradi huu Rais Magufuli alipoanza kuugusia kuwa ataujenga utoke kwenye ndoto za Mwalimu Nyerere na kuwa kweli hakuna Taifa ambalo halikupinga. Mataifa ya Ulaya na kwingineko wote waliionya Tanzania wasijaribu. Sababu kubwa wataharibu mazingira....

Mwandishi Kutoka Kenya anayeishi Lusaka Zambia anayeitwa Mike Mwenda aliandika kwenye jarida la Lifegate Mambo ya ajabu kabisa na hata kumtuhumu Rais Magufuli. Kisa ni sisi kutaka kutengeneza Mradi wa Stiglers. Fuata link ifuatayo kumsoma Mike Mwenda na shutuma zake.

Stiglers itatuondoa kabisa kwenye uhaba wa umeme na kutufikisha kwenye Uchumi wa viwanda. Kila Tanzania inapojenga Kiwanda Moja kwa Moja unagusa Uchumi wa jirani ambao hutegemea Sana soko hapa Tanzania kutokana na sisi kuwa hatuna viwanda..

Tujiulize Kama Stiglers inaharibu mazingira je viwanda vya mabeberu haviaharibu mazingira?.....

Mwaka 1992 Marekani ulikataa kusaini mkataba wa Kyoto Protocol ambao ulihusu kupunguza viwanda ambavyo vinachangia mabadiliko ya Hali ya hewa.

Unaambiwa mataifa haya ya Magharibi pekee huchangia joto Duniani kwa asilimia 45 ya joto lote. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa Kama mataifa haya ya kibepari yatakubali kupunguza Viwanda vyao Basi Dunia inaweza ku maintain joto la centigrade 18°C.

Kwa maana hiyo hili la bandari Vipengele vya Mkataba vinatumika tu kama Silaha ya kupigana vita hii…. Tuangalie panapofaa kurekebisha tukamilishe hili dili haraka sana tumechelewa. Tumuunge mkoni Rais katika nia yake njema hii.

Share kwa manufaa ya taifa lako…..

Ole Mushi

0712702602
 
Bichwa lake kubwa ila limejaza matope.!!.

Kwan watanzania Wanapinga Uwekezaji???.

Mbona anaongea kisiasa na Imani ,Imani, Wakili Msomi Mwabukusi keshasema, Suala la Imani ni masuala ambayo Watanzania tumuachie Mungu , Nchi inaongozwa Kwa sheria na Katiba, watanzania wnahitaji Facts sio kubwabwaja ujinga wako .

Kuna Hoja za Msingi zilizoibuliwa na Wazee wetu ,wasomi nguli,. Hoja hizo ndo tunataka zijibiwe kisheria, sio blaa blaaa .

Nani kasema anataka kuvuruga Amani?? Nani kasema watanzania wagawanyike, ?.

Kwamba Akina Shivj, Slaa ,Nshala, Wana mahali pankukimbilia ndio maana wanahoji ?? Kwan wanafanya uhaini??.

Haya majamaa manene manenen ,mavichwa makubwa, Huwa kichwan ni Hewaaa kabisa !.

Mwenye CV yake aiwekee Hapa, Kama hajasoma Kwa kuunga unga ni Bahati !!.
 
Kusema unajivunia amani wakati Mali za nchi zinaporwa na wageni ni ujinga!
Soma kwanza , usikurupuke na Uzwazwa.
Usipokubali kuliwa kidogo na we huta kula.
Musituletee Tanzania ya Nyerere ya kukalia Rasilimali na kufa umasikini.
Dunia ya leo ni kijiji popote unawekeza na popote unafanya biashara.
50% ya bandari za China zinaendeshwa na kampuni za Sweden
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo amesema Tanzania ikiwa sehemu ya dunia, iko katika mapambano ya vita vya kiuchumi asubuhi, mchana na jioni, akiwataka Watanzania kuwa makini na watu wachache, katikati ya mapambano hayo, wenye dhamira ovu kwa nchi yetu, wanaotaka kutumia mjadala wa uwekezaji bandarini kuvuruga amani iliyopo, kwa sababu wanapo mahali pa kukimbilia nje ya nchi, kama baadhi yao walivyofanya miaka michache iliyopita.

