Chonde Chonde Serikali tupieni upesi ' Jicho lake Kali ' katika huu ' Usanii ' wa uwekezaji wa GSM, Sevilla na la Liga kwa Klabu ya Yanga

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,858
2,000
Nikiwa kama Mwanachama wa Klabu ya Yanga mwenye Kadi ambayo Namba yake haina ulazima wowote ule kwa Wewe Kuijua naomba niwe wa Kwanza kuiomba Serikali makini inayoongozwa na ' Jemedari ' Rais Dkt. Magufuli kupitia Vyombo vyake ' Nyeti ' kabisa vitupie Macho katika hiki kinachoitwa ni ' Mchakato ' wa Kuipeleka Yanga SC yetu katika Mabadiliko na Mafanikio.

Kwa nilichokiona tu jana pale Serena Hotel nilijua nitaona mambo yenye Kuakisi kabisa yale Mafanikio ambayo ' Muhamasishaji ' wetu Antonio Nugaz alikuwa ' akituhubiria ' kwa Wiki nzima, lakini badala yake nilichokuja Kukiona ni harufu ya ' Usamjo Usamjo ' nikimaanisha ' Uwongo Uwongo / Utapeli Utapeli ' unaotaka kufanywa na huyu ' Tajiri ' wa sasa Gharib Said Mohammed ( GSM )

Tunaambiwa sijui La Liga mara tena Klabu ya Sevilla na hapo hapo tena GSM nao wanahusishwa yaani ni ' Kutuchanganya ' tu Sisi Wanayanga na Wanachama wa Yanga SC ambao ni kwa bahati mbaya mno wengi wetu hata uwezo Wetu tu wa Kupambanua mambo ni mdogo na siyo kama Wanachama wa Simba SC na Mashabiki zao ambao wengi Wao ' wamebarikiwa ' sana Akili ( IQ ) na Mungu.

Hivi Klabu yangu ya Yanga ina ulazima wowote ule wa Kumtafuta ' Consultant ' wa Kuleta Mabadiliko Yanga SC kutokea nchini Hispania ( Spain ) wakati hapa hapa Kwetu nchini Tanzania kuna ' Consultancies Firms ' nyingi tu ambazo zingeweza Kuisaidia Klabu yetu ya Yanga tena kwa Gharama nafuu kabisa na Pesa zingine zingesaida Kulipa Madeni ambayo yanaikabili Klabu yetu?

Na ni kwanini kama Jambo ni la Yanga SC yetu lakini anayeonekana kila mara akiwa ' mbele mbele ' na ' Kiherehere ' ni huyu GSM tu pekee lakini Viongozi Wetu wa Yanga SC ni kama vile ama nao ' Wameshatekwa ' na GSM au hawana tena Sauti kutokana na ' Njaa ' zao na Kutokujiamini Kwao? Nayasema haya kwa Uchungu kabisa kwani GENTAMYCINE sitaki Yanga SC yangu ipotee.

Nilitegemea katika Hafla ya pale Serena Hotel basi nami ningeuona kweli huo ' Uwakilishi ' wa unaoitwa ' Utatu ' wa akina GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla ila niliona tu ' Muwakilishi ' asiye na Uzito wowote ule kutokea huko Hispania ( Spain ) huku Wanachana na Wanayanga ' tukidanganywa ' kama Watoto Wadogo tukiwa na Mwanachama Mwenzetu Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Anachokifanya huyu ' Tajiri ' GSM ni kutaka ' Kutuzuga ' tu Sisi Wanayanga hasa baada ya Kutusoma ' Upopoma ' wetu uliotutukuka kujifanya anatutengenezea Mtandao mkubwa wa Mabadiliko na Mafanaikio Sisi Wanayanga ili atuteke Akili kisha baadae aje kuwa ' Main Bidder ' katika ' Uwekezaji ' na baadae aichukue Yanga SC na aanze ' Kujitajirisha ' nayo Kikubwa sana.

Wanayanga hatujaambiwa huu ' Mchakato ' wa GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla una Manufaa gani kwa Klabu yetu ya Yanga hasa Kiuchumi, Kimfumo, Kibishara, Kimchezo na Kiuwekezaji kabisa badala yake GSM imetafuta tu Waandishi wa Habari kadhaa ili waendelee ' Kutuhadaa ' Sisi Wanayanga na hatimaye ' Waaminike ' na ' Waiteke ' rasmi Yanga SC na tuje Kujuta rasmi.

Rais wangu Ndugu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Waziri husika Dkt. Mwakyembe, Baraza la Michezo Tanzania, TAKUKURU na hata Watu wa TISS tafadhali msikae mbali na hili linalofanywa na hii Klabu yangu ninayoipenda ya Yanga kwani kuna kila harufu ya ' Upigwaji ' hapa na tusisahau pia kuwa kwa sasa Hispania ndiyo Lango Kuu ya Biashara za Dawa za Kulevya na ni ' Wabaguzi ' Wakuu pia duniani.

Kwa hili kama Wanachama Wenzangu wa Yanga SC msiponielewa naihama Yanga SC na nahamia rasmi ama Azam FC au kule Biashara Mara FC.
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,729
2,000
Mkuu GENTAMYCINE ,umeweka angalizo la msingi sana sana kwa kweli. Mimi binafsi sikubaliani na sijui "wataalamu washauri" kutoka Uhispania,labda viongozi wangeweka sababu za msingi za kufanya hivyo.
Pili,huyu jamaa GSM naamini kuna jambo kubwa anataka kulifanya kwa Yanga,but ni kwa manufaa ya klabu,wanachama na Taifa,au ni kwa maslahi yake binafsi,hapo ndipo napata taabu kuelewa. Mliopo huko nyumbani ni vyema mkatusaidia kutafiti ili ukweli uwekwe wazi.
Kongole mkuu.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
50,926

Kwani hapa Simba sc MO Dewji anafanya kwa manufaa ya nani?
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,372
2,000
Huu upuuzi kuna mtu atakuja kunyongwa hadharani msola na kundi lake wasitufanye mazuzu. Mikataba ya kipuuzi ndio inafanya nchi nyingi za kiafrica tuendelee kunyanyasika ni bora kujiendesha kwa mfumo uliopo kuliko kujiingiza kwenye madeni yatakayo dumu miaka 200 ijayo. Wapeni salamu yanga niya wananchi na sio ya gsm utapeli wake na kumleta yule jamaa wa perepereche wa clouds wambie itawatokea puani.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,858
2,000
Mkuu GENTAMYCINE ,umeweka angalizo la msingi sana sana kwa kweli. Mimi binafsi sikubaliani na sijui "wataalamu washauri" kutoka Uhispania,labda viongozi wangeweka sababu za msingi za kufanya hivyo.
Pili,huyu jamaa GSM naamini kuna jambo kubwa anataka kulifanya kwa Yanga,but ni kwa manufaa ya klabu,wanachama na Taifa,au ni kwa maslahi yake binafsi,hapo ndipo napata taabu kuelewa. Mliopo huko nyumbani ni vyema mkatusaidia kutafiti ili ukweli uwekwe wazi.
Kongole mkuu.

GSM anataka au anadhani Sisi Wanayanga wote ni Mangumbaru ( Wajinga ) na Mapopoma ( Wapumbavu ) wakati kumbe wenye Akili tupo wengi.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,858
2,000
Huu upuuzi kuna mtu atakuja kunyongwa hadharani msola na kundi lake wasitufanye mazuzu. Mikataba ya kipuuzi ndio inafanya nchi nyingi za kiafrica tuendelee kunyanyasika ni bora kujiendesha kwa mfumo uliopo kuliko kujiingiza kwenye madeni yatakayo dumu miaka 200 ijayo. Wapeni salamu yanga niya wananchi na sio ya gsm utapeli wake na kumleta yule jamaa wa perepereche wa clouds wambie itawatokea puani.

Nawaomba upesi / haraka mno PCCB na TISS ' walimulike ' hili vizuri kwani ninavyoliona huyu GSM atakuja ' Kuichafua ' Ligi na hadi Nchi yetu pia.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,858
2,000
Pesa huna unapiga kelele hapa,mkiambiwa mchangie timu mnapotea.

Mwambie huyo GSM wako kuwa Tanzania hii ya sasa ni ya Rais Dkt. Magufuli hivyo huo Usamjo ( Utapeli ) wake kwa Yanga SC hatoliweza Kamwe.
 
Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,021
2,000
GENTAMYCINE usiharibu mipango ya watu, hivi unafahamu baada ya Manji kuondoka yule msaafu aliyekuwa high table jana ndiye mmiliki halali wa Yanga?

Sina uhakika na hili kuhusiana na kuondoka kwa Manji Tanzania. Niishie hapo
 
MTU ALIYE NYIKANI

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
346
500
GSM ni mfanyabiashara, kwa hiyo kwa vyovyote vile pia anazingatia maslahi yake, Mimi ni mwanachama mtiifu wa Yanga ninachokihitaji ni burudani tu ya mpira maana hayo mambo ya fedha hayanihusu kwani hakuna siku tulishawahi kupata gawio kutoka Yanga tukiwa kama wanachama kabla hata ya kuja hao GSM, hivyo basi GSM waendelee tu, cha msingi tunataka ushindi na mpira mzuri
 
macjay

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
343
500
Yanga bwana kitu kidogo tu .................John Zigzaga Makelele hatusikilizan
 
wayneogoa

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
204
250
Nawaomba upesi / haraka mno PCCB na TISS ' walimulike ' hili vizuri kwani ninavyoliona huyu GSM atakuja ' Kuichafua ' Ligi na hadi Nchi yetu pia.
Una njaa Tumboni mpaka kichwani kwa ufupi hakuna deal yoyote inaweza ikafanyika bila tiss kujua ingekua na ubaya ingeishia juu kwa juu wala usingeiskia pole najua unafaidika na get collection mirija imekatwa njaa tu zinakusumbua unataka timu itembeze bakuli kila siku uchangie mia 2 ?we kwl zuzu hujui mpira wa kisasa Yanga kuna wataam wengi hakuna mazuzu pale wanajua wanachofanya acheni uchumia tumbo
 
Kinjeketile

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
985
1,000
Tukupe wewe basi uuze huo Unga. Ukita kula sharti uliwe kama hutaki kuliwa achana na pesa za watu ubaki na umasikini wako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom