Waziri Ashatu, Wasemaji wa Yanga na Azam Kamwe na Ibwe acheni Kutuchosha wenye Akili kuhusu Jezi Feki za Chang'ombe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,681
109,092
Tunajua huu ni Mkakati wa Kimakusudi wa Kumchafua Mshindani mpya kutoka Klabu Moja Kubwa nchini kwakuwa amefanya vyema sana Sokoni.

Ali Kamwe ( Msemaji wa Yanga SC ) nitafurahi zaidi nikikuona Hasira hii hii ya Kufeki ( Drama ) uliyoionyesha katika kupatikana Jezi Feki hizo za Tsh Bilioni 10 utaihamishia katika Kampuni ya GSM ( ambao ndiyo Wadhamini wenu Wakuu ) na Kuwauliza ni kwanini katika Bei ya Tsh 40,000/= ya Jezi zenu Yanga SC inachukua Tsh 1,800/= tu inayobakia Tsh 38,200/= inaenda ( inachukuliwa ) na GSM.

Kwako Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji kwa kwa Kukurupuka Kwako na kwa ulichokifanya leo umenifanya niamini kuwa huenda 75% ya PhD Holders nchini Tanzania ni Bogus wa Kutukuka ila huenda hawajijui.

Hivi Wewe Waziri inawezekana kweli kukawa na Shehena ( Consignment ) ile ya Jezi Feki za Vilabu Vikubwa nchini Tanzania halafu Watu wa Customs, TRA na hata wa TISS ( walio both penetrated and seconded pale TPA ) wasijue au hata na Wao ( baadhi yao ) kwa Utovu wao wa Maadili wasihusike?

Nina mengi juu ya hili ila niseme acheni tafadhali kutupotezea muda na hii Movie yenu hii ya Kipumbavu ( Kipopoma ) na Kishamba ( Kimbugira ) juu ya hili Sakata. Hapa mmewapata wengi Wasiojua Kufikiri ila Wachache tuliobarikiwa Upeo mkubwa tumechagua Kuwadharau zaidi na kuwaona ni kama vile labda mmechanganyikiwa.

Na mwambieni Ali Kamwe ( Msemaji wa Yanga SC ) kuwa GENTAMYCINE nasema hakuna Mzigo wa Tsh Bilioni 10 wa Jezi Feki uliokamatwa na kama ukiwa na Gharama Kubwa ni Tsh Milioni 500/= mpaka Tsh Bilioni 1 tu.

Na namalizia kwa kusema kuwa hawa Matajiri wakubwa wa hivi Vilabu Vikubwa Viwili nchini hawavifaidishi Kiuchumi hivyo Vilabu bali Wao ndiyo kwa 85% Wanafaidika navyo.

Kwa mfano huku Simba SC Kwangu ( ninakokushabikia ) Akaunti ya Klabu ina Fedha Kiduchu na huenda hata Usikute chochote ila katika Akaunti ya Tajiri Kutwa inapumua tu kwa Mifedha.

Ila Matajiri hawa Wanalindwa na Mamlaka na ya Chama kwakuwa ndiyo Wanaisaidia na Wanakichangia pakubwa katika Kampeni na Kuirejesha tena Madarakani.

Nchi Kutwa imejaa Usanii tupu tu.

Cc: Msanii, Mpaji Mungu
 
Umeandika mule mule ....Kuna ushuzi unasambazwa Kwa nguvu ...haiwezekani jezi feki zikamatwe zenye thamank ya bil 10, kama feki zimekamatwa bili 10 je zisizo feki zitakuwa za bei Gani ikiwa Simba wanapata gawio la Bil 2 Kwa mwaka kutoka Kwa Sandalend, na Yanga Buku 1500 Kwa jezi!?
 
Umeandika mule mule ....Kuna ushuzi unasambazwa Kwa nguvu ...haiwezekani jezi feki zikamatwe zenye thamank ya bil 10, kama feki zimekamatwa bili 10 je zisizo feki zitakuwa za bei Gani ikiwa Simba wanapata gawio la Bil 2 Kwa mwaka kutoka Kwa sandalend, na Yanga Buku 1500 Kwa jezi!?
Nashukuru kwa Kunielewa juu ya nilichokiandika. Hapa Kit Sponsor wa Simba SC Sandaland The Only One anataka Kuchafuliwa na Kuharibiwa Biashara yake kwakuwa ameonekana ni Mshindani mkubwa na mwenye Ubunifu katika Industry kumzidi Wao.
 
Ali Kamwe kwanza unaingilia uhuru wa vyombo vya ulinzi na usalama katika kushughulikia hili suala.

Nilishangaa jana eti anaenda kuwahoji waliokamatwa na jezi feki,hivi kwa akili tu ya kawaida mahojiano hayo kama yangefanyika baina ya msemaji na hao waliokamatwa na jezi yangesaidia nini katika suala zima la utekelezaji wa taratibu za kisheria ili kuwafikisha watuhumiwa mahakamani?

Ali Kamwe ilitakiwa awapatie taarifa wanachama wake kwa kile kinachoendelea,yaani kama wamepelekwa mahakamani au katika vyombo vingine vya kisheria lakini syo yeye eti achukue jukumu la kufanya mahojiano na waliokamatwa na jezi
 
Back
Top Bottom