Ndugu Chongolo amesema kuwa ingawa uhuru wa nchi ulipatikana baada ya kuwaondoa wakoloni, mapambano ya kujikomboa kiuchumi yako katika changamoto ya vita vya kiuchumi ambavyo havionekani kwa macho waziwazi, lakini vinahitaji akili, busara na mikakati zaidi kuvipigana na kwamba nchi inatakiwa kuwa imara ili isiyumbiwe wala kutolewa kwenye mstari sahihi na wapinzani au maadui wasioitakia mema.

Katibu Mkuu Chongolo amesema hayo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo Jumatano, Julai 19, 2023, katika Uwanja wa Shule ya Mazoezi, mjini Korogwe, mkoani Tanga, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake, kufafanua na kuwaelimisha wananchi masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, ikiwemo suala la makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai yanayolenga kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uboreshaji wa uendeshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam.

“Niwaambie miaka ya 50 kwenda ya 60 tulipigania uhuru wa nchi yetu. Uhuru ulipatikana na sasa Tanzania iko huru. Lakini vita haijaisha. Vita inaendelea. Sasa hivi hatupiganii uhuru tena. Kwa sababu upo. Vita ya sasa ni vita ya uchumi. Na hii ni vita ya dunia. Na sisi Tanzania ni sehemu yake. Na sisi tunapigana vita hiyo, asubuhi mchana na jioni. Ndugu zangu wana-Tanga, vita ya uchumi ni vita ya kutumia akili, busara na ya kimkakati zaidi.”

“Huwezi kuiona kwa macho, hauwezi kuishika kwa mkono. Lakini ni vita tena ni vita kubwa, kuliko ile ukombozi wa wakati huo. Ni vita ambayo ukikaa kienyeji umeenda na maji. CCM hoyee…CCM hoyee…Vita hii ukikaa kienyeji umeenda na maji. Kwanini nasema ukikaa kienyeji umeenda na maji? Kwa sababu fursa tunazopigania wote, kuzipata na kuzitumia ili kujiendeleza ni fursa za aina moja na zinapatikana kwenye maeneo yale yale. Kwa hiyo kila mmoja anaiangalia fursa kwa jina lake, kwa jicho lake, kwa namna yake na kwa mazingira,” amesema Ndugu Chongolo.

Ndugu Chongolo ambaye katika mkutano huo aliongozana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Steven Wassira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Ndugu Atupele Mwakibete (Mb) na Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM), Ndugu Jerry Silaa wakitoa ufafanuzi wa kina kuhusu ukweli na uhalisia wa mkataba wa uboreshaji utendaji wa bandari na manufaa yake,

Amesisitiza kuhusu umuhimu wa Watanzania kuilinda amani, amesema kuwa hiyo ni mojawapo ya tunu ambazo waasisi wa Tanzania walihakikisha inakuwa ni utambulisho wa taifa na inatakiwa kulindwa na kutetewa kwa nguvu zote bila kuwaonea aibu wala kuwaogopa wote wanaotishia kuivuruga kwa maslahi ya kisiasa.

“Mwalimu (Nyerere, Baba wa Taifa) alisema ukiulizwa Tanzania una nini, sema una amani huku ukijidai. Amani hii si amani rahisi, si amani ya lelemama, kuna watu wametoka jasho na wanatoa jasho ili hii amani iwepo. Tusiache amani hii ipotee kwa sababu ya wajanja wachache wenye dhamira ovu kwa nchi yetu, wenzetu wana mahali pa kukimbilia.”

“Na ushahidi tumeuona miaka michache iliyopita. Walivyoona huku mambo yao yamekaa vibaya walitafuta pa kuishi. Sisi tuna wapi pa kukimbilia nje ya Tanzania? Kama hatuna tujue tuna wajibu wa kuilinda amani ya nchi hii, tuna wajibu wa kuiendeleza nchi hii. Na tuna wajibu wa kusimamia maslahi ya nchi hii bila aibu wala kumuogopa yeyote,” amesema Ndugu Chongolo akisisitiza pia kuwa CCM itahakikisha maoni ya wananchi yenye tija na chanya, yanafanyiwa kazi na Serikali katika hatua za kuingia mkataba wa utekelezaji.
Inabidi tuwashughulikie hawa mawakala, wanajionesha wazi wazi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom